Ushiriki wa siasa za matusi na kejeli ndani ya bunge unaofanywa na wanasia wa CCM... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushiriki wa siasa za matusi na kejeli ndani ya bunge unaofanywa na wanasia wa CCM...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndulungu, Jun 19, 2012.

 1. Ndulungu

  Ndulungu Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana tumeshudia vituko bungeni baada ya mbunge wa jimbo la iramba magharibi mh. mwigulu nchemba na mbunge jimbo la mbinga magharibi john komba wakitoa kauli za kejeli na lugha za matusi ndani ya bunge.kwa wote tulioangalia bunge jana kupia tbc ccm tumeshuhudia vimbwanga vya wanasisa hao uchwara wakishindwa kujibu hoja zilizotolewa na kambi ya upinzani na kuishia kutoa kauli za kashfa,kejeli ma matusi kwa chama na viongozi wa chadema sina haja ya kuyanukuu matusi yaliotolewa na wanasiasa hao ila ntaungana nao kwa hoja walioitoa ya kabla ya kuingia bungeni ni vizuri wabunge wakapimwa akili na imani kwa asilimia mia moja wa kwanza watakao gundulika na vichaa ni namba 1 atakua lusinde 2 atakua mwigulu nchemba na 3 atakua john enewei niishie hapo naomba nihitimishe kwa kusema wakati wa ccm(magamba)kuendelea kutawala umekwisha matusi kashfa na kejeli siku zote hazijengi hivyo ni vyema ccm wakajiandaa kukabidhi nchi kwa chama ambocho ni tumaini la watanzania
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wnajua hawana la kuongea ndo maana wanakimbilia kutukana..kwao matusi ,wizi ,uwongo na ngono ni sehemu ya maisha yao na wamekuwa wanarithiswa hayo toka muda mrefu sana kwenye vizazi vya uongozi vilivopita..so hakuna jipya hapo
   
 3. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  kwa mujibu wa MTANZANIA,ya leo tarehe 19 06 2012, ukurasa wa pili, pamoja na kutoa matusi makali Bungeni,MWENYEKITI hakuchukua hatua yoyote ,....Waziri wa Sheria na Katiba Mathias Chikawe,Waziri wa Elimu na Mafunzo Philipo Mulugo, na Waziri wa Nchi(soma DOLA) Ofisi ya Rais(SOMA IKULU), Mahusiano na Uratibu,walionekana wakimtuza NCHEMBA kwa VISENTI,kwa lugha alizotumia akichangia Bajeti ya Upinzani!
  Kama bado kuna mwenye imani na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi,basi ana roho ngumu kuliko mwenda wazimu yeyote.
  Tujihadhari maana wakikosa nchi watajilipua kwa mibomu na kuzidi kuharibu nchi hii!
   
 4. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ni vyema waendelee na matusi yao kwani wanainchi ndio wataamua nani ni kichaa, CDM asilani wasiingie kwenye mtego huo wa kitoto, wasijibu hayo matusi asilani bali watengeneze Nondo/Hoja ambazo watu watapima na kutoa jibu nani ni pumba na nani ni mchele, Kuhusu naibu spika kuwaacha watukane mie nafikiri ni jambo jema kwa CDM kwani linawapunguzia credibility yao CCM kwenye jamii yetu iliyostaarabika, hawa weenzetu ni wepesi wa kusahau kwani kosa walilolifanya Arumeru bado wanalirudia Bungeni na watu ni wale wale akina Bajaji et al,

  Napenda kurudia tena na hasa ujumbe huu uwafikie viongozi wa CDM kuwa KAMWE MSIINGIE KWENYE MTEGO WA LUGHA CHAFU BALI GONGENI HOJA ZINAZOKATA MPAKA KWENYE MIFUPA YAO...PROVOKE THEM, DO NOT ABUSE THEN PEOPLE WILL ASSESS
   
 5. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  kejeli alizokuwa akitoa lisu kwa ccm hamkuziona? Au mnbngali upande mmoja
   
 6. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Wametokwa na mapovu vya kutosha! Wameacha hoja wamejikita kwenye mashambulizi binafsi. Hili litaendelea kuwa tatizo na kichochea kwa wabunge wa ccm kuzidi kupoteza credibility kwenye jamii na wananchi wanao pigika kwa hali ngumu ya maisha.
   
