Ushirika wa wanasheria na viongozi kughushi hati za kimahakama ni jinai isiyosameheka.

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Kitendo cha mawakili na mkurugenzi wa jiji la Dsm kutumia hati ya mahakama ambayo ni ya kughushi ili kuzuia kufanyika kwa uchaguzi wa meya wa jiji la Dsm ni utovu wa nidhamu na kiburi kilichopindukia dhidi ya haki na demokrasia ya nchi hii.

Mwanasheria kughushi hati ya kimahakama, kuigonga mihuri ya kughushi, kuiwasilisha kwenye mkutano wa wabunge na madiwani na kuwa na uthubutu wa kuisoma mbele ya mkutano wa kumchagua meya wa jiji na hatimaye kuuzuia mkutano huo kwa hati haramu kama hati halali ya zuio la mahakama ni jinai ambayo katika nchi ya utawala wa sheria wote waliohusika na mchongo huo sasa hivi wangekuwa chini ya zuio la polisi.

Nafikiri, kama serikali ya Magufuli itaruhusu ujinga huu wa kucheza na haki za watu kwa kuitumia mahakama ambacho ni chombo cha kutoa haki na kuitafsiri sheria, tutakuwa tunaipeleka pabaya haki na salama ya nchi hii.

Nadhani badala ya kuwapekua viongozi wa Ukawa ingestahili sasa baads ya kuujua ukweli wangushi ndio wapekuliwe huenda wakakutwa na nyaraka nyingine za kughushi.

Ni vema sheria ichukue mkondo wake kwa kuwamata wahusika wote wa sakata hili na kuwafikisha mahakamani mara moja.
 
Aa haa......kumbe hiyo ndio sababu ya manjagu kupekua nyumba ya Mdee,kuna mtu anataka kupoteza ushahidi wa jinai hii
 
Back
Top Bottom