Ushindi wa CCM Igunga: Mchango wa Nape Ulikuwa ni nini?

MashaJF

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
246
119
Bwana katibu mwenezi wa CCM tafadhali naomba unieleweshe kitu kimoja tuu, ni nini ulikuwa mchango wako kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga?
 
The Analyst

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
464
245
Nape anadaiwa kufurahia ushindi kuliko mtu yeyote mwingine nchini kwa kuwa kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi huo kungechangia kuongezeka sana kwa idadi ya wanaoona kichefuchefu kila anapoonesha uso wake. Hiyo kauli ya kuwataka watu waondoke chamani imemsababishia maadui wengi na wenye nguvu kuliko mimi na wewe tunavyoweza kudhania. Inawezekana hata JK mwenyewe anaboreka sana na kiherehere cha Nape lakini anaona noma kumtema mapema kwa kuwa pia ina impact kwa umaarufu wa chama na mwenyekiti wake.
 
Kiungani

JF-Expert Member
Feb 2, 2007
274
70
Bwana katibu mwenezi wa CCM tafadhali naomba unieleweshe kitu kimoja tuu, ni nini ulikuwa mchango wako kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga?

MashaJF, umeibua swali muhimu sana na linahitaji mjadala muafaka.

Binafsi, sidhani kama swali linabidi liwe Nape, kama Nape mtu mmoja, ila linabidi liwe pana zaidi kwa maana ya Nape kama Katibu Mwenezi na Itikadi, NEC Taifa, na kisha Nape kama mshika ofisi hiyo kwa sasa.

Nitaanza.

Tumeona, tumesikia na tumeshuhudia Katibu Mwenezi na Itikadi akinyimwa nafasi kufanya uenezi wa itikadi na sera za chama katika wakati huu muhimu na wa majaribio. Uchaguzi mdogo wa ubunge - Igunga ndiyo nafasi ya kwanza kamili ya Katibu Mwenezi mpya kuonyesha ubora wake wa kuelewa, kunyanyambua na kueleza sera mpya na mageuzi ya chama. Katibu Mwenezi hakuwepo kufanya hivyo.

Tumeona, tumesikia na tumeshuhudia Katibu Mwenezi akizuiwa kufanya ziara yo yote katika jimbo la uchaguzi, hususani ziara itakayoelekea kuonyesha kuwa anashiriki kwa njia fulani katika kampeni na kueneza itikadi au sera za chama. Katibu Mwenezi hakuwepo kufanya hivyo.

Tumeona, tumesikia na tumeshuhudia Katibu Mwenezi akikosa hata fursa ya kuwa na mgombea (photo opportunity) kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na hata baada ya uchaguzi. Katibu Mwenezi hakuwepo kufanya hivyo.

Tumeona, tumesikia na tumeshuhudia Katibu Mwenezi akiwa hana jukwaa lolote la kitaifa kuelezea sera na itikadi za chama hasa katika kipindi hiki cha mpito na mageuzi, siyo tu kwa Igunga hata katika chaguzi za mitaa na kata ambazo aliweza kushiriki. Katibu Mwenezi hakuweza kufanya hivyo.

Kwa wale wenye kumbukumbu na kujua historia ya nafasi hii toka enzi za akina Kolimba, Kingunge, na hata kufikia sasa kwa Nape, inatufanya tujiulize: Je, ni nini nafasi na wajibu wa Katibu Mwenezi na Itikadi - NEC Taifa?

Na pia, ni nini nafasi, wajibu na mchango wa Nape M. Nnauye kama Katibu Mwenezi na Itikadi - NEC Taifa katika mategemeo, matarajio na hatimaye mafanikio ya sera, itikadi na mikakati ya chama kwa sasa na mbeleni?
Sidhani kama ziara na mikutano ya kujitambulisha, na ziara za magazeti na vyombo vya habari, ndiyo mchango wala wajibu wa nafasi hii.

Wachangiaji mnaweza kuanzia na uchambuzi wa Igunga na kuvuliwa kwa magamba, kama mifano ya awali tu.
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
Mkuu si Nnape peke yake. Ungeuliza pia Naibu Katibu Mkuu Bara alikuwa wapi wakati chama chake kinapigania kura huko Igunga!! Haya mambo si madogo.
 
Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
297
Hakupewa nafasi, kadhalilishwa na viongozi wakuu.

Tatizo ni kuwa Nape hajui kuwa kadhalilishwa. Anajisifu kuwa ana mchango katika ushindi huo badala ya kutafakari kukatazwa kwake.

Nakuhurumia Nape.
 
Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
Nape anadaiwa kufurahia ushindi kuliko mtu yeyote mwingine nchini kwa kuwa kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi huo kungechangia kuongezeka sana kwa idadi ya wanaoona kichefuchefu kila anapoonesha uso wake. Hiyo kauli ya kuwataka watu waondoke chamani imemsababishia maadui wengi na wenye nguvu kuliko mimi na wewe tunavyoweza kudhania. Inawezekana hata JK mwenyewe anaboreka sana na kiherehere cha Nape lakini anaona noma kumtema mapema kwa kuwa pia ina impact kwa umaarufu wa chama na mwenyekiti wake.

View attachment 38434 UJUE NAPE HAKUKANYAGA KABISAAAAA IGUNGA.....(hapa akiwa sokoni Igunga siku mbili kabla ya kufungua kampeni Rasmi)
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
View attachment 38434 UJUE NAPE HAKUKANYAGA KABISAAAAA IGUNGA.....(hapa akiwa sokoni Igunga siku mbili kabla ya kufungua kampeni Rasmi)

Mkuu Nnape hapa si ulienda Igunga kutoa pole tu tena kwa mujibu wa vyombo vya habari (gazeti fulani) vilisema ulienda huko bila ridhaa ya wakuu wako na ati Katibu Mkuu alikukemea? Mimi binafsi sikukusikia kwenye kampeni za Igunga. Labda utuambie hapa nini kilikusibu hadi usiende kueneza sera za Chama ukizingatia kuwa hapo ndipo hasa palikuwa pahala pake. Nilitegemea ungeenda kuwaeleza kuwa tumeanza kuvua gamba na kukitakasa Chama chetu upya kwa hiyo chagueni mbunge mpya.
 
Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
View attachment 38435 "ukivaa nenda kashushe ile bendera yenye rangi ya damu Igunga is for CCM"... sawa kamanda soko lote hili Igunga tuna ijua CCM tu wengine hawa wananogesha harusi. rudi tarehe 03/10/2011 kuja kumchukua mbunge wa CCM
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,743
74,365
Hivi magwanda hamna sera za kuongelea? kila kukicha Nape, Rostam, wamewakaa rohoni. Na Watanzania wanao wapa kura kwa kuongelea watu nawaonea huruma sana.
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
View attachment 38435 "ukivaa nenda kashushe ile bendera yenye rangi ya damu Igunga is for CCM"... sawa kamanda soko lote hili Igunga tuna ijua CCM tu wengine hawa wananogesha harusi. rudi tarehe 03/10/2011 kuja kumchukua mbunge wa CCM

Duh kumbe ulienda ukatia baraka, ukawaacha vijana wakafanya kazi kisha ukaenda kushangilia ushindi!! Hiyo nayo ni strategy tosha.
 
Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
Mkuu Nnape hapa si ulienda Igunga kutoa pole tu tena kwa mujibu wa vyombo vya habari (gazeti fulani) vilisema ulienda huko bila ridhaa ya wakuu wako na ati Katibu Mkuu alikukemea? Mimi binafsi sikukusikia kwenye kampeni za Igunga. Labda utuambie hapa nini kilikusibu hadi usiende kueneza sera za Chama ukizingatia kuwa hapo ndipo hasa palikuwa pahala pake. Nilitegemea ungeenda kuwaeleza kuwa tumeanza kuvua gamba na kukitakasa Chama chetu upya kwa hiyo chagueni mbunge mpya.

View attachment 38436 wana Igunga msifanye makosa eeeh!!!!
 
Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
Duh kumbe ulienda ukatia baraka, ukawaacha vijana wakafanya kazi kisha ukaenda kushangilia ushindi!! Hiyo nayo ni strategy tosha.

View attachment 38438 MMEPOKEAJE KUJIVUA GAMBA IGUNGA?" Ooooh kamanda subiri tarehe 02/10/2011 kama hawajaondoka bila kuaga wala kulipia geusthouse walizolala>>>>>>>>> hahaaaa teh hahaa
 
Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
tofauti uliyonayo na mzee yusufu makamba ni umri tu vinginevyote mnalingana.ujinga,akili,upumbavu ulopokaji ndo usiseme

Oooooh pole kumbe nawe imekugusa sana eeeh? Pole sana sana!!!! Si makusudi imetokea bahati mbaya si kukusudia wewe bahati mbaya umepitia hapa.....
 
Zing

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
1,767
466
Ungekuwa Nape unajitokeza kujibu thread nyingine zinazohusu CCM kama hivi.............. Sio dhumuni langu kushusha umuhimu wa hii thread ila Inaonyesha viongozi wetu kama Nape hawako serious na wakiamua kuwa serious wanatafuta yale yaliyo mepesi mepesi kwao. Comment TANO tayari na hapa page moja tu wakati kuna maswali kibao. kwenye baadhi ya thread kwangu naona ya msingi zaidi lakini hata commment mbili hakuna.........

Badilikeni viongozi wetu@Nape

  • kwa nini wabuge wa CCM walipo dar hatafuti siku za kukusanyamaoni na ushauri kwatu mbali mbali kama watalaama wa ICT, Uchumi,wahandisi
  • Kwa nini CCM msiweke sheria kuwa kila mmbunge wa CCM natakiwa kutimia japo siku 50 kwa mwaka kuwa jimboni au wilayani kwake
 
Ruhazwe JR

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
3,403
919
Oooooh pole kumbe nawe imekugusa sana eeeh? Pole sana sana!!!! Si makusudi imetokea bahati mbaya si kukusudia wewe bahati mbaya umepitia hapa.....

mtaa wangu mwendawazimu kama wewe ukipita unakimbizwa hodi ya vichaa
 
RMA

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
409
87
Hivi magwanda hamna sera za kuongelea? kila kukicha Nape, Rostam, wamewakaa rohoni. Na Watanzania wanao wapa kura kwa kuongelea watu nawaonea huruma sana.
Kwa hiyo we jini makata, kiroboto mchumamboga unataka kusema nini?
 
moblaze

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
231
27
View attachment 38438 MMEPOKEAJE KUJIVUA GAMBA IGUNGA?" Ooooh kamanda subiri tarehe 02/10/2011 kama hawajaondoka bila kuaga wala kulipia geusthouse walizolala>>>>>>>>> hahaaaa teh hahaa

tutaona mwisho wako! cjawai kukuchukia coz tulikua wote INDIA but ukweli umekosa akili za kufikiria. ukipata tena uongozi zaidi ya huo baada ya mme wako J50 kutoka madarakani sio mm. mbona wewe ni kijana na unajua matatizo yote sema unafunga macho? acha kuwa mwanamke m@£..a! angalia nchi yako sio tumbo! utakua ki2ko ndugu...kip on waiting. sio kila mtu anae kuambia ukweli anashibia kwenye chama. kama kweli mwanaume jitume kutumia BBM yako kama wenzako. HAKUNA GAMBA GUMU KAMA WEWE CCMAGAMBA!
 
Mumwi

JF-Expert Member
Jan 9, 2011
592
122
View attachment 38438 MMEPOKEAJE KUJIVUA GAMBA IGUNGA?" Ooooh kamanda subiri tarehe 02/10/2011 kama hawajaondoka bila kuaga wala kulipia geusthouse walizolala>>>>>>>>> hahaaaa teh hahaa
Tumejua kweli ccm ni wezi wakubwa Wa kura ccm ndiyo mtaleta maafa Tanzania watu wakisha choka kuporwa haki zao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom