ushindi wa tsunami wa Mramba. CCM watachukua hatua gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ushindi wa tsunami wa Mramba. CCM watachukua hatua gani?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by JokaKuu, Aug 5, 2010.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Aug 5, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..huyu ni fisadi lakini wana ccm rombo "hawaoni", wala "hawasikii."

  ..na hili inaelekea kama vile ni tatizo la nchi nzima. hata wale mafisadi walioshindwa ktk mahimbo mengine inaelekea wameshindwa kwasababu tofauti na ufisadi wao.
  .
  ..nategemea kura hizi za maoni za CCM zitatoa mwangaza kuhusu future ya vita vya ufisadi.

  ..
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Huyu akija Slaa atafungwa tu. Hii itakuwa pamoja na watu kama Lowassa, RA, Chenge Et el.

  Hili lisikupe shida. Badala ya kutumia panga, tumia SHOKA.
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Aug 5, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Sikonge,

  ..wasiwasi wangu ni kwamba kauli mbiu ya kampeni ya Slaa ni vita dhidi ya ufisadi na mafisadi.

  ..sasa hii kura ya maoni ya ccm inatuelekeza kwamba wananchi hawako interested na kuwaondoa mafisadi. they simply can not connect the dots kati ya ufisadi na uduni wa maisha yao.

  ..sisemi kwamba Chadema nao waukumbatie ufisadi, lakini ili kupata nafasi ya kuunda serikali na kuutokomeza ufisadi, labda Chadema wanapaswa kuifikiria upya kauli mbiu ya kampeni zao.
   
 4. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hili la Mramba pia limetokea kwa Rostam, inawezekana wananchi wa sehemu husika wakawa sehemu ya mafao ya Ufisadi, maana unaweza kuwa fisadi Makini au Fisadi hovyo. sasa Rostam na Mramba wanaweza kuwa Mafisadi Makini, kwamba wanafisadi Mapato ya Watanzania lakini pia wanatumia sehemu ya pesa hizo hizo kuendeleza maeneo wanakotoka, kwa maana ya kujijenga zaidi kwa wapiga kura wao. just my opinion
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  JokaKuu,
  Siasa haina Black or White. Mwenyewe hapa pamoja na kutokutaka, nilikuwa namshangilia Mwakalinga anayegombea kupitia CHADEMA. Mke wa Shwazneger ni Democrat ila mumewe akshinda, anafurahi ingawa yeye ni Republican.

  Watu wa Mramba wana kila hali ya kumpenda jamaa yao maana kaibia Tanzania nzima na kuwajengea wao. Mwenye Shibe hamjui mwenye njaa. Sasa hapa huwa inabidi Mkono wa serikali uje kutembeza usawa. Kama akishinda Slaa, hawa watu watapanda kizimbani kiukweli na kuhukumiwa kwa wizi wao. Jimbo litakosa Mbunge na uchaguzi ufanyike. Huu ndiyo utakuwa mwisho wao.
  Lowassa pia kashinda wa kishindo. RA, na mafisadi wengine. Akija Slaa, wote watapanda kizimbani na wengine wakishitakiwa kwa kutoa RUSHWA ili wawe wabunge. Hapo ndipo Nusu ya bunge litaondoka.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  jokaKuu,
  Ukipanga vizuri sera na kuelezea wananchi madhara ya ufisadi kwa maendeleo yetu utasikilizwa.
   
 7. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Mkuu Joka KUU

  Warombo walichokiangalia jamaa kafanya nini, naamini kilichowasukuma wamkubali ni Barabara ya lami aliyowajengea. na inavyoelekea wafanyabiashara wengi wa huko aliwatoa saana kipindi alipokuwa anaitafuna national cake, Hii ndo iliyochangia watu wamkubali. Nilichojifunza watu wa huko wanaangalia saana mtu kawafnayia nini Ufisadi sio issue hata kidogo,, Si umeona hata KIMARO wa Vunjo japo alikuwa ni kinara wa kupinga ufisadi lakini jimboni hakufanya lolote si umeona wamentosa??? usishangae wapiga kura wa Vunjo wakamchangua Mrema wa TLP kisa alipokuwa waziri wa mambo ya ndani aliwakatanza na kuwafunga wanaume waliokuwa wanapiga wake zao

  Elimu kwa raia bado ni jukulu la kila mzalendo kuwaelimisha wananchi juu ya ufisadi na hawa mafisadi
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ruska kuota ndoto za mchana.
   
 9. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,713
  Likes Received: 3,119
  Trophy Points: 280
  Joka Kuu hii isikupe tatizo kwani kura za maoni ni za wapenda CCM na si za Watanzania wote. Tusubiri October 31 mungu bariki. Dr. Slaa ni MASIHI yeye yule tuliyetabiriwa tangu enzi kwamba atakuja Mkombozi sasa Ukombozi ndio huu.. Acha hao akina Rostam, Lowassa, Mramba washinde kikubwa hapa ni kuomba Dr. Slaa ashinde hapo MAFISADI watajua chapati ni mlo au kitafunio...
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ruksa pia kupata Juice la tende.
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Aug 5, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Ni kweli,

  Sitaki kuwa mkabila ila najua kuwa watu wa huko wana tabia ya kufukuza mtoto wao majumbani ili waende wakatafute mali kokote kule (kwa njia yoyote hata kama ni kuua mtu) alete nyumbani. Hivyo ukipata mali kwa njia ya ufisadi ukaileta nyumbani, basi utakubalika sana. Mramba anaweza kuwa anakubalika sana kwaoo kwa sababu hiyo. Kama angekuwa na mali akaimalizia yote Uswisi bila kusaidia kwao ni dhahiri asingeshinda kabisa.
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Aug 5, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Nadhani Slaa atafanikiwa sana kwa hilo kwani anajua sana kuchambua mambo na kujieleza.
   
 13. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Inajionyesha wazi na nembo yako ya CCM jinsi unavyowashabikia mafisadi. Lakini hio si ajabu, kwa sababu CCM ya siku hizi imesimama juu ya nguzo za ufisadi. Hujui kuwa ndoto zinakuwa kweli? Hasa zikiwa na misingi ya ukweli? Hakika siku ya mafisadi kuona chao inakuja, wameshaona hiyo na matumbo yao moto.
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  fisadi makini na fisadi hovyo? hivi kweli wewe una shingo ya kubeba kichwa chenye ubongo.
   
 15. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  duuuh... hili dongo si la huruma hata kidogo, hakika limechanganyika na simenti!!
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Sawa, ni ushindi wa tsunami lakini wengi tunachosahau ni kuwa ushindi wenyewe ni wa ndani ya CCM. Mimi kilichonifurahisha ni idadi ya hizo kura ukilinganisha na idadi inayodaiwa na Makamba kuwa ni ya wana CCM - milioni tano. Pamoja na kwamba matokeo kamili na rasmi hayajapatikana lakini wana CCM waliojitokeza kupiga hizo kura naweza kusema ni wale ambao rushwa imekuwa sehemu ya maisha yao na itikadi yao.

  Mwananchi anayejitokeza nyakati hizi na kumpigia kura mtu kama Chenge au Rostamu, anatumwa na nini zaidi ya pato analoahidiwa kulingana na thamani ya hiyo kura yake ! Kwa nini wapiga kura ndani ya CCM wako tayari kutoana macho na ngeu - wanagombania nini kama siyo kuhakikisha kama biashara ya kura yao inalipa. Swali zaidi la kujiuliza ni asilimia ngapi ya wananchi hao wanapokea na kuridhika na hivyo vijisenti na wako tayari kuusaliti utu wao kwa kuendelea kuwa watumwa huku amejitokea mkombozi wa kweli ?
   
 17. A

  Adili JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2010
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 1,997
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Ndiyo maana hatashinda.
   
 18. A

  Adili JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2010
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 1,997
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Natumaini kuna mwanaChadema anasoma mawaidha haya - na kuyafikisha kwa wenye maamuzi.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Aug 6, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani eeeeh Ikumbukwe tu kwamba waliomchagua Mramba ni wanaCCM. Hizi kura za maoni ni kura za mapendekezo ya wanaCCM kulingana na vigezo walivyopewa kuwachagua wawakilishi wao..Na wote hawa toka Mramba hadi Lowassa na wengineo hawawakilishi mawazo ya Watanzania wengi wala wapiga kura wengi.

  Hivyo tusichanganye vitu hapa kwamba maadam wana CCM wamemchagua Mramba basi nasi soote tukubali kwamba Ufisadi sio issue. Na lini wanaCCM wamekubali kuwepo na Ufisadi? Ile hata kukubali tu kwamba viongozi wao ni mafisadi hawakubali na wanaapa kwa viapo kwamba viongozi wao wanasingiziwa na watu wenye Chuki na wivu. Pia ni hawa hawa CCM waliotuambia kwamba Ufisadi ni wa baadhi ya viongozi ndani ya chama na sio chama lakini mafisadi wote wamepita kura hizo na wanatarajiwa kurudi bungeni. Hii ina maana gani?
  Sasa sielewi ni Watanzania wangapi wanaamini hivyo pia..
   
 20. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  watanzania tubadilike, mtu asipokuwa waziri hawezi fanya lolote jimboni zaidi ya kuwatetea tu watanzania kama alivyo fanya kimaro,
   
Loading...