 7. gmosha48

  gmosha48 JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Uzuri siku hizi mambo yako hadharani. Hata sisi tulioko huku mwisho wa reli tunajionea laivu kabisa jinsi jamaa wanavyotokota. 2015 mwisho wao!
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Wakuu bajeti inapowasilishwabungeni huwa ni kama hitimisho lamchakato mrefu na wa kisayansi ambao umehusisha wadau wengi sana na zaidiwaheshimiwa wabunge wenyewe. Kamati za kudumu za bunge hupitia bajeti za wizarahusika . Katika vikao baina ya kamati ya kudumu ya bunge na watendajiwaandamizi wa wizara husika wakiongozwa na waziri wao. Waziri huwasilisha rasmuya bajeti ya wizara yake, wabunge huuliza maswali na kutaka ufafanuzi katikamambo ambayo wanadhani hayaeleweki vizuri kwao. Lakini pia wabunge hutoamapendekezo kadhaa ambayo yanaingizwa moja kwa moja katika bajeti.Kamati ya kudumu ya bunge yafedha na uchumi ina jukumu la kuipitia bajeti kuu ya serikali katika kikao chapamoja baina ya watendaji waandamizi wa wizara ya fedha na wajumbe wa kamati yafedha ya bunge. Kwa msingi huo bajeti inayoendelea kujadiliwa bungeni hivi sasainafahamika vema kwa wabunge wote na wote wameshiriki katika kuiunda kutokanana michango ya wabunge katika vikao baina ya wabunge na watendaji wa serikali.Hii ndiyo sababu nikasema tangu mwanzo kuwa bajeti ni mchakato mrefu ambao umehusisha wabunge kwa kina kablahaijawasilishwa bungeni. Kila mbunge anaruhusiwa kuhudhuria vikao vya kamatiyoyote ya bunge hata ambayo haimhusu lengo likiwa ni kumpatia fursa kila mbungekujua kwa kina kinachoendelea serikalini.Jambo la kushangaza ni jazbainayoonyeshwa na wabunge wa pande zote wakati wa kujadili bajeti hii as if nijambo wanaloliona kwa mara ya kwanza. Wabunge wanatumia nguvu nyingi kupinga bajeti hii ilhali walipata fursaya kuipitia kwa kina kabla haijawasilishwa bungeni, huu ni usanii wa kiwangocha juu sana. Hivyo wabunge wetu acheni usanii hii bajeti mnaijua vema namlishaipitia kabla haijawasilishwa bungeni.
   
 9. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Ingekuwa enzi za mchonga,hao ndio walikuwa wanaitwa ikulu kwa siri na kuchalazwa bakora kama watoto.
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  zama za kulindana zimeshapitwa na wakati na wanachi wanaona wazi
  CCm wanalindana hata kwa mambo ya kijinga
  kama leo Lusinde na elimu yake ya std 7 anasema chadema wamerudia bajeti ya mwaka jana
  na kuianza kuiponda badala ya kuchangia bajeti na kuianisha na mazingira halisi ya waliomchagua
  CCm wamepoteza dira na mwelekeo sasa wamebaki kutukana na kuzomea
  kiama chao kimefika chadema na upinzani wote kazi uzi chukueni nchi 2015
   
 11. M

  MUNYAMAKWA Member

  #11
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama kweli "siasa ni mchezo mchafu",siwalaumu sana hawa Waheshimiwa wabunge wetu kwa kinachoendelea mjengoni, lakini tukumbuke imeandikwa kwenye vitabu vitakatifu akupigae shavu la kushoto mgeuzie la kulia.Pia kuna viashiria vya watu walioishiwa na hoja na badala yake wanatafuta wenzao midomoni (provoke) ili wapate la kuongea.Lakini upande mwingine wa shillingi ni kwamba "you cannot push a boat while you are inside" tunatofautiana jinsi ya kutoa ujumbe, walengwa walichukue hili kama changamoto kwao wakae waone wapi wameboronga ili kuboresha,wazitumie hizi wanazoziona kama kejeli kwa ajili ya kuboresha sio kujenga uadui.Hii ndo demokrasia ya kweli, lazima tofauti iwepo kimtizamo miongoni mwa vyama vyote pasipo kuvuruga amani ya nchi yetu.Nyie mnataka msemwe kwa mazuri tu!Acheni wawape uspoon bila wao kujua
   
 12. a

  andrews JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  1 CD YA UKABILA
  2 CD YA UDINI
  3 CD YA UKANDA
  KWA KUWA WATANZANIA WENGI NI WAELEWA CCM IMEANGUKIA PABAYA KWA KUKOSA WANUNUZI WARNING:SASA CCM INAWATUMIA UAMSHO KUWAGAWA WATANZANIA BILA KUJUA WAZANZIBARI WAMEINGIZWA MJINI HIYO NI HUJUMA YA CCM KUOGOPA MABADILIKO YANAYOKUJA 2015 THE ONLY WAY NI KUWAGAWA WATANZANIA KWA KUWATUMIA AKINA SHEIKH MPONDA NA WAJINGA WENZAKE
  :bump:
   
 13. babujii

  babujii Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  tatizo waheshimiwa wameshikwa pabaya, fikiria mjanja akikuwahi na kukukwida sehemu nyeti utaongea kiarabu,kihindi kiyunani,kichina,kimatengo kwa wakati mmoja hata kama lugha hizo huzijui.
   
Loading...