Ushindi wa Kikwete faraja kubwa mafisadi, tuhuma yabatizwa mambo ya makandokando!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,056
22,755
Uchakachuaji wa kura uliompa Kikwete ushindi umeleta faraja kubwa kwa mafisadi na kuwapa jeuri ya ajabu kama tunavyoanza kushuhudia. Moja wao, vijisenti, ametoa mpya kwa kubeza tuhuma zinazomkabili kama mambo ya makandokando. Nyuso zilizokuwa zikifichwa kwa aibu sasa zaanza kujitokeza hadharani na kuwatambia Watanzania bila hofu. Kwa miaka mitano ijayo, ndugu Watanzania heri tuanze kufunga mikanda kwani kuna dalili za walafi kukomba hadi uji wa mtoto.
 
Makandokando! Huyu jamaa akiwa spika, hapo bungeni hakutakuwa na cha maana. Hivi zee hili la kisukuma likoje?
 
Hivi hata hiyo serikali imeshindwa kumwuliza alikopata hayo mabilioni na kuyaweka huko nje? kwa nini asiyaweke Tanzania? Wakati wa Mzee wetu Nyerere huyu jamaa angeingia kwenye kapu la kustaafishwa kwa manufaa ya umma. Lakini sasa hivi mtashangaa anapewa nafasi ya juu kabisa (Ya uspika) wakati hata ile kesi ya ajali haijaisha. Hakimu gani asiyependa watoto wake wapate chakula atamhukumu spika hata kama ataona kuna kosa? Jamani hivi tunaelekea wapi? Kama ingekuwa ulaya au Marekani, mtu mwenye kesi ya namna hiyo anagombea uspika bila aibu. Jamani CCM toeni tamko. CCM inaona watanzania kuwa Mataahira? Kama hayo mabilioni ameyaita vijisenti, hizo senti ziko wapi? Mwenye kujua atupashe
 
mwanzo wa kuona maajabu ni huu usijeshangaa karamaji anakuwa mkuu wa moa na Edo anwania kiti cha Urais 2015
 
Nyie tulieni tu msikilize uteuzi wa wabunge viti maalum, baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa wizara na halmashauri. Mtashuhudia madudu. mafisadi watajaa hadi walioko jela watatolewa kwa msamaha wa rais na kupewa vyeo. Hii ndiyo tanzania ya JK bwana.
 
Mkishangaa ya Salma, subirini ya Kikwete.
Mkishangaa ya Kinana, subirini ya Chenge.

Mkishangaa ya Makamba, subirini ya Bilali.
Mkishangaa ya Ridhwani, subirini ya Januari.

Mkishangaa ya Lowassa, subirini ya Rostamu
Mkishangaa ya Makame, subirini ya Kiravu

Mafisadi washika hatamu, Watanzania kazi tunayo.
Ni maumivu mtindo moja kwa miaka mitano ijayo.

Ingawa wamelikoroga wao, lakini wa kulinywa ni sisi.
Kwa uchaguzi wetu wenyewe, tumejipa laana halisi.

Watanzania tutamlilia nani ?

Mkuu thanx, shairi limetulia na nimekubali.
masikitiko makubwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom