Ushindi wa kishindo CCM lazima -Msekwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushindi wa kishindo CCM lazima -Msekwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jun 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Na Yassin Kayombo, Kibaha
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kina uhakika wa kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kutokana na kukubalika kwa wananchi na mikakati yake thabiti ya kufanikisha azma hiyo. Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, alisema hayo jana, alipofungua semina elekezi ya Makatibu wa CCM wa wilaya na Makatibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya za Kibaha Vijijini, Kibaha Mjini, Bagamoyo, Rufiji, Mkuranga, Mafia na Kisarawe, zilizoko mkoa wa Pwani. Semina hiyo ya watendaji wa Chama iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa, ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na rais unaotarajia kufanyika Oktoba 31, mwaka huu. Msekwa aliitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa, mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005/2010, mipango ya upatikanaji wa fedha za kampeni, uteuzi wa wagombea wanaokubalika, uzoefu wa uchaguzi katika mfumo wa vyama vingi vya siasa tangu mwaka 1961 na utaratibu wa kubadilisha mgombea wa urais kila baada ya miaka 10. Alisema CCM imejiwekea utaratibu wa wazi wa kukusanya fedha za gharama za uchaguzi, ikiwemo ununuzi wa vifaa (yakiwemo magari) kwa kuwashirikisha wanachama na wapenzi kuchangia kwa kutumia simu za mkononi na kuandaa hafla za kuchangisha fedha katika ngazi mbalimbali. Kuhusu utekelezaji wa Ilani, Msekwa alisema wana-CCM hawana budi kwenda kifua mbele kwa kuwa imefanikiwa kuzisimamia serikali kuitekeleza na kwamba, hakuna Mtanzania asiyefahamu hilo. Kutokana na mafanikio hayo, alisema CCM imeweka mikakati ya kuandaa na kuinadi kwa wananchi Ilani itakayotekelezeka kwa kipindi cha mwaka 2010/2015. Msekwa akizungumzia uteuzi wa wagombea katika nafasi mbalimbali, alisema kupanuliwa kwa demokrasia ndani ya Chama kwa kuruhusu wanachama wote kupiga kura za maoni kuwachagua wagombea, CCM ina uhakika kuwa, watachaguliwa wanachama wenye sifa za uongozi na wanaokubalika katika maeneo husika. Hata hivyo, aliwakumbusha wanachama, wapenzi wa CCM na wananchi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa wale ambao bado wana fursa ya kufanya hivyo, ili waweze kuwapigia kura wagombea watakaoteuliwa na Chama. Wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Msekwa alipata fursa ya kukagua madaftari ya wapiga kura wa CCM ya matawi mbalimbali yaliyoko wilaya za Kibaha Mjini na Kibaha Vijijini. Alitoa wito kwa wanachama ambao hawajajiorodhesha kufanya hivyo haraka, ili waweze kushiriki kupiga kura za maoni. Msekwa alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi kuhusu kata mpya zaidi ya 700 zilizoongezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Alisema uongozi wa kata zilizogawanywa utaratibu uchaguzi katika kata hizo, kazi ambayo inatakiwa ikamilike kabla ya kura za maoni.


  Ushindi wa kishindo CCM lazima -Msekwa
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,105
  Trophy Points: 280
  Wizi wa kura kwa kishindo 2010 utakaofanywa na CCM ni lazima.
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Mwizi anapofikia hatua ya kutangaza matendo yake hadharani bila woga hili ni tatizo kubwa sana.
   
 4. d

  damn JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  na hatari kubwa sana kwa kizazi kilichopo na kijacho. Is this our way of life?
   
 5. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ufedhuli, ubwanyenye, ukabaila,ufisadi na wizi wa kishindo kwa ccm 2010
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  source: Uhuru=ccm propaganda za kushindwa
   
 7. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kiburi kikikomaa na kubeba mimba huzaa DHAMBI, dhambi Ikikokamaa hubeba mimba na kuzaa MAUTI. Siombi tufike mahali dhambi itunge mimba maana kitakachozaliwa sitamani kukiona! na lazima CCM waelewe tu kila palipo na mteremko pana mpando pia! ipo siku nayo yaja CCM watalazimika kukwea mpando huo sasa hivi waache watambe kwa kuwa wanateremka!
   
 8. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  KWA HAKIKA KILEMBWE UMENENA! '' TAZAMA SIKU YAJA NAYO YAJA UPESI PALE AMBAPO CCM ITATAMANI MILIMA IIANGUKIE LAKINI HAITAWEZEKANA! ARDHI IFUNUKE IIFUKIE LAKINI HAITAWEZEKANA, SIKU HIYO YAJA TENA YAJA UPESI CCM AMBAO WAMEFANYA DHAMBI KWA MUDA MWINGI;KUWANYIMA WADANGANYIKA HAKI ZAO HUKU WAKICHUMIA MATUMBO YAO; TAZAMA NYOKA NA NGE ZITAWATAFUNA SIKU HIYO..CCM WAOMBE WAKATI HUO USIWE KIPINDI CHA BARIDI...MAANA HATA MAKOTI YA KUVAA WATAKOSA...Ole wao wasipotubu na kuamini maneno haya ya Malaaika!
   
 9. Elisante Yona

  Elisante Yona Senior Member

  #9
  Jun 3, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 130
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Habari Wapendwa wa jukwaa la Siasa,

  Mimi ni mchambuzi wa masuala ya siasa,lakini sio mshabiki wa chama chochote,

  Lakini ukweli ndio huo,uchaguzi wa 2010 kwa CCM,Sio mteremko,kwa sababu kama kweli ni muelewa wa mambo jiulize kwamba Mheshimiwa kashinda kwa kishindo mwaka 2005,sawa,lakini kaifanyia nini Tanzania na wananchi wake,ili tena ashinde kwa kishindo,

  Mheshimiwa makamu mwenyekiti Bara hana mkakati wowote ila anatumia propaganda tu,na hawa CCM watapata shida sana kwenye kampeni za uchaguzi mwaka huu na wanaweza kuifilisi nchi kwa rushwa ili waweze kushinda kwa kishindo.

  Mwenye macho haambiwi tazama,tumia kura yako vizuri ee Mtanzania,

  Mungu Ibariki Tanzania na simamia haki ipatikane.

  Elisante Yona
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Thieves...!!!
   
Loading...