Ushindi wa hoja wa benjamin mkapa - kigoda cha mwalimu nyerere nkurumah | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushindi wa hoja wa benjamin mkapa - kigoda cha mwalimu nyerere nkurumah

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bona, Apr 22, 2012.

 1. bona

  bona JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Niangalia kupitia TBC mdahalo wa kuadhimisha kigoda cha mwalimu nyerere uliofanyika nkurumah udsm, nilishangazwa ni umahiri wa rais mstaafu benjamin william mkapa ktk kuchambua na kuweka hoja mezani hadi waandishi na wachambuzi mashuhuri nchini wakasuuzika na roho zao akina jenerali ulimwengu, makwenga wa kuhenga, prof. isa shivji walishindwa kabisa kumu outclass mkapa hadi wakajiona ni wachanga ktk uchambuzi, mkapa aliweka mchele na pumba pembeni akatofautisha fact na feelings ktk suala zima la maendeleo ya nchi yetu na sera zake alizozitekeleza, nilipata picha mkapa probably was the best president this country has ever had, poitns ambazo mkapa alichukulia points ni kama

  1. tulibinafsisha kwa sababu mashirika yalikua mufilisi na serikali haikua na mitaji ya kuendesha so it was inevitable yauzwe.
  2. ktk mashirika zaidi ya 300 yaliyobinafsishwa zaidi ya 150 yalibinafsishwa kwa wazawa 100% ambayo yalikua hayazalishi kabisa, zaidi ya 20 yaliyokau kidogo yanazalisha kwa wageni lakini serikali kubaki na shares na zaidi ya 20 yaliyokua hayazalishi kwa wageni 100% kwa iyo watanzania wameshirikishwa na wamepewa chance!

  3. ktk mashirika waliyopewa watanzania 100% mostly hayaendi vizuri na hayachangii significantly kwa pato la taifa ila yaliyobinafsishwa kwa wageni almost all yanafanya vizuri na ndo yanayochangia pato la taifa.

  4. tatizo kubwa mashirika kuendeshwa na wazawa management ni mbovu, soko lipo ila management ni poor hata yaliyobaki yanayoendeshwa na wazawa yanastruggle hata sasa!

  5. toka tumebinafsisha tunapiga tu kelele lakini ni viwanda vingapi vipya vimeanzishwa? tunapiga kelele bure kuanzisha viwanda hatuwezi.

  6. kuhusu soko huria, aliuliza je watanzania tuna utashi wa kisiasa kwa mfano tuseme tufufue viwanda vyetu vya nguo na tupige marufuku nguo za nje tuvae kaniki mpaka viwanda vyetu viweze kuzalisha nguo za kututosha! tutakubali?

  7. kuwabishia wazungu ni ngumu kama hatuwezi hata kujihakikishia chakula so huwezi pewa heshima ktk jumuia ya kimataifa kama your no body!

  8. hatuna rasilimali watu kuweza kuendesha vitu wenyewe!
   
 2. B

  BMT JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  NAFIKIRI AMEKATA MZIZI WA FITINA,isupport u that Mzee Mkapa was the best president in TANZANIA,na kwa hawa waliobakia sidhani kama kuna atakayefikia uwezo wake wa kiuongozi kwenye taasisi ya urais
   
 3. bona

  bona JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  nadhan ugumu wa maisha unaozidi kuongezeka hapa nchini ndio tutazidi kukumbuka maneno ya huyu mzee, ukweli na uwazi! kuliko sasa hamna vision ni usanii tu kila jambo linafanyiwa kazi kisanii media nazo zimeingia kweney huo uozo, sioni mediao inayo report hasa data za ugumu wa maisha kama inflation rate sasa imefika ngapi? investment mpya nchini ni zipi? deni la taifa sasa likoje? nk
   
 4. D

  Dr Amri Mabewa Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nilimsikiliza mheshimiwa Mkapa vizuri sana,nilichobaini ni kwamba kama tukipata viongozi angalau watano tu kwenye serikali,hali ya maisha yetu ingekuwa nzuri sana.na wasomi tunatakiwa kujenga hoja kama mzee Mkapa
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kwenye red. Ila tunarasilimali watu wenye ujuzi wa kuwaibia Watz na wale wengine wa kuwalinda! Hao tunao kibao!

  Mkapa is quite boring -- kuna mengi anatakiwa awaeleze Watz: Alikuwa wapi wakati wezi wa EPA wanafanya vitu vyao, vipi aliuza nyumba za serikali bila ya utaratibu wa kanuni za kiserikali, vipi alijiuzia mgodi etc etc.

  Mimi naamini kuna siku atakuja kutuambia kwamba wanaohoji wizi wa EPA waulizwe wenyewe walioiba!
   
 6. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hivi management ya kiwira iliongozwa na nani?
   
 7. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hapo utawadanganya ambao hawakuona kigoda cha mwalimu, kwa tulioona tuliona tofauti na mawazo yako, mkapa alibanwa sana kwa tuhuma za kuiibia serikali, alipaniki sijawahi ona, wachangiaji wote walionyesha ukomavu kwenye maswali waliyomtwanga! Sasa hiyo habari yako sijui umeitoa wapi??
   
 8. B

  BMT JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  COUNTERPUNCH,nenda kajipange uje upya,95% ya watanzania wanamkumbuka huyu mzee we vpi au ukusikiliza kigoda cha mwl kupitia tbc maana umekurupuka tu cjui unatokea wapi
   
 9. Kelvin mwalukas

  Kelvin mwalukas Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 25
  kwa kawaida jf is the home of great thinkers, how comes uzi kama hu ukaletwa na m2 anaejiita great thinker? Kifupi niliudhulia kigoda cha mwlm, bwm ni mkwepaji maswali na mbabe, tz tulikua na rais 1 tu, Nyerere Julias Kambalage bas. (ijapokua alikua na mapungufu lkn ya kibinadamu zaidi na yanayosameheka) Waliobaki nashauri ianzishwe mahakama maarum huru 2washitaki. Bona rudi fanya research ya kutosha ndo upost hapa, la sivyo niliyoyaongea yanakuzidi upeo.
   
 10. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtoa hoja ameweka masuala yaliyomfanya amuone Mkapa bora.

  Wewe great thinker chambua hizo hoja kwa kuzipinga au kukubaliana kisha na tuwekee hapa maswali ambayo aliulizwa akayekwepa ikiwezekana jinsi alivyobanwa. Mwishowe utoe ushauri wako na comment yako. Hapo juu umeonesha hisia zako na sio uhalisia kwa kupingana na hoja.
   
 11. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hata tukimtukana mkapa matusi ya nguoni! ukweli utabaki kuwa ukweli!
  Mkapa alikuwa kiongozi mwenye kujua nini anakifanya kwa ustawi wa baadaye wa Tanzania na Watanzania.
  Mfano TBL ilikaribia kufungwa kutokana na ushindani wa bia za Kenya na Rwanda, baada ya kubinafshwa wakenya na bia zao wameingia mitini.
  Makusanyo ya Kodi yaliendana na uboreshaji wa huduma za jamii. Leo hii Kodi inakunywa kubwa na sambamba na ugumu wa maisha kuongezeka.
  Tatizo JK na kundi lake wameingia madarakani kwa kumchafua ili watanzania wawe busy kumshambulia huku wao wakificha madudu yao.
  Leo hii tumekalia majungu na fitna bila kuangalia uhalisia wa mgao wa pato la taifa.
  tumeshupalia mkapa kajigawia mgodi wa kiwira kwa kuangalia neno anben pasi kujiridhisha authenticity zake.
  BILA KUUMA MANENO NAMSIFU MKAPA KWA KAZI ALIYOIFANYA KATIKA HILI TAIFA BILA KUJALI WENGINE WATASEMA NINI!!
   
 12. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Nilichokubaliana na huyu Mzee kwenye Kigoda cha mwalimu ni kwamba tumekuwa watu wa kulaumu bila solution, hatuna vision, tunakwenda kama vipofu.., mfano mmoja mzuri ni kwamba kama soko lipo na uwezo upo, kwanini tusianzishe viwanda ? (mfano mzuri ni sukari) demand ipo, uwezo wa kuzalisha upo.., ila bado tunakazania importation..

  To put it bluntly hii serikali na viongozi wote wana upeo mfupi sana (tunakalia tu Mkapa mwizi na sijui nini), Sawa Mkapa alikuwa Mwizi, hawa ambao sio Wezi (au ni Wezi) wanafanya nini sasa ?, Wanachojaribu kufanya hawafanyi research (mfano power tillers)..

  Kwahio swali ni kwamba je privatisation ni mbovu, au management ndio mbovu au system ya kusimamia ndio mbovu. Inabidi ifike wakati tuangalia what is wrong au kwanini something is not working (sera zilikuwa mbovu, Mkapa alikuwa hafai, au ni nini ilibidi kifanyike).
   
 13. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkapa was the best!!
   
 14. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jamani ebu acheni kulifagili hili JIZI!!! hali tulionayo leo ni sababu ya JIZI hili yani huu ni mwendelezo wake tu! Maneno yake yaliyonyooka ni tabia tu ya Kitapeli
  Hili ni jizi litaalamu ndiyo maana linaweza kuwashawishi mlipongeze! majizi kama haya wenzetu uko majuu hawayaiti majizi! bali MAJIZI MATAALAMU.
   
 15. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mlevi utamjua tuu! Kwani kiwanda cha bia kingekufa tungepungukiwa nini?? Yani ni bora wewe uvae mitumba kwa kutokuwa na kiwanda cha nguo lakini unye bia! Masaburi wewe!!!
   
 16. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Naombanipangue hoja za huyu mtu moja baada ya nyingine.
  Utanguluzi
  Hivi kwanini uongozi wa CCM hawawi consistent kwenye uongozi wa uchumi wa nchi nyetu hadi leo?
  Nyererealitaifisha na kujenga baadhi ya viwanda (UFI) hali ya maisha ya kwaida yawatanzania ilikuwa afueni hasa kwa wale ambao walifaidika na ajira na sisiwakulima.
  Mwinyialitoa ruksa na kuweka misingi ya sera ya soko huria lisilokuwa na usimamizi.Ya Nyerere aliyatelekeza. Ni mategemeo ya baadhi yetu kuwa angesahihisha yalemabaya ya mtangulizi yake na kuyapalilia mema. Miaka ya Nyerere ilitoswa kwenyedust bin kwa maana focus ya Nyerere kuwanufaisha wote kwa usawa; mwinyi alianzakuwatosa wasio na uwezo wa kiuchumi
  MkapaBalaa tupu. Hakuwa na huruma na wananchi ila kuzingatia ushauri wa wazungu waliokuwawanaitamani nchi.
  1. tulibinafsisha kwa sababumashirika yalikua mufilisi na serikali haikua na mitaji ya kuendesha so it wasinevitable yauzwe.
  Napendamnaoweza mpate majibu toka kwa Mkapa haya mashirika yalifilisiwa na nani?
  Kwa niniiwakati wa kuyabinafsisha serikali ilitumia pesa kuyainua thamani?
  Na kwanini waliobinafsishiwa ni watu fulani tu waliokuwa na uhusiano na utawala?
  Kwa ninimwenendo mzima haukuwa shirikishi angalau taarifa kwa umma?
  NBSilikuwa mfilisi au ilikuwa njama?
  Vipiwakulima walifaidika vipi na ubinafisishaji?
  Majibu yoyote atakayotoa kama mwananchi naona alituingiza mkenge katurudisha nyuma nakufuta cho chote tulichokuwa nacho kama anavyokiri.
  2. ktk mashirika zaidi ya 300yaliyobinafsishwa zaidi ya 150 yalibinafsishwa kwa wazawa 100% ambayo yalikuahayazalishi kabisa, zaidi ya 20 yaliyokau kidogo yanazalisha kwa wageni lakiniserikali kubaki na shares na zaidi ya 20 yaliyokua hayazalishi kwa wageni 100%kwa iyo watanzania wameshirikishwa na wamepewa chance!


  Alitoachance kwa watanzania ambao alijua anajua hawana uwezo wa kuyamanage. Kwa lughanyingine alikusudia kuyaua kupitia kwa wazawa ili wasimlaumu kwa hila alizokuwanazo za kujinufaisha yeye na jamaa zake nakuwaacha wananchi tufe kwa kupotezahata kidogo tulichokuwa nacho. NBC, Reli, Shirika la posta na simu, General Tyres.etc
  Hali yahayo mashirika yalivyo ndicho kilikuwa lengo zima la zoezi hilo? Anatoasuluhisho gani hata kama kukiri kuwa alikosea ni suluhisho.
  3. ktk mashirika waliyopewawatanzania 100% mostly hayaendi vizuri na hayachangii significantly kwa pato lataifa ila yaliyobinafsishwa kwa wageni almost all yanafanya vizuri na ndoyanayochangia pato la taifa.
  Sawalakini ndiyo lilikuwa lengo la ubinafishsaji kuwa wageni ndio wafaidi kwasababu wana uwezo? Maana yake zoezi zima lilikuwa limeelekezwa kuondoa uchumiwa kitaifa kuweka kwa wageni kwa kuwa wazawa hawana uwezo, na hasa palewananchi wakawaida walipowekwa kando kushiriki kwenye uchumi. Hapa serikali (yaovyo) ilijipachika majukumu ya kusimamaia uchumi badala ya wananchi


  4. tatizo kubwa mashirikakuendeshwa na wazawa management ni mbovu, soko lipo ila management ni poor hatayaliyobaki yanayoendeshwa na wazawa yana struggle hata sasa!
  Moja ya sababuza ubinafishaji ilikuwa kuwaondoa wazawa wasiokuwa na uwezo wa kuongozamashirika na kuyafanya yazalishe. Mbona hilo likiwa linajulikana wamepewawasiokuwa na uwezo wa kuyabadirisha yawe na tija? Bado inathibitisha dhamiri yaubinafisishaji ilikuwa kuwapoka wananchi na raslimali zao kwenye mashirika
  5. toka tumebinafsisha tunapiga tukelele lakini ni viwanda vingapi vipya vimeanzishwa? tunapiga kelele burekuanzisha viwanda hatuwezi.
  Hakunaviwanda vilivyoanzishwa kwa sababu hakuna uzoefu wa uongozi, wataalamu, serarafiki chini ya mtazamo potofu kuwa wageni tu ndio wanaweza. Hakuna mahali po pote baada ya vision yaNyerere ya kuanzisha viwanda ambapo Human Resource ilikuzwa kubeba jukumu laindustralisation. Wale waliotayarishwa na mwalimu eg ceramics, clotheswaliishia kuajiliwa kama makolokoloni. Na serikali yake kuwakeji kuwa siwabunifu. Kweli hatuwezi kuanzisha viwanda kwa sababu tumepokwa na bmaamuziyake mabovu ya kauzibe na kimaskini ya kujibinafisishia mali za watanzania.
  Swali dogo tu alikuwa na mkakati gani wakuwatayarisha wataalumu kwenye nyenja zote za viwanda?
  6. kuhusu soko huria, aliuliza jewatanzania tuna utashi wa kisiasa kwa mfano tuseme tufufue viwanda vyetu vyanguo na tupige marufuku nguo za nje tuvae kaniki mpaka viwanda vyetu viwezekuzalisha nguo za kututosha! tutakubali?
  Si sualala utashi wa kisiasa tu yeye alipata wapi utashi wetu wa kuingia soko huria naubinafisishaji? Viwanda vile vitarudishwa tu kama siyo sasa baadaye maana hilisoko letu kwa bidhaa hafifu za wageni hata siku moja halitachangia kwenyeuchumi. Yeye ataingia kwenye historia ya rais aliyeshindwa na sera yake ya ubinafisishajikwa sababu haikutoa matunda yaliyokusudiwa.


  7. kuwabishia wazungu ni ngumu kama hatuwezi hata kujihakikishia chakula so huwezipewa heshima ktk jumuia ya kimataifa kama your nobody!
  Mwisho wakufikiri wa Mkapa na CCM ni hapo anapowaenzi wazungu na kutukatisha tamaa kuwahatuwezi. Hii ndiyo balaa ya mfumo wa CCM uluiojikita kwenye kuenzi wageni nahasa wazungu. Namwambia mbona wazungu wanatutambua na kutuomba ushauri kuhusumambao mengi ya uchumi na wanafanikisha mambo yao kwa ushgauri wa baadhi yetu?(eg Prof Lipumba na sisi wengine tusio na majiana)
  CCM naviongozi wake wote ni janga tu. Ona sasa mrithi wake anavyojiibia akifikirihaonekani. Hakuna taifa duniani lililolenga lipewe heshima bila kujiheshimu.Mkapa anaona tuna hisa na heshima anayopewa huko nje. Anasahau kuwa wanampaheshima baada ya kuwapi uchumi wetu kwenye kisahani bila jasho. He is somebodysisi watanzania ni nobody hata mbele ya jumuiya ya mashariki.

  8. hatunarasilimali watu kuweza kuendesha vitu wenyewe!
  Atoetakwimu za rasilimali watu ambazo hazipo. Anaowataka ni wale around the circleya utawala na CCM. HAWAPO. Lakini tupo wengi tunaonyimwa fursa kwa sababuhatuko kwenye mduwara wa utawala na CCM.
  Mwishokuhitimisha
  Ubinafisishajini janga kama Mkapa alivyojanga.
  Tunawezakugeuza rasilimali tulizonazo kuwa mtaji, kitu ambacho hakiwezekana ndani yautawala wa sasa.
  TUTHUBUTUWALA TUSIMSIKILIZE MKAPA WALA KIO0NGOZI YE YOTE WA CCM WAMEISHIWA NA FIKRA ZAKJIZAWA NA NCHI
   
 17. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu Mkapa hana akili anapouliza ni viwanda gani vipya vimeanzishwa ana maana gani? wakati CCM iliona opportunity ya kuiba hela ni kwenye kuuza? Ingekuwa wana akili ya kuvi maintain tusingekuwa tunahangaika leo hii.

  Ok management kwenye Viwanda ilikuwa mbovu, Kilichomfanya atoe madini yetu kwa bei ya kutupa ni nin? au kwa vile wao ni Matrilionea... Subiri CDM iingea madarakani mtakufa kwa Presha.
   
 18. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  wewe ni mwongo, mkapa alijitahidi sana kujibu hoja, ulimwengu mwenyewe hakuuliza swali ila alisaidia kuulewesha ukumbi na mkapa akamshukuru. Ukumbi wote ulijiandaa kuhusu uwekezaji na aliilezea kwa ufasaha sana na mtiririko ulikuwa kama alivyopanga mtoa maada.
  Mkapa was the best president ever naungana na wachangiaji wengine.
  Epa mhusika mkuu ni Kikwete ndiyo maana hawezi kuchukua hatua alikuwa hana hela za kampeni. Na mkapa akibanwa najua atasema ukweli ndiyo maana mahali ambapo mkapa anatakiwa kutoa ushaidi ikulu huanza kuhangaika ili asiongee naomba waendelee kumprovoke ili aendelee kumwaga ugali watu tupate shule. Mkwer.e hana jipya.
   
 19. d

  dotto JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  yaonyesha udhaifu wa Mkapa na sera yake ya wizi. NBC ilikuwa na kosa gani? Aliiuza kwa bei gani? Yapo mashirika mengi yaliuzwa kwa bei ya wizi
   
 20. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mimibaba naona hata hoja zako mwenyewe unajichanganya mpaka huelewi unazungumzia nini, Mkapa alikuwa the best president with vision to our nation. Hebu fikiria huyu Kikwete anachofanya nini. Watanzania tunachelewa kubishana kuhusu mkapa wakati kikwete anaifilisi nchi. Tatizo hapa naona ni kuwa sisi wabongo ndo wenye matatizo, mawaziri wanaiba kikwete anawatetea, anajiandaa kuongea na wazee wa dsm kubariki wizi. Hebu tuamke Mkapa alikuwa ameweka misingi imara ya utawala bora. Ndiyo maana hata malalamiko hayakuwepo.
   
Loading...