Ushindi wa nasari,siasa vyuoni na mtazamo wa kimagamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushindi wa nasari,siasa vyuoni na mtazamo wa kimagamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lunyelunye, Apr 3, 2012.

 1. l

  lunyelunye Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia kutoka kwa viongozi hasa wenye kuogopa wimbi la weledi wa vijana katika siasa mpya zinazotegemea facts na akili za kichambuzi zaidi kuliko propaganda mfu, wamekuwa wakijaribu kuonyesha kutuaminisha kwamba vijana wakiwa vyuoni kushiriki kwao katika mijadala ya uchambuzi na hata kujiunga na harakati mbalimbali za kupigania haki za wenzao katika maisha yao wakiwa chuoni, inaonekana kama vile ni uasi na vurugu.

  Watu wenye mtazamo huo wangetamani au wanadhani hata katika ngazi hiyo ya elimu ya juu, na tena hata kwa mtu anaesoma masomo yanayohusu siasa na uongozi anapaswa kuishi maisha ya pembe tatu yaani darasani,kula na kulala kama vile wanasoma elimu ya msingi.

  HOJA YANGU: Nyota njema huonekana asubuhi, wanasiasa maarufu, na hata viongozi wazuri tunaowajua wameanza kuonekana wakiwa vyuoni katika ushiriki wao wa siasa za wanafunzi. mfano JK nyerere akiwa makerere, kikwete,mseveni na warioba katika siasa za DUSO wakiwa UDSM. Pia kuna vijana kama kina ZITO, silinde, Nasari, Mwita Waitara na wengine wengi ambao wamelelewa na siasa za wanafunzi na kupata moyo wa harakati na uongozi na kazi zao tumeziona.

  My Take:Fikra tete na moyo wa udadavuzi wa hoja na tafakuri jadidi unaanza kujengwa sheleni, tuwaache vijana wajifunze changamoto za uongozi wakiwa chuoni na washamiri na kupata hamu ya kuongoza taifa lao. Wazee tusiogope changamoto na nguvu za hoja za vijana bali tuwape nafasi na ushauri ili wakue katika busara na hekima. Ushindi Wa Nasari kama ulivo wa vijana wengine kama Zito,Silinde, January, Mnyika n.k uwafumbue macho muone umuhimu wa vijana ku-practice siasa zao za kiuanafunzi wakiwa shule maana ndizo huleta akisi picha ya baadae katika siasa za nchi yetu. NAOMBA KUTOA HOJA
   
 2. i

  interesting New Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  true nyota njema huonekana asubuhi
   
 3. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono hoja!
  Kamwe kama wapambanaji,tusitegemee CCM na serikali itengeneze mazingira mazuri kwetu kama wapambanaji!
  Rather,tunatakiwa kuendelea kupambana!
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,159
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Na JK mkuu, au nimeona vibaya kwenye mfano wako hapo juu.
   
 5. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Lunyelunye nimependa sana hoja yako. Ni kweli huu ni muda wa mabadiliko. Ningependa kukuona ana kwa ana ili tujadili suala hili. Mimi ni mmoja wa watu wenye kuamini kuwa vijana ndio ukombozi wetu na vyuo ndiyo sehemu hasa ya kuanzia. Ni moja ya watu wanaosikitika kwa wanavyuo kuzuiwa kushiriki uchaguzi 2010 na nahisi hata kwenye mchakato wa katiba watawakwepa. Naweza kusema viongozi wa CCM ya sasa 80% hawapatani na vitabu, hawapendi kusoma na ndio maana kwenye shughuli nzito kama ya kutetea jimbo wanawapeleka watu wenye sifa za matusi akina wasirra na Lusinde.
   
 6. v

  vngenge JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  WAZEE WANA TATIZO MOJA NALO NI KuAMINI KUWA KITU AMBACHO YEYE AMESHINDWA BASI KIJANA HAWEZI KUFANYA. Kitu ambacho si kweli. Ndio maana unaona wengi wanazeekea makazini bila kuwapa nafasi vijana. Wanawaambia hawana uzoefu! sasa uzoefu wanapataje kama sio hizo harakati mashuleni na nyie muwape nafasi makazini waonyeshe vipaji. Kufanya mambo kwa mazoea kunanyima fursa za kufikiri njia bora zaidi ya kufanya mambo!
   
 7. nyabibuye

  nyabibuye Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwenye mchakato wa katiba mpya, naomba wafunge chuo tena, ili tukatoe elimu huko vijijini, yani kwa sasa tumejipanga hatutadhulumiwa haki yetu hata kidogo, katiba mpya lazima kila mtu ashiriki kwa namna yeyote!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 8. l

  lunyelunye Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haina shida bwana Mpitagwa vijana tunatakiwa kupata muda wa kujadiliana sisi kwa sisi pia ili kujijenga
   
 9. O

  OSCAR ELIA Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  naunga mkono hoja.
   
 10. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hoja muafaka hii: Naunga mkono mia kwa mia........
   
 11. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja 100%
   
 12. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  CCM iliyomlea Nyerere na kumfanya PM wa Kwanza wa Tanganyika sio CCM hii ya akina Kikwete na Mkama. CCM hii haimini katika vijana. Wao wanasema kwamba VIJANA NI TAIFA LA KESHO na nafasi yao ni UVCCM.

  CDM imeonesha kwamba inaweza ku-nuture VIJANA kutoka vyuo vya Elimu juu and from there wakaenda majimboni kugombea UBUNGE na kushinda kama walivyofanya akina Silinde, Nassari hii ni ndoto kwa CCM, labda kwenye VITI MAALUMU tena uwe nyumba ndogo ya mtu au ndugu wa kigogo nk. lakini SIO JIMBO.

  Hivyo vijana walio vyuo vya elimu ya juu changamkieni fursa hii ya CDM shirikini siasa na 2015 mjitokeze kwa wingi kwenda majimboni kugombea Udiwani na Ubunge. CCM hawatatoa mazingira rafiki ya VIJANA kushiriki siasa vyuoni because it is like shooting themselves on foot, lakini inabidi HAKI hiyo ipiganiwe.

  CDM tunasema VIJANA NI TAIFA LA LEO. Tuwaache CCM na mawazo yao mgando kuwa VIJANA NI TAIFA LA KESHO, hiyo kesho haitafika kwa vijana hadi mwisho wa dunia.
   
 13. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hoja yako ni nzuri, pia ni swala ambalo viongozi wa cdm wanatakiwa kuliangalia kwa kina, wanatakiwa wa-invest sana huko vyuoni, kwani ni ukweli usio na shaka kuwa almost vijana wote wanataka mabadiliko na mabadiliko ya kweli yapo cdm.
  M/kiti - mh Mbowe na katibu - mh Slaa, lifanyieni kazi hili swala, vile vile vijana ndio wapiga kura, na kura zao wanapigia cdm...
   
 14. T

  Tejai Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hoja ya vijana taifa la kesho imepitwa na wakati sana tu,sijui magamba kwa nini wanapenda kuitumia,vijana ni taifa la leo waandaliwe vizuri ili wawe viongozi wazuri,hoja nzuri kamanda
   
 15. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Naunga mkono hoja NASSARI alikuwa naibu spika wangu pale udsm nikiwa mbunge kweli lile bunge lilitukomaza sana NDO mana magamba yanaogopa siasa za vyuo nachoshukuru yameshindwa kuzuia hilo.....PIPOZZZZZZZ.
   
 16. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mabadiliko yakishafika hayana makundi ila kwa wakati huu vijana ndiyo wanatakiwa kuwa mstali wa mbele hasa wale wa vyuoni, nashukuru kwa post yako..
   
 17. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hata mimi mara baada ya kujiunga University 2009 nikajiunga CDM.Na sasa najiandaa kuchukua jimbo la Ulanga,nataka nimwangushe huyu Waziri
   
 18. w

  wade kibadu Senior Member

  #18
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimemipenda nakala yako.
   
 19. l

  lunyelunye Member

  #19
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera sana mnyonge namba moja
   
 20. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Kuna yeyote anayefahamu Nassari kasoma kozi gani pale UD?

  Na ushiriki wake katika harakati na siasa za daruso?

  Please!!!!:yo:
   
Loading...