Elections 2010 Ushindi wa Chadema wachafua hali ya hewa CCM Mpanda

Ilumine

Senior Member
Dec 27, 2008
196
4
Chadema%2837%29.jpg

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Wakati wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Mpanda Mjini wakifurahia matokea ya ushindi wa ubunge, Said Amor Alfi, hali si shwari kwa wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo ambao juzi walilazimika kuvamia ofisi za Jumuiya ya Wazazi na ya Umoja wa Vijana (UVCCM) na kufunga milango kwa makufuli, wakishinikiza viongozi wa jumuiya hizo wajiuzulu.
Wafuasi hao waliwatuhumu viongozi hao kwamba wamekisaliti chama hicho katika uchaguzi wa marudio wa ubunge uliofanyika Jumapilili iliyopita na Chadema kuibuka na ushindi.
Wakizungumza kwa jazba, baadhi ya wafuasi hao waliokuwa nje ya jengo la ofisi ya CCM Wilaya ya Mpanda, walisema ushindi wa mgombea wa Chadema umetokana na viongozi hao kukisaliti CCM na kuongeza kuwaCwalipiga kura zilizokipa chadema ushindi ni za wana-CCM.
Aidha, vijana hao walidai kuwa kutokana na hali hiyo hawataki kuwaona katibu wa UVCCM na Jumuiya ya Wazazi kwa madai ya kukisaliti chama.
Katibu wa CCM wilaya ya Mpanda, Jacob Nkomola, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Hata hivyo, alisema CCM wamekubali matokeo hayo na kuongeza kuwa pamoja na ushindi wa Chadema, lakini wao ndio wanaounda Serikali ya halmashauri ya wilaya kutokana na chama chao kupata madiwani wengi.
Aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CCM, Sebastian Kapufi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Mpanda, alisema ataendelea kukijenga chama na ameyapokea matokeo kwa moyo mkunjufu.CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom