Ushindi wa kwanza wa Taifa Stars vs Malawi COSAFA leo June 25 2017

PAGAN

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
11,224
17,797
Leo, June 25 2017 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambao ni wageni waalikwa katika michuano ya COSAFA 2017 inayoendelea nchini Afrika Kusini, walicheza game yao ya kwanza ya michuano hiyo dhidi ya timu ya taifa ya Malawi katika uwanja wa Moruleng uliopo katika mji wa Rusterburg.

Taifa Stars ambayo imeshiriki michuano hiyo ikiwa na wachezaji wake wote kasoro nahodha wao Mbwana Samatta, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-0, magoli ambayo yote mawili yalifungwa na Shiza Kichuya dakika ya 13 na 18 ya mchezo.

Taifa Stars ambayo ipo Kundi A na timu za Angola, Mauritius na Malawi, kwa sasa inaongoza kundi hilo kwa kuwa na point tatu na magoli mawili wakati huu ambao inasubiria matokeo ya mchezo wa pili kati ya Mauritius dhidi ya Angola.

Ushindi huo wa Tanzania dhidi ya Malawi unakuwa ni ushindi wa pili katika mechi zao tatu za mwisho kwa timu hizo kukutana, baada ya kuifunga mara ya mwisho uwanja wa Taifa October 7 2015 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 lakini baadae Taifa Stars ilipoteza kwa goli 1-0 ugenini October 11 2015 na kusonga mbele kwa aggregate. [Habari kutoka: millardayo.com]

DSC_0013-660x400.jpg
 
Chadema watapinga.
 
Hongera Kichuya, ila Msuva kwanini mechi za nje huwa anazubaa sana? Nampenda na napenda michuano hii abaki South hukohuko. Ajitume zaidi na zaidi
 
ThanksTE="balibabambonahi, post: 21853599, member: 282931"]Anaitwa Shiza. Ramadhan Kichuya[/QUOTE]
Thanks
 
Back
Top Bottom