Ushiriki wa JWTZ katika 'Operesheni Tokomeza'

Upo sahihi kabisa na hili tangu mwanzo watu wengi walionya sana kuihusisha JWTZ kwenye shughuli ile lakini serikali haikusikia na matokeo yake ndiyo haya. Tunao polisi wengi sana yanini kuwatumia wanajeshi? huwa sionagi mantiki ya kukimbilia kuwatumia wanajeshi angalia hata kule mtwara walipeleka wanajeshi wakati polisi wapo?!
 
Tembo wauawe na Kinana kupigwa wapigwe Wanayalukolo hii inakuja kweli.

CCM kweli ni Chama Cha Majambazi.

JWTZ limekuwa jeshi la kutekeleza Ilani za CCM na si kulinda nchi.

Mtwara na Lindi zimegeuzwa kambi za jeshi na wananchi wote wako Mahabusu, Mkuu kiguu na njia sasa hivi yupo hapa kusafishwa KISUSIO ili afya imrudie tena.

Kama kagasheki ni mzigo kwa kutumia jeshi kulinda akina Kinana, Kikwete naye ni ZIGO lisilo bebeka kwa kutumia Brigedi nzima kulinda Biashara za Wachina kutimiza ahadi baada ya shingo ya kijana wake kukoswa koswa huko China.

Mwamunyange naye aachie ngazi.

Sasa hivi JWTZ wanadhani adui yao namba moja ni RAIA wote wa Tanzania.

Mipaka yetu ipo kama chekecheke kwa kuvuja wao wako BIZE kuua raia wasio na hatia ndani ya nchi.
 
Kilichoiponza serikali ni kuona "mafanikio" ya JWTZ kwenye kumaliza vurugu kule Mtwara... Lakini wajue kuwa issue ya Mtwara ilikuwa ni very isolated case ambayo hadi sasa hakuna mwenye uhakika imeisha au itaishaje...

Kiufupi ni kuwa huu ni udhalilishwaji wa jeshi la ulinzi...

Hii ndiyo nidhamu ya JWTZ

Mfano; ndugu Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga alidai kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa viboko huku mwanae wa kiume (11) akishuhudia.

Mfano; katika Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga, mwanamke mmoja alidai kubakwa na Askari wawili (2) wa Operesheni Tokomeza Ujangili mida ya usiku. Vilevile, mama mmoja mkazi wa Kata ya Matongo Wilayani Bariadi, alibakwa na askari watatu (3) wa Operesheni Tokomeza Ujangili huku akiwa ameshikiwa mtutu wa bunduki

Diwani wa Kata ya Sakasaka wilaya ya Meatu Ndg. Peter Samwel, alidai kuadhibiwa akiwa mtupu kwa kupewa adhabu za kijeshi kama kuning’inizwa kichwa chini miguu juu, kupigwa kwa vyuma na kulazimishwa kufanya mapenzi na mti.

Mfano; katika Wilaya ya Itilima,Kijiji cha Mbogo Ndg Sita Rumala alidai kupigwa na kuvunjwa mkono alionesha wajumbe mkono uliokuwa umefungwa bandeji ngumu (P.O.P).

Ndugu Munanka Machumbe (24) ambaye ni bubu alipigwa risasi 3 zilizomjeruhi mapajani na kuharibu sehemu za siri wakati akijaribu kuwahoji Askari wa Operesheni kwa ishara sababu za kumtesa baba yake.

Mheshimiwa Spika, baadhi ya wananchiwalidai kuwa ndugu zao waliteswa kikatili kwa muda mrefu na bila kupatiwa huduma za lazima kama chakula, maji na matibabu (siku 1 -2) hadi mauti yalipowafika. Kwa mfano Ndg. Kipara Issa wa Wilaya ya Kaliua na ndugu Emiliana Gasper Maro wa Gallapo, Wilaya ya Babati

wengine waliodaiwa kupoteza maisha wakati wa Operesheni Tokomeza ni Ndg. Wegesa Kirigiti wa Kijiji cha Remagwe na Ndg. Peter Masea wa Kijiji cha Mrito (Tarime), Ndg. Mohamed Buto (Masasi) na Gervas Nzoya (Kasulu).

Pamoja na uthibitisho wa picha zilizotolewa na wananchi kuhusu kuteswa hadi kufa kwa Bi Emiliana Gasper Maro, Serikali kupitia Mkurugenzi wa Wanyamapori ilitoa Taarifa kwa Umma ikipinga Taarifa iliyorushwa na kituo cha luninga cha ITV

Hii ndiyo nidhamu inayosifiwa ya jeshi letu; JWTZ...
 
Mkuu Free ideas,

Una haki ya kusema hivyo. Lakini umeeleza jeshini hakuna cha dscussion kama ilivyoagizwa ni hivyo, sasa SWALA ni kwamba hawakuelzwa majukumu yao ktk hiyo operation. Kama wanajeshi wanafanya walichoelezwa na makamanda wao na hawawezi fanya vingine basi wangepewa very clear mission basi haya mambo yasingetokea. Nina wasiwasi na hao viongozi wao hasa mkuu wa operation. Hawakuelezwa what should be achieved and under which conditions!

Kwa kifupi ni kwamba hata iwe jeshi kama kuna clear mission haya makosa hayawezi kutokea. Pili lazima tujue na viguma kwa watanzania kufanya vitu vya kutumia akiri na kuwaza zaidi. Watanzania hasa wale ambao wako ktk nagazi za uongozi iwe siasa au hata nje ya hapo SWALA LA KUTUMIA AKIRI NYINGI NA KUWAZA HALIPO what counts first ni je kuna CHOCHOTE HAPA!!!!!!!!

IT IS A SHAME KUWA NA WASOMI AMBAO HAWAWEZI KUTUMIA AKILI KIDOGO KUFIKIRI KABLA YA KUTENDA KITU. WASOMI WETU THEY CANNOT DELIVER ANYTHING AT ALL. HII NDIYO TANZANIA YA SASA. MWALIMU NYERERE MASIKINI AMEONDOKA NA TANZANIA TUNAYOYIJUA!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Upo sahihi kabisa na hili tangu mwanzo watu wengi walionya sana kuihusisha JWTZ kwenye shughuli ile lakini serikali haikusikia na matokeo yake ndiyo haya. Tunao polisi wengi sana yanini kuwatumia wanajeshi? huwa sionagi mantiki ya kukimbilia kuwatumia wanajeshi angalia hata kule mtwara walipeleka wanajeshi wakati polisi wapo?!

Hapa rais hawezi kukwepa lawama kwa sababu jeshi lisingeweza kutumika bila idhini yake.
 
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinatumika na Serikali iliyopo madarakani kulinda maslahi ya wachache,issue je wahusika wakubwa wa ujangili wameshughulikiwa,wakuu wa idara husika zilizoendesha operesheni wameshughulikiwa?Mnafaham kuwa baadhi ya wakuu wa idara kwny operesheni hyo wamepandishwa vyeo? Hii ndo TAnzania yetu ya kuwajibishwa wachache kwa maslahi ya wachache pia
 
Nakumbuka issue ya west gate nchini Kenya Jinsi wanajeshi walivyoiendesha badaae wakaiba vitu Ndani na kulilipua jengo la westgate
 
Kilichoiponza serikali ni kuona "mafanikio" ya JWTZ kwenye kumaliza vurugu kule Mtwara... Lakini wajue kuwa issue ya Mtwara ilikuwa ni very isolated case ambayo hadi sasa hakuna mwenye uhakika imeisha au itaishaje...

Kiufupi ni kuwa huu ni udhalilishwaji wa jeshi la ulinzi...

Nyongeza!

Kama tume itaundwa kuchunguza uvunjwaji haki za binadam ktk fiasco ya Mtwara/Lindi dhidi ya bomba la mafuta itakuwa ni balaa zaidi ya hii ya ripoti ya Lembeli!

Operation ya Mtwara/Lindi iliendana na ubakaji,oporaji wa mali za raia,mauaji na hata kuwekwa vizuizini kwa wale wote walio onyesha kuipinga serikali!

Serikali haitakubali kuunda Tume huru Mtwara!
 
Huu ni udhaifu mkubwa wa CDF Mwamunyange na Kikwete wake!
Upo sahihi kabisa na hili tangu mwanzo watu wengi walionya sana kuihusisha JWTZ kwenye shughuli ile lakini serikali haikusikia na matokeo yake ndiyo haya. Tunao polisi wengi sana yanini kuwatumia wanajeshi? huwa sionagi mantiki ya kukimbilia kuwatumia wanajeshi angalia hata kule mtwara walipeleka wanajeshi wakati polisi wapo?!
 
Wanatakiwa wahusika wafunguliwe kesi kwa mahakama malumu kama wao walivyokwenda na mahakimu huko kwenye tokomeza ujangili ili hukumu zao zifanyike mda malumu kama
 
Wanatakiwa wahusika wafunguliwe kesi kwa mahakama malumu kama wao walivyokwenda na mahakimu huko kwenye tokomeza ujangili ili hukumu zao zifanyike mda malumu kama

Mi nimesoma tena na tena ile taarifa ya Lembeli, kwa kweli itakuwa ni aibu kama serikali haitawachukulia hatua kali hao watesaji na wauaji...
 
ccm na serikali yao hawana cha kutafta mtu wa kumtupia hili zigo kungekuwa na kaupenyo ungesikia chadema wanahusika,lakini kwa sasa jeshi lao ndo limeua.Shame on you gambaz
 
Serikali yoyote ile inayoamua kulitumia jeshi kupambana na wananchi wake ni ya kidhalimu na ya kifashisti. Jemadari anayeliruhusu jeshi kutumika dhidi ya wananchi wake ni wa kuchukuliwa hatua ikiwemo kuvuliwa cheo na kufikishwa mahakamani...huyo ni adui wa taifa na hana tofauti na kamanda wa jeshi la uvamizi. Kiongozi yeyote wa nchi anayeamuru jesho kufanya uovu kama huu ni wa kukamatwa na kufikishwa kwenye mahakama za kimataifa.
 
Ripoti ya kule Mtwara nayo ina madhila mabaya kwa mujibu wa Mtatiro leo Star Tv
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom