Ushindi wa CCM Kigamboni na mkono wa Jeshi


Mnyamahodzo

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Messages
1,858
Likes
236
Points
160
Mnyamahodzo

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined May 23, 2008
1,858 236 160
Katika hali isiyotarajiwa, huku zikiwa zimebakia kata mbili za Mbagala kuwasilisha matokeo yao kwa Msimamizi Mkuu wa Jimbo la Kigamboni, kwenye kituo cha kupokelea matokeo yote ya uchaguzi wa jimbo hilo ambacho ni Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(Mwalimu Nyerere Memorial Academy) faustine Ndugulile alitangazwa kuwa ameshinda ubunge na askari(mjeshi). Akapewa ulinzi na wajeshi kutoka hapo chuo hadi kuelekea pande za Kigamboni (kwamba ni kwake au kwenye ofisi za CCm haikujulikana).

Wakati yanafanyika majumuisho hadi saa 5 asubuhi, Mama Maulida-anna Komu alikuwa amemwacha Ndugulile kwa kura zaidi ya 3000.

Mama Komu alipokwenda ili kutangazwa rasmi kuwa ni mshindi , ndipo tik-tak hiyo ilipopigwa.

Kitu kizuri ni kuwa si yeye wala mgombea wa CUF waliokubali matokeo hayo, pia hawakuweka saini zao.
 
Domo Kaya

Domo Kaya

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2007
Messages
530
Likes
9
Points
0
Domo Kaya

Domo Kaya

JF-Expert Member
Joined May 29, 2007
530 9 0
Hongera sana Ndugulile kwa ushindi wa Kigamboni, hope utatutetea ili Kigamobni yetu irudi mikononi kwetu kutoka kwa wawekezaji. Lakini Jimbo hili bora lingechukuliwa na Wapinzani labda mabadiliko yengewezekana.
 
S

Selemani

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2006
Messages
876
Likes
12
Points
35
S

Selemani

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2006
876 12 35
Ukiacha Unazi wa chama. Be honest for a minute. Dr Faustine au Mama Komu nani atakuwa mbunge bora? Its the same way with Halima Mdee, she was better than yule mama wa CCM. Same thing as yule Profesa wa Chadema wa Ulanga, the guy is brilliant. Dr. Buriani is better than Godbless Lema. Chenge, Prof Maji Marefu and Sugu hawafai kuwa wabunge, regardless wametoka chama gani.
 
Fidel80

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Messages
21,972
Likes
134
Points
145
Fidel80

Fidel80

JF-Expert Member
Joined May 3, 2008
21,972 134 145
Ukiacha Unazi wa chama. Be honest for a minute. Dr Faustine au Mama Komu nani atakuwa mbunge bora? Its the same way with Halima Mdee, she was better than yule mama wa CCM. Same thing as yule Profesa wa Chadema wa Ulanga, the guy is brilliant. Dr. Buriani is better than Godbless Lema. Chenge, Prof Maji Marefu and Sugu hawafai kuwa wabunge, regardless wametoka chama gani.
Wewe unae faa mbona hukugombea ili uwatumikia wananchi?
 
A

ATENGEZEKE

Member
Joined
Oct 25, 2010
Messages
11
Likes
0
Points
0
A

ATENGEZEKE

Member
Joined Oct 25, 2010
11 0 0
Ushindi ni ushindi tu,Mkwezi zake mbili zinazobaki ni za mwenye mnazi,mmeshapewa Kawe na Ubungo finish zinazobaki ni zamwenye mnazi.
 
K

kibunda

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
403
Likes
1
Points
35
K

kibunda

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
403 1 35
Huo ni mtazamo wako. Si lazima uwe sahihi maana uongozi haupimwi kwa mitazamo.
 
Gerad2008

Gerad2008

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2009
Messages
532
Likes
160
Points
60
Gerad2008

Gerad2008

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2009
532 160 60
Usimtukane Mbunge wetu G. lema kwani kufanya hivyo ni kusema Arusha hatuna akili woote tuliomchagua Lema. hatukurupuka hapa hatuchaguai Mbunge wa kwenda kuwa lecturer bungeni bali mwenye uwezo na utashi wa kuyaelewa matatizo ya wananchi na kuyafanyia kazi. Hili halihitaji elimu kubwa. DK. Batilda anaweza kuwa Brilliant lakini kwenye proffessional aliyosomea na siyo kuongoza watu wa Arusha. Sisi tumempima Lema na wasomi wote wakaona anaweza na kama wewe unabisha basi tusubiri na tuone.

