Free ideas
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 3,456
- 1,932
Hvhgjjkk
Mfano; ndugu Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga alidai kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa viboko huku mwanae wa kiume (11) akishuhudia.
Mfano; katika Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga, mwanamke mmoja alidai kubakwa na Askari wawili (2) wa Operesheni Tokomeza Ujangili mida ya usiku. Vilevile, mama mmoja mkazi wa Kata ya Matongo Wilayani Bariadi, alibakwa na askari watatu (3) wa Operesheni Tokomeza Ujangili huku akiwa ameshikiwa mtutu wa bunduki
Diwani wa Kata ya Sakasaka wilaya ya Meatu Ndg. Peter Samwel, alidai kuadhibiwa akiwa mtupu kwa kupewa adhabu za kijeshi kama kuninginizwa kichwa chini miguu juu, kupigwa kwa vyuma na kulazimishwa kufanya mapenzi na mti.
Mfano; katika Wilaya ya Itilima,Kijiji cha Mbogo Ndg Sita Rumala alidai kupigwa na kuvunjwa mkono alionesha wajumbe mkono uliokuwa umefungwa bandeji ngumu (P.O.P).
Ndugu Munanka Machumbe (24) ambaye ni bubu alipigwa risasi 3 zilizomjeruhi mapajani na kuharibu sehemu za siri wakati akijaribu kuwahoji Askari wa Operesheni kwa ishara sababu za kumtesa baba yake.
Mheshimiwa Spika, baadhi ya wananchiwalidai kuwa ndugu zao waliteswa kikatili kwa muda mrefu na bila kupatiwa huduma za lazima kama chakula, maji na matibabu (siku 1 -2) hadi mauti yalipowafika. Kwa mfano Ndg. Kipara Issa wa Wilaya ya Kaliua na ndugu Emiliana Gasper Maro wa Gallapo, Wilaya ya Babati
wengine waliodaiwa kupoteza maisha wakati wa Operesheni Tokomeza ni Ndg. Wegesa Kirigiti wa Kijiji cha Remagwe na Ndg. Peter Masea wa Kijiji cha Mrito (Tarime), Ndg. Mohamed Buto (Masasi) na Gervas Nzoya (Kasulu).
Pamoja na uthibitisho wa picha zilizotolewa na wananchi kuhusu kuteswa hadi kufa kwa Bi Emiliana Gasper Maro, Serikali kupitia Mkurugenzi wa Wanyamapori ilitoa Taarifa kwa Umma ikipinga Taarifa iliyorushwa na kituo cha luninga cha ITV
Yako juu ya uwezo wangu.
Upo sahihi kabisa na hili tangu mwanzo watu wengi walionya sana kuihusisha JWTZ kwenye shughuli ile lakini serikali haikusikia na matokeo yake ndiyo haya. Tunao polisi wengi sana yanini kuwatumia wanajeshi? huwa sionagi mantiki ya kukimbilia kuwatumia wanajeshi angalia hata kule mtwara walipeleka wanajeshi wakati polisi wapo?!
Kilichoiponza serikali ni kuona "mafanikio" ya JWTZ kwenye kumaliza vurugu kule Mtwara... Lakini wajue kuwa issue ya Mtwara ilikuwa ni very isolated case ambayo hadi sasa hakuna mwenye uhakika imeisha au itaishaje...
Kiufupi ni kuwa huu ni udhalilishwaji wa jeshi la ulinzi...
Upo sahihi kabisa na hili tangu mwanzo watu wengi walionya sana kuihusisha JWTZ kwenye shughuli ile lakini serikali haikusikia na matokeo yake ndiyo haya. Tunao polisi wengi sana yanini kuwatumia wanajeshi? huwa sionagi mantiki ya kukimbilia kuwatumia wanajeshi angalia hata kule mtwara walipeleka wanajeshi wakati polisi wapo?!
Wanatakiwa wahusika wafunguliwe kesi kwa mahakama malumu kama wao walivyokwenda na mahakimu huko kwenye tokomeza ujangili ili hukumu zao zifanyike mda malumu kama
Ripoti ya kule Mtwara nayo ina madhila mabaya kwa mujibu wa Mtatiro leo Star Tv