Ushiriki wa watz big brother na matumizi ya bendera ya taifa

Marumeso

JF-Expert Member
Oct 3, 2009
1,410
1,313
Suala la ushiriki wa watanzania wenzetu kwenye shindano la bigbrother lilikwisha jadiliwa bungeni na Serikali ilieleza kuwa hao washiriki wanajiwakilisha wenyewe na kuwa washiriki hao hawaiwakilishi nchi. Tatizo langu ni pale wakati wa ushiriki kwenye shindano hili wawakilishi hutambulishwa kwa utaifa wao na mara zote wanakuwa na bendera za nchi zao mikononi.

Najiuliza iwapo watu hawa hawatuwakilishi watanzania inakuwaje wanakuwa na bendera ya taifa? Bendera ya taifa kwa ufaham wangu ni moja ya alama muhimu ya utambulisho wa taifa na kamwe sio kitu cha mchezomchezo. Kama Serikali imekwisha sema hawa wenzetu hawatuwakilishi, je na hizo bendera zinafikaje mikononi mwao.

Na je hivi kwa kitu muhimu kama bendera ya taifa hivi hakuna protokali zinazoongoza matumizi yake sahihi au unaweza kuchukua bendera ya taifa na kuitumia popote pale utakavyo.
 
wewe bwana waache watu waitangaze nchi....hao mafisadi wanaouza wanama na bandari si wanatembea na bendera kila siku na wengine hadi wanalala nazo.
 
wewe bwana waache watu waitangaze nchi....hao mafisadi wanaouza wanama na bandari si wanatembea na bendera kila siku na wengine hadi wanalala nazo.

Mkuu kosa halisahihishwi kwa kufanya kosa!
 
mkuu bendera sio issue

mimi nina bendera hadi kwenye begi yangu ya toilet nikisafiri, ni alama ya utaifa/uraia/uzalendo tu
 
Si kila abebaye/ashikaye bendera anaiwakilisha TZ. Wawakilisha huwa wanakbidhiwa bendera na kiongozi wa serikali
 
mkuu bendera sio issue

mimi nina bendera hadi kwenye begi yangu ya toilet nikisafiri, ni alama ya utaifa/uraia/uzalendo tu

Kitu kinachotambulisha utaifa wako SIO ISSUE? TAFAKARI!
 
Si kila abebaye/ashikaye bendera anaiwakilisha TZ. Wawakilisha huwa wanakbidhiwa bendera na kiongozi wa serikali

Hawa wanamuwakilisha nani basi? Wakati na wao wana bendera zilezile kama za hao wanaokabidhiwa?
 
Muda wa kuangalia pilau live live umefika. Nakumbuka sehemu panapoitwa Baruti, kipindi nasoma Musoma tech ilikua maarufu kwa Pilau.
 
Kila Mtanzania ana haki ya kubeba bendera, hii ni non issue.
 
Muda wa kuangalia pilau live live umefika. Nakumbuka sehemu panapoitwa Baruti, kipindi nasoma Musoma tech ilikua maarufu kwa Pilau.

Pale kwa bry unavuka kidogo stend ya hyce ukiwa unaelekea nyasho. Kijana umenikumbusha mbali sana.
 
Mi bado nashindwa kuelewa watu kama Luck ambao wana mawazo kama yako. Bendera si ya serikali iliyopo madarakani bendera ni ya nchi na ni mali ya wananchi wake wote. Kila mwananchi wa tanzania ana haki ya kuwa nayo na wajibu wa kuitunza na kuitumia kadri anavyoona ili mradi asi-abuse the true meaning of bendera. Sasa hiyo ni ngumu sana kuelewa?au ndo mwataka kila kitu kiandikwe kwenye katiba? Hata wewe Luck ukitaka bendera nenda bohari kuu pale utapata as simple as that. Utundike dirishani au ujifunike kama shuka la kimasai (proud of being tanzanian) au usafiri nayo no one will ask you unless ujiulize mwenyewe kama unavyouliza sasa.
 
Una uhakika na unachokisema au unafurahisha kijiwe? Mbona mara kibao tunashuhudia wawakilishi (wa ukweli) mbalimbali wakikabidhiwa bendera formally!

No Research No Right To Speak
 
Suala la ushiriki wa watanzania wenzetu kwenye shindano la bigbrother lilikwisha jadiliwa bungeni na Serikali ilieleza kuwa hao washiriki wanajiwakilisha wenyewe na kuwa washiriki hao hawaiwakilishi nchi.Tatizo langu ni pale wakati wa ushiriki kwenye shindano hili wawakilishi hutambulishwa kwa utaifa wao na mara zote wanakuwa na bendera za nchi zao mikononi! Najiuliza iwapo watu hawa hawatuwakilishi watanzania inakuwaje wanakuwa na bendera ya taifa? Bendera ya taifa kwa ufaham wangu ni moja ya alama muhimu ya utambulisho wa taifa na kamwe sio kitu cha mchezomchezo. Kama Serikali imekwisha sema hawa wenzetu hawatuwakilishi, je na hizo bendera zinafikaje mikononi mwao. Na je hivi kwa kitu muhimu kama bendera ya taifa hivi hakuna protokali zinazoongoza matumizi yake sahihi au unaweza kuchukua bendera ya taifa na kuitumia popote pale utakavyo.

Unajua hauwezi ukamkana m-Tanzania mwenzio kwa kigezo tu kwamba anachoenda kukiwakilisha ni msimamo tofauti na wengine au serikali.
Na hauwezi kumtenganisha mtanzania na Bendera ya nchi yake wala kumzuia mtanzania asibebe bendera ya nchi yake kokote aendako.Jambo la msingi ni kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Bendera wakati umeibeba.
Mbona wa Marekani wana hadi leso za Bendera za nchi zao hadi katika michezo ya olimpiki tumeona watu wamevaa chupi za Bendera za nchi zao,au Tanzania sheria ni tofauti na kwingineko?.
Kama issue ni kuidhalilisha nchi na utaifa basi huko huko yanapofanyikia mashindano mabalozi wachukue hatua na wakirudi washitakiwe kwa mambo waliofanya huko ng'ambo au wafutiwe uraia,sheria hizo zipo.
Mfano:- OSAMA BIN LADENI alinyang'anywa uraia baada ya kuonekana anafanya mambo hayafai katika jamii zao.
 
unajua kiukweli TZ bendera ya taifa tunaichukulia kitu cha mchezo mchezo kama wimbo wa taifa ukiwa unaimbwa bungeni wabunge wanatumia wakati ule kusalimiana na hata uzima simu hivi itakuja kuwa bendera ya taifa kutumika inavyotakiwa. kiukweli hatujui ni taasisi gani ambayo inawapa hawa wawakilishi wa kujiongesha uchi dunia nzima kuwa Tz inatembea uchi kwenye lilejumba
 
watu wana bendera na wanafutia makamasi we unajali huyo aliye nje ya nchi...BENDERA!!! sema jingine siyo bendera.
 
Back
Top Bottom