Ushirika uligeuzwa Mtaji Kununua Madaraka Wana-CCM.

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,099
8,727
Habari za IJUMAA YA MOSI wanajamvi?

Nianze kwa kutoa salamu kwa wazee, na vijana wenzangu ambao, kwa namna moja au nyingine tulibahatika kupanga foleni, kusubiri unga wa njano kutoka kwenye maduka yaliyokuwa yanamilikiwa na vyama vya ushirika nchini.

Ushirika..............................................., natumai usomapo uzi huu utakuwa umeitikia, nisiwabague kizazi kilichoitwa cha Jakaya, kizazi ambacho ukikiambia ushirika kinaitikia POWA, nikifundishe kuwa mwitikio wa salamu hiyo, ni PAMOJA TUJENGE UCHUMI.

Baada ya kutoa elimu, bure kama sera ya serikali ya awamu ya tano, niende kwenye msingi wa hoja yangu ya leo, ingawa hoja yangu ni ngumu sana kueleweka kabsa kama wengi wetu hatujui ni nini maana ya ushirika.

kwa ufupi ushirika ni muungano wa hiyari wa wananchi, wanao fanana kimawazo, na hata kishughuli, kwa lengo la kuwezeshana katika mbalimbali za kimaisha.

Maana hii, si sisi, inatokana na uelewa wangu juu ya ushirika, kumbe hata wewe msomaji wangu unaweza kuwa na tafsiri yako kulingana na uelewa wako, na mazingira yanayokuzunguka.

ili kukufanya uelewe vyema, nitakupatia mfano, wa ushirika, ulio undwa na wakulima wa MIWA, ambao wao wanalima MIWA na kuuza kwenye viwanda vya sukari nchini,

ukienda kule MTIBWA, utakuta kuna chama kinaitwa TURIANI, iki kilikuwa chama cha wakulima wa miwa kipindi kile kiwanda hakija binafusishwa kwa wageni chama hiki kilikuwa na nguvu, sanaaa ila baada kiwanda kubinafusishwa, yule Bwana YULE, aliye kichukua nae akaanza kulima miwa, wakulima wale haijulikani kilicho wakumba mpaka wa leo kile chama sasa kimekuwa cha wafanya biashara tu, wakulima hawana lao pale, ukifika pale wanamama na wana baba wazee wanalia sanaaa.

Ndio maana ukienda pale, utakuta Wakina kayunguya wamiliki wakubwa wanao miliki masheri, ndo wenye mikopo mikubwa, lakini pia kwa kuwa na fedha waliweza kujipenyesha na kuwa watawala na sasa ni watuhumiwa namba moja kwa ubadhilifu wa fedha za chama.

Wakulima walio anzisha chama hawana nguvu tena, wamebakia kulalamika hawana lao tena, wanalalamika hata isa zao hazijulikani ziliko.

Chama kingine kiliitwa UDZUNGWA, hiki nacho kama yaliyotokea mtibwa ndiyo yanayokipata chama hiki, vyama sasa vimekuwa vya tabaka la wafanya biashara, wema na wasio wema kwa nchi yao.


Hii, ni mifano tu, ila kwa sababu nimetolea mfano vyama hivi viwili, basi navitumia pia kujengea hoja ya msingi wa andiko langu.

Kwa kizazi cha nyuma kidogo mtaku baliana na mimi kwa viongozi wa chama cha mapinduzi, kwa uwezo wao hasa katika ujio wa jina SACCOSS, ndio wengi walishawishi sana kuanzishwa saccoss kila kona ya nchi hii, kumbe walifanya hivyo baada ya kunusa harufu ya pilau la pesa na sio kwa uzarendo WA kutaka kuwaunganisha wanachi kwa lengo fulani kumbe ilikuwa kuwatumia kujipatia mikopo, na kutafuna fedha za akiba zilizochangwa na wananchi wale.


Viongozi hawa walishawishi uanzishwaji wa vyama vingi kila kona, na kipindi kile sheria haijawakataza kuwa viongozi wa ushirika ndipo walipo tumia fursa hizo kuiba fedha za wananchi walizokuwa wamezichanga na kujiwekea akiba zao.

vyama vingi vya ushrika wapo walio vitumia kupanda ngazi kwa njia ya kununua madaraka kwa kutumia fedha za akiba za wanachama, tutake tusitake walioongoza kwa kufanya hivyo walikuwa ni wanachama wa chama cha mapinduzi.

USHIRIKA umekufa kwa sababu mojawapo, fedha za wananchi nyingi zilitumika katika kufanya kampeni za kununua madaraka,

Pili viongozi hao, waliviingiza vyama hivi, katika Mikopo hisyo tija na pasipo kutoa elimu elimu kwa wanachama, mwishowe vyama viliuziwa majengo yake na mali mbalimbali za vyama na vyama vikuu vingi vimekufa kabsa.

Tukitaka kuufufua ushirika tukubaliane kuwa lazima walio tumia fedha hizo wakamatwe na kuuziwa mali zao, wewe mfano, chama akiba na mikopo cha wanawake TEMEKE, sasa ni chama marehemu, kilifikia hatua za kuwa na jengo lao kubwa la kibenki, ila hivi sasa, jengo sjui limeisha uzwa au bado kwa mikopo ambayo viongozi wa ccm wilaya ya temeke leo hii walikopa ili wapate madaraka, na wako madarakani mpka leo.

Nenda Turian, utakuta pale kiongozi mkubwa wa ccm, ndiye anae ongoza kwa kuwa na mikopo mkubwa na ukiuliza una ambiwa alichukua fedha wakati wa kampeni ili aweze kuwa kiongozi,very shame,

Nenda udzungwa, pale ndo balaaa, Meya mstafu wa chama chetu kizuri (ccm), yeye alikiingiza chama kwenye mikopo balaaa,kwa kushirikiana na wazee wajiitao makamanda wa vijana wilaya ya kilombero, hezni hizo.

Nendeni mtwara kule mambo ni hayo,hayo, hapo mjini Da resalaama,maeneo ya ukonga Banana, kulikuwa na chama kikubwa sanaa cha ushirika, lakini meneja ambae nae ni mwanachama mzuri wa cccm alikopa fedha ili agombee UDIWANI TU, nao hakaukosa sasa ili alipe madeni analazimika kuuza mali za chama kama mabasi, na mali nyingine alipe madeni, huyu ni kada wa ccm,

Ninajua vijana wa ccm mtakuwa hamuelewi msingi wa hoja yangu, maana neno ushirika sasa umekuwa msamiati mkubwa kwa kizazi cha leo.

Nitoe rai,kwa wanao jitamba kuwa wanaunda CCM mpya kuwa hatuwezi kuunda mpya ilihali watoto wakina wale wale ndio viongozi wetu watarajiwa, Pamoja na ccm kuwa na hazina ya viongozi, wazuri pia wapo wabaya ambao ccm mpya haina budi kuwatoa nje, na kuwataka walipe fedha za umma.

Ni Mimi, Mwanaushirika kijana ninae amini maendeleo yanaweza fikiwa katika nchi hii, kupitia umoja wetu, wananchi washirikishwe, wataeleta maendeleo yao kupitia wao kwanza kuchanga walicho nacho

USHIRIKA-Kwa Pamoja Tujenge Uchumi
 
Ukifupisha nitarudi kuisoma, huwezi kuniharibia wikiend na huo waraka
 
Back
Top Bottom