Dumelambegu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 1,052
- 257
Ndugu zangu,
Kwanza nianze kwa kuipongeza cdm kwa ushindi mkubwa na munono walioupata Igunga hivi karibuni baada ya kampeni za mwezi mzima. Nauita ushindi kwa sababu kwa upande wa Igunga ni kama vile cdm ilikuwa ndiyo kama inaanza harakati zake za siasa kwani nasikia wakati wa uchaguzi wa mwaka jana hawakuweka hata mgombea wa ngazi ya ubunge.
Hivyo, hatua iliyofikiwa na cdm siyo ya kubeza ikizingatiwa kuwa ilikuwa inapambana na ccm yenyewe, serikali na vyombo vyake vyote na hata cuf. Kinachonipa faraja na kuamini kuwa watanzania sasa wameamka, ni namna wana-Igunga walivyoiunga mkono cdm bila kujali utitiri wa viongozi waandamizi wa ccm waliopo na wasiokuwepo madarakani waliokwenda Igunga kufanta kampeni kama vile mkapa, mangula, magufuli, wasira, n.k
Hakika ukiangalia nguvu halali na isiyo halali (ya kutumia rasilimali za serikali) iliyotumiwa na ccm hutachelewa kuamini kuwa wananchi wameichoka ccm kwani kinachowatofautisha na cdm kiasilimia ni kiasi kidogo hasa ukizingatia rasirimali iliyotumika katika kupata ushindi huo. Kwa mwana-ccm makini kamwe hawezi kushangilia ushindi wa Igunga.
Labda nimalizie kwa kuwatia moyo cdm kwamba ahadi walizotoa ccm kwa wananchi wa Igunga ni kabyri tosha watakalozikwa ifikapo 2015. Kama kawaida yao, mojawapo ya ahadi ni kufikisha maji ya ziwa victoria hadi mjini Igunga. Wananchi wasioelewa walishangilia sana waliposikia ahadi hii lakini ukweli ni kwamba haitekelezi na kama itatekeleza basi siyo leo wala kesho wala keshokutwa.
Ujenzi wa bomba kutoka Kahama hadi Nzega na hatimaye Igunga unahusisha mabilioni ya fedha ambazo ni punguani tu anayeweza kuamini kuwa serikali ya kikwete inaweza kuwa nayo. Mbaya zaidi ni kuwa hovi sasa hata wahisani kwenye sekta ya maji wameanza kujitoa mmoja mmoja. Walianza waholanzi na hivi sasa wajerumani wapo katika hatua za mwisho za kujiondoa.
Kwa mwenendo huu, nina hakika kwamba uchaguzi wa 2015 utafika wakati ambapo hata mchakato tu wa kupeleka maki Igunga haujaanza. Kwa hiyo, Bw. Kashindye na viongozi wengine wa cdm msikate tamaa. Endeleeni na jitihada zenu za kufungua matawi mengi zaidi ya chama na kuwaelimisha wananchi kuhusu uraia na inshallah mwisho wa siku ccm itaangukia pua. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.