Ushindi wa lazima unavyoufedhehesha moyo

Itovanilo

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
1,289
2,000
Habari za asubuhi wapendwa, Ni asubuhi ya jumapili hii najiandaa kwenda church, ila nikaona niwaache na hii

Nakumbuka miaka fulani nikiwa darasa la tano katika shule moja huko mkoani,aliingia mwl wa darasa kwaajili ya kuendesha zoezi la kumpata Monitor na monitress,

Hivyo yakapendekezwa majina mawili mawili kwa mvulana na msichana halafu kura zinapigwa, but kwa upande wa wasichana mshindi alipata asilimia karibu Zote za kura, kwa upande wetu mwenzangu alipata asilimia 93, Mimi nilipata aslimia 4 ya kura.

Nadhani 3 ziliharibika kutokana na baadhi ya wahuni ambao hawakosekani chini ya jua. Kilichonisukuma niandike haya Ni mwalimu kugeuza kibao na kunipendelea Mimi kwa kigezo yule hakuwa na uwezo kuanzia taaluma, nidhamu, usafi wa mavazi pia alikuwa mpiga kelele mzuri darasani hivyo hawezi kuongoza

Kiutoto mchizi hakumaindi Wala Nini licha ya zomeazomea ya hapa na pale tukiwa class, hivyo Mimi nikawa Monitor wao, kwa vigezo ambavyo teacher alivielezea.

Cha ajabu, nilijikuta naumia Sana, yaani nilijikuta mwenye hatia, takribani week nzima sikuwa na amani kwa kupewa nafasi ambayo najua wazi sistahili, siyo siwezi kuongoza bali najua darasa liliamua kumpa kura mtu flani na siyo Mimi jamani.

Kila nikikumbuka huwa nacheka tu,nawaza wenzetu wanasiasa wanawezaje kuishi na vyeo ambavyo wanajua wazi walipora watu?

Dhuluma ni dhambi, inanyong'onyesha sijui wengine wanawezaje. ni njaa? Ni kutafuta heshima? au Ni nini, kama Ni njaa wengine hawana, Kama ni heshima wengine wanayotoka enzi na enzi?

Je unajisikiaje kuwaongoza watu ambao hawana imani na wewe? kwasababu hawakuamini ndiyo maana hawajakuchagua wewe.

Asubuhi njema JamiiForums.
 

Chacho Haulage

JF-Expert Member
Aug 25, 2017
204
250
Kama hapo kazini kwako uliingia kiujanja ujanja, basi umedhulumu nafasi ya mtu aliyetakiwa kuingia kihalali. Na kama hujishtukii basi umezoea dhambi ya dhuluma.

Zingatia neno 'kama'
 

mkupuo

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,459
2,000
Mkuu usifanani$he uchaguzi wa wanafunzi na wanasiasa.Kwa wanasiasa kuna maslahi makubwa sana wanayapata hivyo yanafuta kabisa aibu.
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,934
2,000
Hukuiba kura wala kutishia watu wala hukuhonga kwa hiyo uwe na amani tu
Ilikuwa sio upendeleo bali hakukidhi masharti
Hawa wengine hawajutii bali wanafurahia hali hiyo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom