figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Kuwa Profesa si kuwa Tajiri.
Uprofesa ni daraja katika taaluma.
Kuwa Profesa hakukupi nafasi HAZINA wala kukupa nafasi katika biashara. Kuna Maprofesa wa kutibu macho, kuimba, siasa, sheria, elimu,atomiki n.k. Vyote havina nafasi katika utajiri! Ni kweli wapo wengine ni matajiri wa kuweza kuwekeza huku lakini ile sheria ya UHUJUMU UCHUMI ya 1983 iliwatisha wengi ambao walikwishaanza kurudi huku kuwekeza.
Watu wengi wa Kagera (matajiri) waliwekwa rumande kwa zaidi ya mwaka. Jela ilijaa wafanya biashara hadi wengine walilazwa bwalo la Polisi Buyekera. Watu walimwaga mali zao kwenye mito na wengi wawekezaji wa miundombinu kama mabus gari ndogo walinyanganywa mali zao. Uhujumi huo uliwakamata hatawatu waliokutwa na laki, gari za mitumba na ajabu zaidi hata walioneemeka kupitia mikopo ya karadha(taasisi ya kukopesha ya serikali) wakaweza kununua malori wote gao waliwekwa mahabusi.
Yuko mmoja huko Kagoma Muleba alijijengea ghorofa yake naye aliwekwa ndani. Biashara zake ilikuwa Dar! Mkoa ulikuwa unang'ara na ghafla taa ikazimwa.
Sina la kufanya lakini sintosahau kumkumbuka Mkuu wa Mkoa wa Kagera Lt. Col. NSA KAISI 1981 -1987 kwa madhara aliyoyaleta hapa Kagera! VIJANA KAGERA haikuwa kama ilivyo sasa.
Tulikuwa tunaruka hewani! Niliwaambia kuhusu mikakati ya kuudhoofisha Mkoa kwa ujumla. Yaliyofanyika Kagera hayakufanyika mkoa mwingine wowote Tanzania. Ilikuwa kama hiyo Sheria ilitungwa kwa ajili ya kagera! Vijana mnaosema Kagera kuna fitna, si kweli! Nitajieni mkoa ambao hauna fitna! Anti-Economic Sabotage act 1983 ndiye mchawi wa Kagera.
Niwaambie kitu kimoja Tukiwa shule huko katika seminar presentation nilimbishia PhD holder darasani nikipinga kwamba sheria ya Uhujumu Uchumi ilikuwa ni sheria ya kitaifa kama nyingine. Katika presentation hiyo nikiwa ni presenter wa kundi letu wenzangu(wanafunzi) walinikana kabisa lakini mimi nilistick katika ukweli huo kwamba ile sheria ilikuwa mkakati wa Mkoa mmoja na kuroa impirical evidences. Mnajua? Presentation yetu ilipata 8/10 ! Wenzangu walinishangaa sana. Kagera hakuna fitna bali tumebanwa sana licha ya kuwa tunapakana na mataifa manne.
Eti Kagera tunafanya Magendo kuliko mikoa ya Kaskazini kusini na magharibi! Wasiofahamu:-
Makao Makuu ya Jimbo la Ziwa yalikuwa Bukoba ikiviongoza viwilaya vya Mwanza Mara shinyanga! Leo nenda Kahama Geita uangalie!!
Mifano mingine mumeiona wenyewe niwakumbushe ? "Tulipotandikwa na tetemeko la ardhi ni fitna za Kagera? Je hatukusikia lolote?
Nimechoka! Mengine Mtajaza wenyewe
Baada ya Sokoine kutembelea Mkoa Kagera na kufika Bohari ya Mkoa alitaka aonyeshwe mali nyingi iliyokamatwa Kagera wakati wa Uhujumu Uchumi. Hakukuta mali ye ye thamani iliyokuwa ikitangazwa redioni iliyofikia thamani ya mabilioni.
Hakuikuta na inasemekana alitaka maelezo ya hiyo mali na kuamuru RC wakutane Bunge Dodoma akiwa na taarifa ya mali ya uhujumu uchumi. Aliondoka na haikuwezekana kwa sababu alipatwa ajali "Dumila" na kufariki pale pale.