Acha kuchambua elimu ya mtu kwa kuangalia uwezo wa Elimu yake. Kama elimu inaweza kuwa ni kipimo cha kuweza kila kitu basi kwa mfano rahisi kabisa tungetegemea kwa kuanzia kuona ndoa zao zikiwa stable kuliko za watu wasiokwenda shule. Ubunge ni uwezo na utashi wa mtu kama sivyo basi akina Mtemi Mirambo, Mangi Sina, Mkwawa na Kinjikitile na wengine wengi wasingeweza kuongoza kwa sababu hawakusoma .
 
Gerad2008

Gerad2008

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2009
Messages
532
Likes
160
Points
60
Gerad2008

Gerad2008

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2009
532 160 60
Pamoja na kukosa elimu nataka nikwambie akina Mkwawa na Mtemi Mirambo na watemi woote maarufu wangekuwepo wangetuongoza vizuri kuliko JK ambaye amesoma
 
T

TanzActive

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2007
Messages
350
Likes
0
Points
33
T

TanzActive

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2007
350 0 33
Hongera sana Ndugulile kwa ushindi wa Kigamboni, hope utatutetea ili Kigamobni yetu irudi mikononi kwetu kutoka kwa wawekezaji. Lakini Jimbo hili bora lingechukuliwa na Wapinzani labda mabadiliko yengewezekana.
HIVI NDIVYO MBUNGE ANVYOCHUJWA
KURA ZA MAONI NDANI YA CHAMA = UNAOSEMA HAWAFAI WALIPITA
MCHUJO WA NEC = UNAOSEMA HAWAFAI WALIPITA
KURA ZA WANANCHI = UNAOSEMA HAWAFAI WALIPITA
MAPAMBANO ZIDI YA UCHAKACHUAJI =UNAOSEMA HAWAFAI WALIPITA
KUPIGWA MABOMU NA POLISI =UNAOSEMA HAWAFAI WALIPITA
KUPEWA HONGO NA CCM(400Million -900Million) ILI WAACHIE =UNAOSEMA HAWAFAI WALIPITA

Jamani alipita vikwazo hivyo vyote anafaa, amepita katika moto na sasa ni dhahabu safi
 
PAS

PAS

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2010
Messages
452
Likes
3
Points
35
PAS

PAS

JF-Expert Member
Joined May 3, 2010
452 3 35
Ukiacha Unazi wa chama. Be honest for a minute. Dr Faustine au Mama Komu nani atakuwa mbunge bora? Its the same way with Halima Mdee, she was better than yule mama wa CCM. Same thing as yule Profesa wa Chadema wa Ulanga, the guy is brilliant. Dr. Buriani is better than Godbless Lema. Chenge, Prof Maji Marefu and Sugu hawafai kuwa wabunge, regardless wametoka chama gani.

kinyeo wewe

:nono::nono::nono::nono::nono::nono:
 
Mnyamahodzo

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Messages
1,858
Likes
236
Points
160
Mnyamahodzo

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined May 23, 2008
1,858 236 160
Ukiacha Unazi wa chama. Be honest for a minute. Dr Faustine au Mama Komu nani atakuwa mbunge bora? Its the same way with Halima Mdee, she was better than yule mama wa CCM. Same thing as yule Profesa wa Chadema wa Ulanga, the guy is brilliant. Dr. Buriani is better than Godbless Lema. Chenge, Prof Maji Marefu and Sugu hawafai kuwa wabunge, regardless wametoka chama gani.
Selemani, huenda ukawa hujui ama unajifanya hujui wakati haujui kweli. Katafute gazeti la RAI la tarehe 20,27 na 3 april 2008 sambamba na Mwananchi ya wiki hizo usome vizuri.

Mbogela: said:
Re: Cd4 Count And Sd Bioline, Moh

Prof. Mwakyusa anaswa tena na mtego wa mafisadi
na mwandishi wetu

KWA mara nyingine tena, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa David Mwakyusa amewashangaza wanasayansi duniani kwa kukubali kunaswa na mtego wa mafisadi na kutangaza ripoti ya uongo kuhusu kipimo cha Capillus na mashine ya kupima chembechembe za damu (CD 4) inayojulikana kama Cyflow.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Profesa Mwakyusa aliwaambia waandishi wa habari kuwa kamati aliyounda zaidi ya mwaka mmoja uliopita kuchunguza kashfa ya vipimo vya kupimia ukimwi (HIV rapid Test Kit) na mashine ya kupimia chembechembe za damu, aina ya CD 4, ilibaini kuwa kipimo cha Capillus kinafaa kutumika hapa nchini na kuongeza kwamba mashine ya Cyflow haina ubora wa kutosha.

Alisema mashine hiyo inayotengenezwa nchini Ujerumani, haina uwezo wa kupima chembeche za CD4 zikiwa chini ya 200.

Taarifa hiyo ya Dk. Mwakyusa, inayotokana na ripoti mbili tofauti za kamati moja aliyoiunda na zote mbili zikipingana, moja ikisema kuwa uchunguzi uliofanywa Muhimbili uligubikwa na rushwa, na nyingine ikisema hakukuwa na rushwa kabisa.

Kamati yake iliyokuwa na watu watatu tu, ilitoa ripoti mbili tofauti zinazopingana; moja ikisema tathmini ya mashine ya Cyflow iliyofanywa na Hospitali ya Muhimbili Akizungumza na waandishi wa habari, Profesa Mwakyusa hakugusia kabisa suala la ripoti hizo mbili, wala kupingana kwake. Na hakuonyesha kabisa kwamba kulikuwa na ripoti mbili tofauti mezani kwake.

Katika mkutano huo, Mwakyusa aliitumia ripoti iliyoficha ufisadi bila kuzingatia kwamba ni yeye mwenyewe aliyewabadilisha vituo vya kazi, watu wote waliohusika katika kashfa hiyo na kuviahidi vyombo vya habari kuwa suala hilo angelikabidhi mikononi mwa PCCB.

Taarifa ambayo inapingana kabisa na utafiti uliofanywa na wanasayansi kutoka mabara yote duniani. Utafiti huo kutoka vyuo vikuu kadhaa vinavyoheshimika duniani kote, unaonyesha kuwa Cyflow, ni moja kati ya mashine bora duniani za kupima chembechembe za damu mwilini. Ni chuo Kikuu cha Muhimbili peke yake duniani kilichofanya tathmini na kuonyesha kuwa mashine hiyo ina udhaifu.

Mmoja kati ya wanasayansi waliompa changamoto Profesa Mwakyusa ni Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Utafiti wa Magonjwa (National Institute for Medical Research) Dr. John Changalucha ambaye amesema yeye ameitumia mashine hiyo kwa muda wa miaka miwili sasa na inampa matokeo mazuri kabisa kama alivyotarajia.

Akizungumza na Rai kwa njia ya simu, Dk. Changalucha alisema tangu mwishoni mwa mwaka 2005, amekuwa akiitumia mashine hiyo aina ya Cyflow na inawasaidia sana katika utafiti wa TB na inafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.

"Ni mashine ndogo na rahisi kuitumia. Inafanya kazi tofauti na udogo wake,"alisema Dk. Changalucha.

Alisema pamoja na yeye kuitumia mashine hiyo, amekuwa akisoma kutoka kwa wanasayansi wenzake duniani taarifa mbali mbali za ufanisi wa mashine hiyo na hizo ndiyo zinamwongoza kama mwanasayansi.

Dk. Changalucha alitoa changamoto kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kuiweka hadharani ripoti ya tathmini iliyofanywa na Chuo Kikuu cha Muhimbili ili wanasayansi wengine waweze kujua wenzao wa Muhimbili walivyofanya.

"Hivyo ndivyo wanasayansi tunavyofanya. Tunaongozwa na documentations. Tunaposema Cyflow inafaa, tumewasoma wengine. Tunaposema FactsCount inafaa ni baada ya kuwasoma wengine. Hatusikilizi vipande vinavyotolewa kwenye press conference. Tunaitaka ripoti nzima tuisome wenyewe kisayansi. Hiyo ndiyo sayansi," alisema Dk. Changalucha.

Maelezo ya Dk. Changalucha yanafanana na maelezo ya mabingwa wengine kutoka taasisi kadhaa duniani ambazo zimethibitisha ubora wa mashine hiyo.

Ingawa Profesa Mwakyusa katika mkutano wake na vyombo vya habari alisema mashine hiyo inatumiwa na nchi za Kiafrika tu, na akashangaa ni kwa nini, Rai inaweza kuthibitisha kuwa Profesa Mwakyusa ni mwongo kwani uchunguzi wetu umebaini kuwa inatumiwa katika mabara yote duniani.

Tofauti na maelezo ya Profesa Mwakyusa kwamba mashine hiyo inatumiwa katika nchi za Afrika tu, Rai imegundua kuwa baadhi ya taasisi muhimu zinazotumia mashine hiyo nje ya Afrika ni pamoja na Harvard School for Public Health, Boston, Marekani,

Taasisi ya Human Virology, Chuo Kikuu cha Baltimore, Maryland, Marekani,

Taasisi ya Microbiology, na magonjwa ya kitropiki, Antwerp, Ubelgiji, Taasisi ya Croix-Rouge Française, Paris, Ufaransa,

Maabara ya Kinga ya mwili katika Hospitali ya Pitiè Salpetriere, Paris, Ufaransa.

Nyingine ni Taasisi ya kinga ya mwili, Idara ya Biomedical Sciences, Chuo Kikuu cha Modena na Reggio Emilia, Italia,

Hospitali ya Spallanzani, Rome, Italia,

Taasisi ya Imunolojia katika hospitali ya Pascale, Naples, Italia, Taasisi ya Immunology, katika kliniki ya Robert-Rössle- Berlin Ujerumani, Hospitali ya Chuo Kikuu cha Bad Oeynhausen, Ujerumani, Hospitali ya Chuo Kikuu cha Lübeck, Ujerumani, Hospitali ya Chuo Kikuu cha Münster, Ujerumani, Wizara ya Afya, huko California, Marekani

Kwa upande wa Afrika, zipo nchi nyingi zinazotumia mashine hiyo ikiwa ni pamoja na Senegal, Cameroon, Ghana, Malawi, Sudan, Rwanda, Kenya, Uganda, Zimbabwe na Bukina Faso.

Huko Nigeria, mashine hiyo inatumiwa na mpango wa misaada wa Rais wa Marekani (PEPFAR).

Kwa upande wa Tanzania, taasisi za kidini zisizoguswa na masuala ya ufisadi zinatumia mashine hiyo ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Kanisa Katoliki, Consolata ya Ikonda, Makete ambayo kiongozi wa Hospitali hiyo Padre Sandro, anasema ilikuwa imeshahudumia wagonjwa 2,000 kwa wastani wa wagonjwa 50 kwa siku.

Hospitali nyingine zinazotumia mashine hii kwa upande wa Tanzania, ni ile ya Tanwat Njombe ambayo kwa mujibu wa muuguzi, Bety Liduke, mwaka jana tu, 2007 ilihudumia watu 1,800. Hospitali nyingine zinazofahamika kutumia mashine hizo ni pamoja na Hospitali ya Brock Bond Njombe, na Peramiho ya Songea.

Wakati Profesa Mwakyusa akisema Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitoa kasoro mashine ya Cyflow, kampuni ya Partec inayotengeneza mashine hiyo inasema siyo WHO bali ni watu mmoja tu katika Idara ya Essential Health Technology (EHT) anayewahujumu kwa faida ya kampuni ya Kimarekani. Kampuni hiyo, imeamua kuliandikia WHO ikilitaka limfanyie uchunguzi ofisa wake, ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Essential Health Technologies mjini Bursseles, Dr. Vercauteren Dk. Gaby Vercauteren.

Katika barua yao ya mashtaka iliyopelekwa kwenye chombo cha kisheria cha WHO na nakala kutumwa kwa Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo, kampuni ya Partec, anataka daktari huyo achunguzwe kwa jinsi alivyohusika katika tathmini ya Muhimbili na anavyoendelea kuipaka matope mashine hiyo.

Kampuni hiyo, pia inataka WHO ichunguze mazingira ya kuajiriwa katika Idara hiyo, Daktari wa Kitanzania, Willy Urassa ambaye wakati wa kuifanyia tathmini mashine hiyo alikuwa akifanya kazi Muhimbili na wanamtuhumu kuhusika katika hujuma hiyo.

Rai imethibitisha kutokana na mawasiano ya barua pepe kwamba Dk. Urassa sasa ni miongoni mwa watendaji katika kitengo cha (EHT) Switzerland. Hatukuweza kupata mawasiliano yake kupitia email yake urassaw@who.int ambayo hadi wakati tukienda mitamboni, alikuwa hajajibu.

Habari zaidi tulizozipata tukienda mitamboni, zinaeleza kwamba Dk. Vercauteren ndiye aliyemwita kazini Dk. Willy Urassa. Sasa Dk. Urassa sasa amehamia Switzerland katika Idara anayoiongoza Dk. Vercaurteren.

Katika ripoti iliyobainisha dalili za rushwa, imeonyesha wazi uhusiano uliokuwapo kati ya Dk. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya na Dk. Vercauteren. Katikati ya tathmini, Dk. Ndugulile alimpelekea Dk. Vercauteren ujumbe wa email ya Desemba 23 mwaka 2005 akimwambia mambo ya siri yaliyoonekana kwenye tathmini ambayo yeye alikuwa hahusiki nayo. Ni Dk. Ndugulile mwenyewe aliyepeleka email hizo kwenye kamati ya Profesa Mwakyusa lakini akiwasihi wasimtaje.

Kitu kinachowashangaza wengi ni kwamba wakati mashine ya Cyflow ililazimika kupitia katika chekeche mara tano katika kipindi cha miezi 12, mashine iliyopewa baraka haijawahi kutathminiwa nchini licha ya sheria kutaka kufanya hivyo. Kwa mujibu wa sheria ya Bodi ya Maabara za Afya za Umma mwakla 1997, na tangazo la serikali namba 226 kifungu kidogo cha 2.5.2 (1)-(v) linalotoa masharti ya matumizi ya kifaa chochote cha tiba, ni lazima kifaa chochote kipate tathmini moja ndani ya nchi, na moja nje ya nchi. Zaidi ya mashine 40 za Facts Count zinazotumika hapa nchini, hakuna hata moja iliyofanyiwa tathmini hapa nchini.

Ripoti hiyo ya awali ambayo Profesa Mwakyusa hataki kuiongelea, inaonyesha kuwa kulikuwepo na mbinu nyingi zilizoandaliwa kuichafua mashine ya Cyflow wakati wa kuifanyia tathmini, jambo ambalo lilisababisha ionekane haina ufanisi wa kutosha. Moja ya mbinu ilikuwa ni kuchelewesha vifaa vyake toka bandarini ambayo ripoti mpya inasema vilicheleweshwa na kampuni inayoitengeneza.

Baada ya matokeo ya tathmini hiyo kutolewa, Oktoba 6, 2005, Dk. Roland Gohde, Rais wa kampuni inayotengeneza mashine hizo na ambaye pia ndiye Mtendaji Mkuu na mtoto wa mwasisi wa mashine hiyo, Profesa Wolfgang Gohde, alilalamikia matokeo hayo akisema: "Uchunguzi wa MUHAS ulichukua kipindi kirefu cha miezi 14 bila sababu na hivyo kusababisha vitendanishi kuisha muda wa uhai wake (expiry) na hivyo kutoa majibu yasiyo sahihi.

Aliongeza: "Ripoti ya MUHAS kwamba mashine ya Cyflow ni dhaifu katika kupima idadi ya CD 4 pungufu ya 200 si sahihi na haiendani na ripoti za wanasayansi wengine maarufu duniani kwa lengo la kuzinufaisha mashine zilizokuwepo za Facs Counter kutoka Marekani."

Baada ya kupigwa marufuku Cyflow, sasa Tanzania imebakiwa na mashine aina ya Facs Counter ambaye kila kipimo kimoja kinagharimu dola 40 za Kimarekani. Gharama ya kipimo cha Cyflow ni dola 2 tu.

Ili nchi kuweza kufikia ufanisi katika upimaji na udhibiti wa virusi vya ukimwi, kunahitajika angalau aina nne za mashine zikiwapo rapid test, CD4 tests, viral load na chemistry analyzers.

Kwa Tanzania, ni mtu mmoja tu Bharat Rajan wa Biocare Health Products ambaye huwa anashinda mara zote tenda zote za kuingiza vifaa hivi. Kampuni hii imekuwa na ukiritiba huu tangu mwaka 1966 na mtu akitaka kuagiza mashine za kupima CD4, ni lazima apeleke proforma invoice kwa Rajan ambaye ndiye anaruhusu mashine hiyo kuletwa ndani kwa masharti kwamba ni lazima iwe Facts Count. Wakati fulani, aliyekuwa Waziri wa Afya, Anna Abdalah aliwahi kuonya maisha ya Watanzania kuwekwa mikononi mwa mtu mmoja.

Source: Gazeti la Rai,3/4/2008.
NEED WE SAY MORE?

Kitu gani kilimtoa Wizara ya afya hata akakimbilia Afrika ya Kusini?
 
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
4,003
Likes
1,443
Points
280
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
4,003 1,443 280
Katika hali isiyotarajiwa, huku zikiwa zimebakia kata mbili za Mbagala kuwasilisha matokeo yao kwa Msimamizi Mkuu wa Jimbo la Kigamboni, kwenye kituo cha kupokelea matokeo yote ya uchaguzi wa jimbo hilo ambacho ni Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(Mwalimu Nyerere Memorial Academy) faustine Ndugulile alitangazwa kuwa ameshinda ubunge na askari(mjeshi). Akapewa ulinzi na wajeshi kutoka hapo chuo hadi kuelekea pande za Kigamboni (kwamba ni kwake au kwenye ofisi za CCm haikujulikana).

Wakati yanafanyika majumuisho hadi saa 5 asubuhi, Mama Mauli-anna Komu alikuwa amemwacha Ngugulile kwa kura zaidi ya 3000.

Mama Komu alipokwenda ili kutangazwa rasmi kuwa ni mshindi , ndipo tik-tak hiyo ilipopigwa.

Kitu kizuri ni kuwa si yeye wala mgombea wa CUF waliokubali matokeo hayo, pia hawakuweka saini zao.
HAIWASAIDII, WAENDE WAKADAI HAKI YAO KORTINI:tape:
 
Mnyamahodzo

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Messages
1,858
Likes
236
Points
160
Mnyamahodzo

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined May 23, 2008
1,858 236 160
Sawia na hilo selemani et al jiulizeni ni watanzania wangapi walikufa na wanaendelea kufa hadi sasa kutokana na maamuzi yaliyotokana na rushwa yaliyofanywa na huyu Dk na wenzake?

Kisha njoo utafute, ukipata tuambie, madudu aliyofanya Mama Komu yanayowagharimu watanzania hadi sasa.
 
Profesy

Profesy

Verified Member
Joined
Jun 24, 2009
Messages
380
Likes
0
Points
33
Profesy

Profesy

Verified Member
Joined Jun 24, 2009
380 0 33
Selemani, huenda ukawa hujui ama unajifanya hujui wakati haujui kweli. Katafute gazeti la RAI la tarehe 20,27 na 3 april 2008 sambamba na Mwananchi ya wiki hizo usome vizuri.NEED WE SAY MORE?

Kitu gani kilimtoa Wizara ya afya hata akakimbilia Afrika ya Kusini?
AISE ASANTE. Yani hawa watu wazushi. Alafu hio gazeti sio ya Rostam kweli?
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,375
Likes
31,594
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,375 31,594 280
Hongera sana Ndugulile kwa ushindi wa Kigamboni, hope utatutetea ili Kigamobni yetu irudi mikononi kwetu kutoka kwa wawekezaji. Lakini Jimbo hili bora lingechukuliwa na Wapinzani labda mabadiliko yengewezekana.
ni sawa na fisi kukurudishia mfupa
 

Forum statistics

Threads 1,235,910
Members 474,863
Posts 29,240,285