Ushindi wa Kupita bila Kupingwa Ludewa wapingwa mahakamani

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,502
2,000
Gazeti la Nipashe linatuhabarisha ya kuwa ushindi wa Mbunge wa Ludewa huko Njombe Mheshimiwa Deo Phillip sasa kuamuliwa na mahakama baada ya kupingwa huko...............
 
Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
195
Mwanzo mzuri sana!!!!!!!!!!!! Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetakiwa itamke kwamba kushinda bila kupingwa ni batili; huu hasa ni mwanzo mzuri kwa move yetu ya kum-support MwanaJF M.M.Mwnakijiji kwa ajili ya jumla ya wabunge wote 19; Filikunjombe, ambaye ni mbunge wa Ludewa, ni mmoja wa waliolalamikiwa katika kesi Na: 02/2010, yeye akiwa mlalamikiwa na. 1; wengine, na.2 ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ludewa, na na. 3 ni Mwnansheria Mkuu wa Serikali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Wakili -Kampuni ya Uwakili ya Mpoki ya Dsm-itathibisha mbele ya mahakama hiyo jinsi sheria za uchaguzi na. 343 mapitio ya 2002, na kanuni zake ambazo zipo kwenye tangazo la Serikali na. 279 la 2010 zilivyovunjwa!!!!; Naamini sheria hizi zitakuwa zimetokana na sheria mama ya msingi-KATIBA!!!!!
Mlalamikaji ameiomba mahakama itamke kwamba kushinda bila kupingwa ni BATILI-hivyo uchaguzi URUDIWE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
195
MwanaJF Ruta thanks alot kwa kufungua thread hii! Ina mchango mkubwa sana kwa support yetu kwa Mwanakijiji!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,045
2,000
Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, amefunguliwa kesi ya kupinga ushindi wake.
Kesi hiyo imefunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa akipinga ushindi wa bila kupingwa wa mbunge huyo.

Aliyefungua kesi hiyo, Manfred Peter Mtitu, anaiomba Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa kutamka kwamba ushindi wa bila kupingwa wa Filikunjombe ni batili na kuamuru uchaguzi mdogo ufanyike katika jimbo hilo.

Msajili wa Wilaya wa Mahakama hiyo, Firmin Matogolo, amethibitisha kesi hiyo kufunguliwa mahakamani hapo na kueleza kuwa kesi hiyo ni Namba 02 ya mwaka huu.
Kwa mujibu wa Matogolo, Mtitu amefungua kesi hiyo kupitia kampuni ya uwakili ya Mpoki ya Jijini Dar es Salaam ambapo mshitakiwa wa kwanza ni Mbunge wa Ludewa, mshitakiwa wa pili ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ludewa na wa tatu ni Mwanasheri Mkuu wa Serikali.

Mtitu anadai kuwa yeye ni mwanachama wa Chadema na aliteuliwa kihalali na chama chake kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa.
Anadai kuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo alimtangaza Filikunjombe wa CCM kuwa mgombea pekee baada ya mtu mbaye hakuteuliwa na Chadema, Geofrey Mgaya kuenguliwa.

Anadai kuwa Mgaya hakuwa mgombea wa Chadema kwa sababu kwa mujibu wa utaratibu wa Chadema, mgombea ubunge anateuliwa na makao makuu ya Chadema na kwamba yeye ndiye aliyeteuliwa.

Anadai kuwa alipopeleka fomu zake kwa msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ludewa, alizikataa kwa madai kuwa hawezi kupokea wagombea wawili kutoka chama kimoja (Chadema).
Mlalamikaji katika kesi hiyo anadai kwamba alipeleka barua ya kulalamikia hatua hiyo kwa msimamizi huyo, lakini aliidharau, kitendo ambacho kilimnyima haki yake ya kikatiba.

Anadai kwa kufanya hivyo, uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi ikiwemo ya kutozingatia sheria ya uchaguzi namba 343 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002 pamoja na kanuni zake ambazo zipo kwenye tangazo la Serikali namba 279 la mwaka huu.
Aidha, anadai kuwa kwa kushindwa kupokea fomu zake, msimamizi wa uchaguzi alikiuka kifungu namba 38, kifungu kidogo cha 5 cha sheria hiyo ya uchaguzi.

Kwa msingi huo, mlalamikaji anaiomba Mahakama kutamka kwamba kushinda bila kupingwa kwa Filikunjombe ni batili na uchaguzi mdogo urudiwe.
Pia, anaiomba Mahakama itamke kwamba tamko kuwa Filikunjombe alipita bila kupingwa ilikuwa ni batili na ombi lake la tatu ni kwamba Filikunjombe na washitakiwa wengine katika shauri hilo, warejeshe gharama za kesi na gharama nyingine ambazo Mahakama Kuu itaona zinafaa.
CHANZO: NIPASHE
 
kiraia

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
1,713
2,000
Mwanzo mzuri, ila wasiwasi wangu ni kwamba hukumu ya Kesi hii itatolewa June 2015
 
Shalom

JF-Expert Member
Jun 17, 2007
1,315
1,195
Tusisahau kuwa na Fredirick Mpendazoe nae kafungua kesi wazee na Jumamosi kutakuwa na hafla ya kumwezesha kugharamia kesi. Inabidi uweke deposit kama ya million 15 hivi kupangiwa judge
 
QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
0
Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, amefunguliwa kesi ya kupinga ushindi wake.
Kesi hiyo imefunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa akipinga ushindi wa bila kupingwa wa mbunge huyo.

Aliyefungua kesi hiyo, Manfred Peter Mtitu, anaiomba Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa kutamka kwamba ushindi wa bila kupingwa wa Filikunjombe ni batili na kuamuru uchaguzi mdogo ufanyike katika jimbo hilo.

Msajili wa Wilaya wa Mahakama hiyo, Firmin Matogolo, amethibitisha kesi hiyo kufunguliwa mahakamani hapo na kueleza kuwa kesi hiyo ni Namba 02 ya mwaka huu.
Kwa mujibu wa Matogolo, Mtitu amefungua kesi hiyo kupitia kampuni ya uwakili ya Mpoki ya Jijini Dar es Salaam ambapo mshitakiwa wa kwanza ni Mbunge wa Ludewa, mshitakiwa wa pili ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ludewa na wa tatu ni Mwanasheri Mkuu wa Serikali.

Mtitu anadai kuwa yeye ni mwanachama wa Chadema na aliteuliwa kihalali na chama chake kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa.
Anadai kuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo alimtangaza Filikunjombe wa CCM kuwa mgombea pekee baada ya mtu mbaye hakuteuliwa na Chadema, Geofrey Mgaya kuenguliwa.

Anadai kuwa Mgaya hakuwa mgombea wa Chadema kwa sababu kwa mujibu wa utaratibu wa Chadema, mgombea ubunge anateuliwa na makao makuu ya Chadema na kwamba yeye ndiye aliyeteuliwa.

Anadai kuwa alipopeleka fomu zake kwa msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ludewa, alizikataa kwa madai kuwa hawezi kupokea wagombea wawili kutoka chama kimoja (Chadema).
Mlalamikaji katika kesi hiyo anadai kwamba alipeleka barua ya kulalamikia hatua hiyo kwa msimamizi huyo, lakini aliidharau, kitendo ambacho kilimnyima haki yake ya kikatiba.

Anadai kwa kufanya hivyo, uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi ikiwemo ya kutozingatia sheria ya uchaguzi namba 343 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002 pamoja na kanuni zake ambazo zipo kwenye tangazo la Serikali namba 279 la mwaka huu.
Aidha, anadai kuwa kwa kushindwa kupokea fomu zake, msimamizi wa uchaguzi alikiuka kifungu namba 38, kifungu kidogo cha 5 cha sheria hiyo ya uchaguzi.

Kwa msingi huo, mlalamikaji anaiomba Mahakama kutamka kwamba kushinda bila kupingwa kwa Filikunjombe ni batili na uchaguzi mdogo urudiwe.
Pia, anaiomba Mahakama itamke kwamba tamko kuwa Filikunjombe alipita bila kupingwa ilikuwa ni batili na ombi lake la tatu ni kwamba Filikunjombe na washitakiwa wengine katika shauri hilo, warejeshe gharama za kesi na gharama nyingine ambazo Mahakama Kuu itaona zinafaa.
CHANZO: NIPASHE

This is good. Hakuna kupita bila kupingwa nchi hii
 
matawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2010
2,055
1,195
Mtitu komaa maana haki lazima itendeke haya mambo ya kupita bila kupingwa binafsi siyapendi naona kama yanaua democrasia
 
Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,457
1,500
komaa mtitu, anayetakiwa kupita bila kupingwa ni Mungu, komaa ukishinda kunauwezekano mkubwa mahakama ikatamka kuwa hakuna kitu kina itwa '' kupita bila kupingwa" ikifanyika hivyo kilio na kusaga meno kitakuwa nchi nzima. ujanjaujanja tu!!!!
 
