Elections 2010 Ushindi wa upinzani mijini kuliko vijijini, wa vijijini bado ni wadanganyika?

mi_mdau

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
1,104
1,471
Hodi humu mjengoni!

Ukiangalia kwa haraka haraka na kujaribu kulinganisha, ni kama vile upinzani hasa (Chadema) umeweza kufanya vizuri katika maeneo mengi ya mijini na chama tawala kupata kura nyingi maeneo ya vijijini! Cha kusikitisha watu hawa wa vijijini ndio hasa wenye matatizo mengi kama vile huduma za maji, umeme na barabara. Maswali hapa ni je, watu hawa hawana taarifa kuhusu upinzani na sera zake au wameshindwa kuzielewa kutokana na uwezo wao wa kupambanua mambo? Au tuseme bado ni wadanganyika wanaodhani CCM hii ni ile ya enzi za Mwalimu?
 
Kuna mawili: Either Chama cha Sisi wenye eM wanawachakachua zaidi vijijini kwa kuwa hawajashtukia mbinu zao chafu au Vijijini (ambako hadithi za kale bado zinahusudika) bado wanadhani nyerere yuko atawatoa macho kwa kukisaliti icho. Hamkuskia juzjuz mbibi mmoja alisema anataka kumpigia nyerere?
 
naam, tshirt, kofia na elfu tano ndio bado zinaendelea kuwadanganya ndugu zetu wa huko vijijini
 
kwa hali hii sitashangaa umaskini ukiendelezwa ili waendelee kupata kura zao. Miaka mitano itatumika kuchimba visima viwili vya maji vitakavyotumika kuombea kura za miaka mingine mitano. Amkeni mnaibiwa!!!
 
MWENYE NJAA ANATAWALIKA VIZURI. CCM INAFANYA MAKUSUDI KUWANYIMA WATU WA VIJIJINI MAISHA MAZURI. WEE UNAFIKIRI WANAKIJIJI WANAFANYA VITU KWA MATAKWA YAO? THEY ARE HYPONOTISED!

HATA MJINI WAPO WATU AMBAO NI WANAKIJIJI HATA KAMA WANAKAA CITY CENTRE.....YAANI AKILI YAO NI 'SHAKE WELL BEFORE USE':doh:
 
Hodi humu mjengoni!

Ukiangalia kwa haraka haraka na kujaribu kulinganisha, ni kama vile upinzani hasa (Chadema) umeweza kufanya vizuri katika maeneo mengi ya mijini na chama tawala kupata kura nyingi maeneo ya vijijini! Cha kusikitisha watu hawa wa vijijini ndio hasa wenye matatizo mengi kama vile huduma za maji, umeme na barabara. Maswali hapa ni je, watu hawa hawana taarifa kuhusu upinzani na sera zake au wameshindwa kuzielewa kutokana na uwezo wao wa kupambanua mambo? Au tuseme bado ni wadanganyika wanaodhani CCM hii ni ile ya enzi za Mwalimu?

Nionavyo mimi ni kwamba CCM inatumia umaskinini na ujinga wa Watanzania walio vijijini kujipatia ushindi kwa kuwaahidi maziwa na asali na Watanzania walio vijijijini bado wana matumaini ya kupata hiyo asali na maziwa. Hata wakisikia sera za vyama vingine, bado wanaona ni heri wakiunge mkono CCM kuliko kujiunga au kupigia kura vyama vingine. Ni wale tu wanaopata mwanga wa elimu ndio wanaokitosa CCM baada ya kuona kwamba ni chama kiinachowafaidi zaidi watu wenye uwezo (matajiri) kuliko wakulima na wafanyakazi. Nadhani wafanyakazi wameanza kuliona hilo, bado wakulima!
 
its quite easy to lure in rural areas than in cities, people up there have first fear of leaders, so no one can question a doubtful movement or inverted numbers!
 
Back
Top Bottom