Ushindi wa Lema una maana kubwa sana kwenye Ujenzi wa chama

FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
1,195
Kwanza nachukua fursa hii kuwatakia heri ya christmas na mwaka mpya watanzania wote tukae salama kipindi hiki.

Wakati wana chadema wanatoka nje kushangilia ushindi wa ndugu Godbless Lema kurudishiwa ubunge wake nilikua nje ya mahakama hakika nilipatwa na mawazo ya haraka sana hivi ni kwanini tokea mahakama ya rufaa hawakumpa haki yake Lema je alikua tishio sana kwa ccm ndo maana walinyima mikutano kufanyika Arusha baada ya Lema kusimamishwa ubunge.

Na baada ya lema kushinda Nape akaja anasema ni wakati wa Lema kuacha maandamano lakini bado nikajiuliza je tatizo la Arusha CCM hawalijui je kumuweka Meya Feki watu ilibidi wapinge kwa maandano lakini kwa kipindi kifupi kama Lema anavyosema alikua mapumziko ameleta mabadiliko makubwa sana kuzunguka na M4C na kujenga chama hadi vijijini.

Haipiti wiki hujasikia leo Lema yuka dar,arusha,monduli,simanjiro,kagera,mwanza,geita na pengine anastaili sifa huku akiwa anadai haki yake ya ubunge irudi ndo alivyokua akizidisha kasi ya kujenga chama hakika ni Lema alikua lulu mwaka huu.

Ubunge wa Lema umerudi kipindi muafaka sana kwa inabidi ajitafakari aweze kuulizia baadhi ya maswala bungeni kuhusu Arusha ili kutekeleza baadhi ya Ahadi japo alirudishwa nyuma lakini naamini sasa wana Arusha mmepata haki yenu mna mbunge wenu mnayempenda kupita maelezo kutoka chama mnachokipenda msaidie sana kutekeleza ahadi msaidieni sana kutekeleza ndoto zake ziwe kweli Arusha iwe imara.

Lakini kurudi kwa Lema bungeni kuachia chama nafasi ya kuziba ni dhahiri sehemu ambazo Lema alikuwa anapita kila wiki sasa atashindwa atabidi ahudhurie vikao vya bunge,vikao vya kamati,baraza la madiwani,kuandaa bajeti ya wizara ya mambo ya ndani kivuli ni dhahiri Lema atakua busy sana hata ujenzi wa chama kuna muda hataonekana kama mwanzoni.

Ni wakati sasa wa vijana wa chadema kufuata nyao kama lema M4C iendelee mbele wao watapiga kupitia bungeni sisi tutapiga huku uraiani wakirudi majimboni tutawaaomba mara moja moja kuongeza hamasa kwenye mikutanao.

Sasa wabunge wa chadema wanahitakijika kufanya kazi mara 10 zaidi walivyofanya nusu muhula wafanye kazi kama vichaa wazunguke majimboni kwao washirikiane na wananchi majimbo yetu mpaka 2014 yawe ya mfano tuna majimbo 24 uchaguzi wa serikali za mtaa unakuja ina maana kila jimbo 1 lina serikali za mitaa labda 14 kama kila jimbo letu tutabeba serikali za mitaa 10 tutakua na serikali za mitaa 240 hadi hapo huku kwenye majimbo ambapo hatuna wabunge tutaokoteza serikali za mitaa nyingine lengo zifike zaidi ya serikali za mitaa 500 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ujayo.

Wabunge wetu wakumbuke bila wao kusimamia ufisadi na kukisimamisha chama kionekane itabidi wapambane zaidi na zaidi wapeleke hoja binafsi mbalimbali kama zilizopita usiswi-zitto,mdee-ardhi,mnyika-maji,nasari-baraza la mitihani.

Kuna hoja nyingine kibao kama 1.reli ya kati,2.mfumo wa elimu,3.ajira wazitumia kama chachu ya kukikuza chama chetu kukijenga ndani ya bunge na nje ya bunge.

Niwashukuru wanachama wote kwa mapenzi mema na chama chetu tunaingia kipindi kigumu sana kipindi kinachohitaji akili na sio nguvu kipindi kinachohitaji umoja mshikamano pamoja na busara na hekima.

Fk
 
kasuku1

Senior Member
Oct 19, 2012
125
195
Hilo ni wazo zuri hata mimi nakuunga mkono ni lazima kuwe na tofauti kati ya maeneo ambayo chadema inaongoza na maeneo ambayo CCM inaongoza watu waweze kuona tofauti kati ya CDM na CCM alafu waone kuwa kuchagua CDM ni bora zaidi kuliko kuchagua CCM. Kuna maeneo ambayo baadhi ya madiwani wa CDM wamelala hawaonekani wala hawafanyi vikao na wananchi kujua wanashida gani na kuona jinsi ya kushirikiana kuzitatua hili linasikitisha. Kwenye baadhi ya maeneo ambayo nimetembelea ukiwauliza wananchi ambao wako chini ya uongozi wa CDM kama wanaona tofauti yoyote kati ya sasa na walipokuwa chini ya uongozi wa CCM watakuambia hamna tofauti wote ni walewale. Hii inatia shaka na inaondoa uaminifu wa chama kwa wananchi. Ninawaombe viongozi wa juu wa CDM kuhakikisha wanawasimamia wabunge na madiwani wa CDM na kuhakikisha kuwa wanawajibika kwa wananchi ipasavyo ikiwezekana wabunge na madiwani wawe wanaandaa taarifa za utendaji wao kila mwaka na viongozi wa juu wa CDM wahakiki hizo taarifa kuona kama zinaukweli. Kuna mambo mengine ambayo ni madogo na utekelezaji wake hauhitaji kiongozi awe na fedha anaweza tu kuwahamasisha wananchi wakafanya jambo fulani la maendeleo kwa kuchangia mambo kama madawati, ujenzi wa barabara za mitaa ujenzi wa darasa ni mambo ambayo wananchi wakihamasishwa na kukawa na usimamizi mzuri wanaweza kuchangia na kuyatekeleza.
 
Kweli kabisa mkuu
 
KIBE

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
943
0
hilo ni wazo zuri hata mimi nakuunga mkono ni lazima kuwe na tofauti kati ya maeneo ambayo chadema inaongoza na maeneo ambayo ccm inaongoza watu waweze kuona tofauti kati ya cdm na ccm alafu waone kuwa kuchagua cdm ni bora zaidi kuliko kuchagua ccm. Kuna maeneo ambayo baadhi ya madiwani wa cdm wamelala hawaonekani wala hawafanyi vikao na wananchi kujua wanashida gani na kuona jinsi ya kushirikiana kuzitatua hili linasikitisha. Kwenye baadhi ya maeneo ambayo nimetembelea ukiwauliza wananchi ambao wako chini ya uongozi wa cdm kama wanaona tofauti yoyote kati ya sasa na walipokuwa chini ya uongozi wa ccm watakuambia hamna tofauti wote ni walewale. Hii inatia shaka na inaondoa uaminifu wa chama kwa wananchi. Ninawaombe viongozi wa juu wa cdm kuhakikisha wanawasimamia wabunge na madiwani wa cdm na kuhakikisha kuwa wanawajibika kwa wananchi ipasavyo ikiwezekana wabunge na madiwani wawe wanaandaa taarifa za utendaji wao kila mwaka na viongozi wa juu wa cdm wahakiki hizo taarifa kuona kama zinaukweli. Kuna mambo mengine ambayo ni madogo na utekelezaji wake hauhitaji kiongozi awe na fedha anaweza tu kuwahamasisha wananchi wakafanya jambo fulani la maendeleo kwa kuchangia mambo kama madawati, ujenzi wa barabara za mitaa ujenzi wa darasa ni mambo ambayo wananchi wakihamasishwa na kukawa na usimamizi mzuri wanaweza kuchangia na kuyatekeleza.

mumepewa halmashauri nne zimewashinda kilichobaki ni kufukuzana tu...sijui kama mnajua tatizo ni nini??.... ( ccm wanaweka stoo tu 2015 sijui itakuwaje) ..
 
FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
1,195
mumepewa halmashauri nne zimewashinda kilichobaki ni kufukuzana tu...sijui kama mnajua tatizo ni nini??.... ( ccm wanaweka stoo tu 2015 sijui itakuwaje) ..

Mkuu kwenye uongozi kuna challenge ndo hizo sasa tunajifunza tuondoe matatizo kwani ccm imekosea mara ngapi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom