Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,392
- 39,493
Saa na wakati huu vikosi vya majeshi ya Jumuiya ya Afrika vimeanza mapambano ya kukikomboa kisiwa cha Anjouan ili hatimaye kurudi katika shirikisho la Comoro. Vikosi hivyo vikiongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania wanashiriki katika Operesheni Demokrasia Komoro yenye lengo la kumuondoa Rais aliyejipachika Bw. Mohammed Bacar.
Hivyo saa na wakati kama huu ambapo vijana wetu wako katika hali ya hatari na ambapo wanayaweka maisha yao hatarini ni kitendo cha kutokuwajibika kwa mwanasiasa kama Wangwe kudai kuwa Rais amevunja Katiba wakati kipengele alichokinukuu hakihusiki na mapigano haya. Kitendo cha kutumia mapigano hayo kujipatia pointi za kisiasa nakipinga na kinaonesha ni jinsi gani Bw. Wangwe siyo tu hajui Katiba lakini wakati wanajeshi wetu wako kwenye mapigano yeye anaongoza jitihada za kuwavunja moyo.
Kama raia wa Tanzania naomba nitumie nafasi hii kutuma salamu za ushindi kwa Jeshi la Wananchi, kwa Amiri Jeshi Mkuu na kwa makamanda na wapiganaji wote huko Comoro ili hatimaye wafanye kazi tuliyowatuma kwa haraka, ufanisi na kuhakikisha kuwa maisha ya raia yanalindwa kwa kiasi chote kinachowezekana.
Saa na wakati kama huu, hakuna Chadema, CUF, CCM au SAUT Tanzania ni moja na hatima yake ni moja, na ni jukumu la kila raia kusimama na kutakia ushindi vikosi vyetu na haya mambo ya kulalamika yaje baadaye siyo wakati risasi zinarushwa.
Kwa jeshi letu, USHINDI NI LAZIMA!
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika.
NB: Kwa matangazo yangu ya leo nikichambua hoja dhaifu za Mhe. Wangwe kama zilivyosikika BBC tafadhali tembelea http://www.klhnews.com na usisahau kutumia search injini yetu pale.