Newvision

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
448
0
Mtitu nakusupoti 100% hawa jamaa yaanai wasimamizi wa uchaguzi wanaowekwa kwa manufaa ya CCM hatuwataki. La msingi haki itendeke. CHADEMA wanabase ya kutosha kule Ludewa komaa tu
 
Mabel

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
1,134
1,500
Hii dhana ya kupita bila kupingwa haiingii akilini hata kidogo. Nafikiri pia hata TAKUKURU ingekuwa kweili ni chombo cha kumbana na kuzui rushwa ingepinga kambi kwenye majimbo yote ambayo watu walidai kupita bila kupingwa (japo kwa ndugu Masha mambo yalikwenda mrama kwake) na hapa tungepata maana halisi ya kupita bila kupingwa.

Katiku kupita bila kupingwa kuna mambo mawili dhahili;
  1. Mlungula ulifanya kazi yake hadi wapinzani wa yule aliyepita bila kupingwa akapita (mifano; Jimbo la Mkono na Mkuu wa mkoa wa wa Dar)
  2. Either mtu kafanyia hila na kuenguliwa (mfano yaliyotaka kutokea kule Nyamagana)
Hakuna kupita bila kupingwa hapa, huu ni usanii na ulaghai mkubwa kwa wananchi
 
Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
195
Mtitu omba Chadema wakupe support kubwa ili mbinu za hongo na uchakachuaji wa sisiemu vishindwe!!!!!!!!!! Uchaguzi ukirudiwa sisiemu haitaona ndani I tell you!!!!!!!!!!!!!!!! Ni mpaka majimbo yote 19 yamerudiwa uchaguzi na sisiemu kupoteza vyoooooooooteeeeeeeee na CDM kuongeza viti 19 bungeni!!!!!!!!!!!!!!!!!! Yes We Can!!!!!!!!!!!!!!
 
cabhatica

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
1,077
1,225
There is no such a thing as KUPITA BILA KUPINGWA. You can never become elected MP without election. THIS IS PURE COMMON SENSE. Whether you have been elected by your party's elite or a group of party members YOU ARE NOT AN ELECTED MP to represent a constituent as long as polls organised and mornitored by NEC were not cast, PERIOD. To me all these constituents are still VACANT and I am still waiting for any smart chap to tell me otherwise.

By allowing this null and void MPs, NEC has proved incapable incompetent intolerable - a total failure.
That is why NEC must resign voluntarily in lieu of facing the wrath of the people.
 
Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
0
Wakili wa mlalamikaji aongeze msingi mwingine wa kupinga dhana nzima ya mtu kupita bila kupigiwa kura. Nijuavyo mimi dhana ya kupita bila kupingwa, inakuja pale tu ambapo mgombea anakuwa hana mpinzani na hivyo anapigiwa kura za hapana na ndiyo.
 
Ng'azagala

JF-Expert Member
Jun 7, 2008
1,287
1,250
Tehetehe sasa ilikuwaje kuwe na wagombea wawili wa CDM jimbo moja?

ni kama kule Zanzibar wakati wa kuchukua form za urais kuna watu wawili waligombania form kupitia chama kimoja wakarudishwa mpaka chama kilipotoa maelezo
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,502
2,000
Mwanzo mzuri sana!!!!!!!!!!!! Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetakiwa itamke kwamba kushinda bila kupingwa ni batili; huu hasa ni mwanzo mzuri kwa move yetu ya kum-support MwanaJF M.M.Mwnakijiji kwa ajili ya jumla ya wabunge wote 19; Filikunjombe, ambaye ni mbunge wa Ludewa, ni mmoja wa waliolalamikiwa katika kesi Na: 02/2010, yeye akiwa mlalamikiwa na. 1; wengine, na.2 ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ludewa, na na. 3 ni Mwnansheria Mkuu wa Serikali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Wakili -Kampuni ya Uwakili ya Mpoki ya Dsm-itathibisha mbele ya mahakama hiyo jinsi sheria za uchaguzi na. 343 mapitio ya 2002, na kanuni zake ambazo zipo kwenye tangazo la Serikali na. 279 la 2010 zilivyovunjwa!!!!; Naamini sheria hizi zitakuwa zimetokana na sheria mama ya msingi-KATIBA!!!!!
Mlalamikaji ameiomba mahakama itamke kwamba kushinda bila kupingwa ni BATILI-hivyo uchaguzi URUDIWE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Bora kukata mzizi wa fitina huko mahakamani tu...................
 
Rufumbu

Member
Nov 19, 2010
7
0
Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, amefunguliwa kesi ya kupinga ushindi wake.
Kesi hiyo imefunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa akipinga ushindi wa bila kupingwa wa mbunge huyo.

Aliyefungua kesi hiyo, Manfred Peter Mtitu, anaiomba Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa kutamka kwamba ushindi wa bila kupingwa wa Filikunjombe ni batili na kuamuru uchaguzi mdogo ufanyike katika jimbo hilo.

Msajili wa Wilaya wa Mahakama hiyo, Firmin Matogolo, amethibitisha kesi hiyo kufunguliwa mahakamani hapo na kueleza kuwa kesi hiyo ni Namba 02 ya mwaka huu.
Kwa mujibu wa Matogolo, Mtitu amefungua kesi hiyo kupitia kampuni ya uwakili ya Mpoki ya Jijini Dar es Salaam ambapo mshitakiwa wa kwanza ni Mbunge wa Ludewa, mshitakiwa wa pili ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ludewa na wa tatu ni Mwanasheri Mkuu wa Serikali.

Mtitu anadai kuwa yeye ni mwanachama wa Chadema na aliteuliwa kihalali na chama chake kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa.
Anadai kuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo alimtangaza Filikunjombe wa CCM kuwa mgombea pekee baada ya mtu mbaye hakuteuliwa na Chadema, Geofrey Mgaya kuenguliwa.

Anadai kuwa Mgaya hakuwa mgombea wa Chadema kwa sababu kwa mujibu wa utaratibu wa Chadema, mgombea ubunge anateuliwa na makao makuu ya Chadema na kwamba yeye ndiye aliyeteuliwa.

Anadai kuwa alipopeleka fomu zake kwa msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ludewa, alizikataa kwa madai kuwa hawezi kupokea wagombea wawili kutoka chama kimoja (Chadema).
Mlalamikaji katika kesi hiyo anadai kwamba alipeleka barua ya kulalamikia hatua hiyo kwa msimamizi huyo, lakini aliidharau, kitendo ambacho kilimnyima haki yake ya kikatiba.

Anadai kwa kufanya hivyo, uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi ikiwemo ya kutozingatia sheria ya uchaguzi namba 343 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002 pamoja na kanuni zake ambazo zipo kwenye tangazo la Serikali namba 279 la mwaka huu.
Aidha, anadai kuwa kwa kushindwa kupokea fomu zake, msimamizi wa uchaguzi alikiuka kifungu namba 38, kifungu kidogo cha 5 cha sheria hiyo ya uchaguzi.

Kwa msingi huo, mlalamikaji anaiomba Mahakama kutamka kwamba kushinda bila kupingwa kwa Filikunjombe ni batili na uchaguzi mdogo urudiwe.
Pia, anaiomba Mahakama itamke kwamba tamko kuwa Filikunjombe alipita bila kupingwa ilikuwa ni batili na ombi lake la tatu ni kwamba Filikunjombe na washitakiwa wengine katika shauri hilo, warejeshe gharama za kesi na gharama nyingine ambazo Mahakama Kuu itaona zinafaa.
CHANZO: NIPASHE

Safi sana mtitu usimuachie huyo. Ila kuwa macho kwani jamaa anajua kucheza na rushwa huyo atawahonga watu kibao kama alivyohonga Ludewa kwa kuwanunulia pombe na na kumuhujumu prof. Mwalyosi hadi akaonekana hafai wakati alijitahidi sana kutuletea maendeleo. Alinunu kadi za CCM akawapa wanafunzi yaani huyu Deo hamna kitu. Nipo pamoja nawe katika hili na naamini ukijipanga vizuri utashinda kwani ni mungu yu pamoja nawe na kafanya dhambi sana kumuhongo msimamizi wa uchaguzi ludewa na yule aliyejifanya ni CHADEMA akaenda kuchukua form za kugombea wakati ahana hata barua. Jipange utuokoe wana Ludewa huyu Filkunjombe njaa zake na fitna zake ndiyo zitatumaliza wanaludewa.
 
Mbalinga

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
1,705
2,000
Safi sana Mtitu, lakini katika hoja zako nilitamani uweke kipengele cha katiba kinachosema kuwa mbunge atakuwa wa kuchaguliwa, kwa hiyo hakuna kitu kama kupita bila kupingwa. Mzee Mwanakijiji anajua sana kuiweka hii point
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom