Ushindi mwingine kwa Iran na Hamas baada ya Netanyahu kupigwa chini

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,996
2,000
Zarif: Netanyahu naye pia ametupwa katika jaa la taka za historia; Iran inasimama kwa heshima

Jun 04, 2021 08:11 UTC

[https://media]

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif ameashiria mchakato wa kuondolewa Benjamin Netanyahu katika nafasi ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema, Netanyahu pia ametupwa katika jaa la taka za historia.

Katika ujumbe alioutuma Alhamisi katika ukurasa wake wa Twitter, Zarif ameashiria kufika ukingoni utawala wa Netanyahu na pia akamtaja rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na maafisa wake wawili waliokuwa na misimamo ya kufurutu ada dhidi ya Iran ambao ni aliyekuwa mshauri wake wa usalama wa taifa John Bolton na aliyekuwa waziri wake wa mambo ya nje Mike Pompeo na kusema watatu hao walikuwa washirika wa Netanyahu katika misimamo yake dhidi ya Iran.

Zarif ameandika katika ukurasa huo wa Twitter kuwa: "Netanyahu amejiunga na wenzake waliuokuwa na misimamo mikali dhidi ya Iran yaani Bolton, Trump na Pompeo katika safari ya kuelekea katika jaa la taka za historia. Iran nayo inabaki ikiwa imesimama kidete na kwa heshima. Hii ndio hatima ya wale wote waliokuwa wakitaka kuidhuru Iran."

[https://media]Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif

Jumatano ilikuwa siku ya mwisho ambayo Benjamin Netanyahu alikuwa amepewa na rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuunda serikali na baada ya kushindwa kufanya hivyo sasa muungano mpya unatazamiwa kuundwa na wanasiasa wengine katika utawala huo.

Kuondolewa Netanyahu madarakani ni miongoni mwa mafanikio ya operesheni ya "Panga la Quds"

Jun 05, 2021 02:31 UTC

[https://media]

Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imetangaza kuwa moja kati ya matunda ya opesheni ya "Panga la Quds" ni kuondolewa madarakani Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Ahmad al Mudallal ambaye ni miongoni mwa viongozi wa ngazi ya juu wa harakati ya Jihad Islami amesema kuwa, Netanyahu alitumia nguvu zote za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza lakini mwishowe jeshi la utawala huo halikuweza kuingia katika eneo hilo.

Al Mudallal amesema kuwa, yaliyomtokea Netanyahu baada ya vita vya Panga la Quds yamewatokea na yatawatokea viongozi wengine wa utawala wa kigaidi wa Israel na kuongeza kuwa, kubadilishwa kwa mabaraza ya mawaziri huko Israel hakuna maana na kubadilika kwa mtazamo wa utawala huo kuhusianana na wanamapambano wa Palestina.

Wakati huo huo Dimitri Diliani ambaye ni mjumbe wa harakati ya Fat'h ya Palestina amesema kuwa mabadiliko ya baraza la mawaziri ya utawala wa kibaguzi wa Israel hayana maana yoyote kwa Wapalestina na kwamba utawala huo utaendelea kufanya uhalifu na jinai kwa raia wasio na hatia.

Jumatano iliyopita Yair Lapid kiongozi wa chama cha upinzani cha Yesh Atid, alimtaarifu Rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Reuven Rivlin kwamba yuko tayari kuunda serikali mpya baada ya aliyekuwa waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda baraza jipya la mawaziri.

4bv690c81129851lbyi_800C450.jpeg
 
Ausar

JF-Expert Member
Mar 19, 2021
308
500
Ule uvamizi jamaa alicheza karata mbovu ikamuharibia zaidi kwa wananchi
 
Simba Forever

JF-Expert Member
May 4, 2021
856
1,000
Aliechaguliwa kushika hiyo nafasi anasema anajisikia furaha sana kuwaua waarabu na haoni aibu kufanya hivyo

Swali: Je, Iran Inatupa mkeka kwa msala upitao?

Unafurahia kuondoka kwa Adui yako wakati anaeingia ni Ndugu wa Damu wa huyo Gaidi?
 
permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
6,020
2,000
Zarif: Netanyahu naye pia ametupwa katika jaa la taka za historia; Iran inasimama kwa heshima

Jun 04, 2021 08:11 UTC

[https://media]

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif ameashiria mchakato wa kuondolewa Benjamin Netanyahu katika nafasi ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema, Netanyahu pia ametupwa katika jaa la taka za historia.

Katika ujumbe alioutuma Alhamisi katika ukurasa wake wa Twitter, Zarif ameashiria kufika ukingoni utawala wa Netanyahu na pia akamtaja rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na maafisa wake wawili waliokuwa na misimamo ya kufurutu ada dhidi ya Iran ambao ni aliyekuwa mshauri wake wa usalama wa taifa John Bolton na aliyekuwa waziri wake wa mambo ya nje Mike Pompeo na kusema watatu hao walikuwa washirika wa Netanyahu katika misimamo yake dhidi ya Iran.

Zarif ameandika katika ukurasa huo wa Twitter kuwa: "Netanyahu amejiunga na wenzake waliuokuwa na misimamo mikali dhidi ya Iran yaani Bolton, Trump na Pompeo katika safari ya kuelekea katika jaa la taka za historia. Iran nayo inabaki ikiwa imesimama kidete na kwa heshima. Hii ndio hatima ya wale wote waliokuwa wakitaka kuidhuru Iran."

[https://media]Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif

Jumatano ilikuwa siku ya mwisho ambayo Benjamin Netanyahu alikuwa amepewa na rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuunda serikali na baada ya kushindwa kufanya hivyo sasa muungano mpya unatazamiwa kuundwa na wanasiasa wengine katika utawala huo.

Kuondolewa Netanyahu madarakani ni miongoni mwa mafanikio ya operesheni ya "Panga la Quds"

Jun 05, 2021 02:31 UTC

[https://media]

Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imetangaza kuwa moja kati ya matunda ya opesheni ya "Panga la Quds" ni kuondolewa madarakani Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Ahmad al Mudallal ambaye ni miongoni mwa viongozi wa ngazi ya juu wa harakati ya Jihad Islami amesema kuwa, Netanyahu alitumia nguvu zote za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza lakini mwishowe jeshi la utawala huo halikuweza kuingia katika eneo hilo.

Al Mudallal amesema kuwa, yaliyomtokea Netanyahu baada ya vita vya Panga la Quds yamewatokea na yatawatokea viongozi wengine wa utawala wa kigaidi wa Israel na kuongeza kuwa, kubadilishwa kwa mabaraza ya mawaziri huko Israel hakuna maana na kubadilika kwa mtazamo wa utawala huo kuhusianana na wanamapambano wa Palestina.

Wakati huo huo Dimitri Diliani ambaye ni mjumbe wa harakati ya Fat'h ya Palestina amesema kuwa mabadiliko ya baraza la mawaziri ya utawala wa kibaguzi wa Israel hayana maana yoyote kwa Wapalestina na kwamba utawala huo utaendelea kufanya uhalifu na jinai kwa raia wasio na hatia.

Jumatano iliyopita Yair Lapid kiongozi wa chama cha upinzani cha Yesh Atid, alimtaarifu Rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Reuven Rivlin kwamba yuko tayari kuunda serikali mpya baada ya aliyekuwa waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda baraza jipya la mawaziri.

View attachment 1809186
Jawad anapaswa aungane na "Mkojani " ili vichekesho vinoge vizuri.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Ausar

JF-Expert Member
Mar 19, 2021
308
500
Unajua uchaguzi wa Israel ulifanyika lini?hadi uuhusishe na huu uvamizi wa juzi tu?au umekurupuka tu, una jua ni muda gani wamekuwa wanavutana kuunda serikali kutokana na kutokuwa na mshindi wa moja kwa moja?
Uchaguzi umetoka wapi hapo?Naongelea ishu ya sasa na nimesema imekuharibia zaidi kumaanisha tayari palishakua na hali ngumu.......rudi kwenye hilo pango ulilotoka ujielewe zaidi
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,921
2,000
Uchaguzi umetoka wapi hapo?Naongelea ishu ya sasa na nimesema imekuharibia zaidi kumaanisha tayari palishakua na hali ngumu.......rudi kwenye hilo pango ulilotoka ujielewe zaidi
Eti ule uvamizi umemuharibia kwa wananchi!!???ki vipi kwani kuna uhusiano wowote na kushindwa kwake kuunda serikali?!bado hujaeleweka,
 
Semahengere

JF-Expert Member
Nov 29, 2020
427
1,000
Amekuja Naftali Bennett kama mlitegemea ahueni huyu ndio mbaya kuliko Netanyahu.
Atawachinja hawa warusha mawe kama Kuku
 
Tango73

JF-Expert Member
Dec 14, 2008
1,753
2,000
unaikumbuka Entebe raid? Menahem alivyo muunga mkono Rabin na kuonesha lao lilikuwa moja. Unakumbuka alipoingia madarakani Menahem begin alikuwa mkali kuliko Rabin. Alimfukuza Arafat Lebanon, na kuuangamiza mtambo wa nukes wa sadam. Naftali benet siku zote anlalamika kuwa badala ya kumpiga Hamas akirusha maroketi lazima kwanza apigwe Iran.hapo watupa mawe hawana nafuu kila mmoja kitumbo joto,.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom