Ushindi wa CCM Igunga hauwezi kushangiliwa na mwana-CCM yeyote makini


Dumelambegu

Dumelambegu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
1,052
Likes
15
Points
0
Age
57
Dumelambegu

Dumelambegu

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
1,052 15 0
Ndugu zangu,

Kwanza nianze kwa kuipongeza cdm kwa ushindi mkubwa na munono walioupata Igunga hivi karibuni baada ya kampeni za mwezi mzima. Nauita ushindi kwa sababu kwa upande wa Igunga ni kama vile cdm ilikuwa ndiyo kama inaanza harakati zake za siasa kwani nasikia wakati wa uchaguzi wa mwaka jana hawakuweka hata mgombea wa ngazi ya ubunge.

Hivyo, hatua iliyofikiwa na cdm siyo ya kubeza ikizingatiwa kuwa ilikuwa inapambana na ccm yenyewe, serikali na vyombo vyake vyote na hata cuf. Kinachonipa faraja na kuamini kuwa watanzania sasa wameamka, ni namna wana-Igunga walivyoiunga mkono cdm bila kujali utitiri wa viongozi waandamizi wa ccm waliopo na wasiokuwepo madarakani waliokwenda Igunga kufanta kampeni kama vile mkapa, mangula, magufuli, wasira, n.k

Hakika ukiangalia nguvu halali na isiyo halali (ya kutumia rasilimali za serikali) iliyotumiwa na ccm hutachelewa kuamini kuwa wananchi wameichoka ccm kwani kinachowatofautisha na cdm kiasilimia ni kiasi kidogo hasa ukizingatia rasirimali iliyotumika katika kupata ushindi huo. Kwa mwana-ccm makini kamwe hawezi kushangilia ushindi wa Igunga.

Labda nimalizie kwa kuwatia moyo cdm kwamba ahadi walizotoa ccm kwa wananchi wa Igunga ni kabyri tosha watakalozikwa ifikapo 2015. Kama kawaida yao, mojawapo ya ahadi ni kufikisha maji ya ziwa victoria hadi mjini Igunga. Wananchi wasioelewa walishangilia sana waliposikia ahadi hii lakini ukweli ni kwamba haitekelezi na kama itatekeleza basi siyo leo wala kesho wala keshokutwa.

Ujenzi wa bomba kutoka Kahama hadi Nzega na hatimaye Igunga unahusisha mabilioni ya fedha ambazo ni punguani tu anayeweza kuamini kuwa serikali ya kikwete inaweza kuwa nayo. Mbaya zaidi ni kuwa hovi sasa hata wahisani kwenye sekta ya maji wameanza kujitoa mmoja mmoja. Walianza waholanzi na hivi sasa wajerumani wapo katika hatua za mwisho za kujiondoa.

Kwa mwenendo huu, nina hakika kwamba uchaguzi wa 2015 utafika wakati ambapo hata mchakato tu wa kupeleka maki Igunga haujaanza. Kwa hiyo, Bw. Kashindye na viongozi wengine wa cdm msikate tamaa. Endeleeni na jitihada zenu za kufungua matawi mengi zaidi ya chama na kuwaelimisha wananchi kuhusu uraia na inshallah mwisho wa siku ccm itaangukia pua. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.
 
Tango73

Tango73

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2008
Messages
1,678
Likes
44
Points
135
Tango73

Tango73

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2008
1,678 44 135
Kwa kweli Igunga kunatia haibu sana. Baada ya miaka 50 ya uhuru baadhi ya wananchi wa Igunga bado hawajui kuosma na kuandika! Hawana vyoo vya kisasa wala nyumba za matofari ya kuchoma! Maji wanatafuta maili mia moja na yakifika nyumbani hayamwagwi hata kama yananawiwa mara kumi!CCM imetawala Igunga miaka 50 tangia tupate Uhuru, inaweza kujivunia nini kuhusu utawla wake hapo Igunga?

Ina maana CCM haikuona maisha duni haya ya wana Igunga tangia miaka yote ya uhuru? Gharama za kampeni na mikwara ya helopta kuruka Igunga angani, zingetumika kuwaletea maji na kujenga maktaba na shule za secondari za kutosha. Hospitali zingejazwa na madawa na wakulima hao wa igunga wangekuwa na nafuu. Halafu watu

sizani hata kama kuna magazeti ya Daily news, the citizens na News week yanafika huko Igunga. Bali vitu viwafikiavyo wananchi wa huko ni nyimbo za chama na hotuba za makada tuu. Poleni wana Igunga!

Lazima mushukuru marekani kuutokomeza ukomunisti na tanzania kuachana na siasa za ujamaa na kujitegemea. maendeleo yatawafikia tuu wana Igunga.
 
Mzee

Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Messages
13,426
Likes
3,481
Points
280
Mzee

Mzee

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2011
13,426 3,481 280
Ya Igunga yamepita.
 
Gosbertgoodluck

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
2,865
Likes
32
Points
0
Gosbertgoodluck

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
2,865 32 0
Wanaoshangilia ni mukama na nape tu ambao walikuwa kwenye wakati mgumu kutokana na upya wao katika nafasi walizonazo sasa kwenye chama.
 
twahil

twahil

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Messages
3,635
Likes
2,012
Points
280
Age
32
twahil

twahil

JF-Expert Member
Joined May 31, 2011
3,635 2,012 280
Suala hapa CCM ilishinda uchaguzi na inapaswa kujipongeza.kama kulikua na mapungufu hayo CCM imeishaanza kuyafanyia kazi ktk vikao vya ndani.CCM si wajinga kiasi hicho na ndio maana wanawadunda kila kukicha hadi 2090 kwasababu mkidundwa mnatafuta visingizio vya kitoto.
 
Chakunyuma

Chakunyuma

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Messages
811
Likes
3
Points
35
Chakunyuma

Chakunyuma

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2011
811 3 35
Ni kweli kabisa kwamba ahadi zisizotekelezeka ndio zitakazowaondoa.
 
K

KUNYWA

Member
Joined
Sep 30, 2011
Messages
32
Likes
0
Points
0
K

KUNYWA

Member
Joined Sep 30, 2011
32 0 0
Ushindi ni ushindi tuu hata kama ni wa matuta.Waloshinda wameshinda,na waloshindwa wameshindwa.Yalobaki,tugange yajayo.
 
Josephine

Josephine

Verified Member
Joined
Sep 5, 2010
Messages
786
Likes
5
Points
0
Josephine

Josephine

Verified Member
Joined Sep 5, 2010
786 5 0
Ushindi ni ushindi tuu hata kama ni wa matuta.Waloshinda wameshinda,na waloshindwa wameshindwa.Yalobaki,tugange yajayo.
Mmmmmmmmmmmmmmmmmmmm,kazi kwelikweli.haya bwana
 
Jembe Ulaya

Jembe Ulaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2008
Messages
456
Likes
1
Points
0
Jembe Ulaya

Jembe Ulaya

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2008
456 1 0
CCM walichofuata Igunga ni ushindi "kwa namna yoyote ile". Aliyasema Mkapa mwenyewe mkapa kwa mdomo wake siku ya uzinduzi wa kampeni zao. Mwanaccm yoyote makini alitakiwa ajitahidi awaletee ushindi. Sasa ushindi wameupata asiyesheherekea yeye sio wanaccm makini.

CCM wame prove kwamba wako juu ya sheria. Wanafanya madhambi wao lakini chadema ndio wanafunguliwa kesi. Leo mjini Tabora mahakamani yuko Mhe Kasulumbayi na Mhe Kiwanga wana kesi zinazowakabili. Kwanini wasisheherekee?

CCM wanatoa ahadi kwenye majukwaa kwasababu hawana cha kuongea. Ukiacha fitina na propaganda kwamba chadema ni chama cha fujo wahana la kuwaambia wananchi. Wanaambia kwamba wao tu ndio wanaweza kutekeleza mambo kwa kuwa wana serikali. Wananchi wanakubali. Kwanini wasisheherekee?

Leo Rostam kupitia Dowans analipwa kwa kufinance helikopta uchaguzi wa Igunga. Wamejazwa mahela mfukoni na wameondoka na ushindi. Kwanini wasisheherekee??
 
CR wa PROB

CR wa PROB

Senior Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
170
Likes
1
Points
0
Age
98
CR wa PROB

CR wa PROB

Senior Member
Joined Sep 21, 2011
170 1 0
CCM wanao uwezo wa kutekeleza ahadi zote kwa wana Igunga endapo watatumia zile Pesa za DOWANS, Hivyo basi kwa kuwa wao ndio walioshika dola ni vyema hizi pesa za DOWANS wazipeleke igunga kama vile walivyopeleka ile TAKRIMA ya kugawa Sukari kipindi cha kampeni ili wapewe kura!!! Nje ya hapo wajiandae kuaga Igunga kwenye uchaguzi ujao.
 

Forum statistics

Threads 1,235,517
Members 474,633
Posts 29,225,483