Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,414
- 23,595
Uchakachuaji wa kura uliompa Kikwete ushindi umeleta faraja kubwa kwa mafisadi na kuwapa jeuri ya ajabu kama tunavyoanza kushuhudia. Moja wao, vijisenti, ametoa mpya kwa kubeza tuhuma zinazomkabili kama mambo ya makandokando. Nyuso zilizokuwa zikifichwa kwa aibu sasa zaanza kujitokeza hadharani na kuwatambia Watanzania bila hofu. Kwa miaka mitano ijayo, ndugu Watanzania heri tuanze kufunga mikanda kwani kuna dalili za walafi kukomba hadi uji wa mtoto.