Ushindi lazima, Wapinzani Tuwachanechane Tuwatupe

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
430
Mwenendo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) hasa katika kuhaha kurejesha baadhi ya halmashauri za miji, manispaa na majiji ambayo hayako chini yake kwa kutumia mbinu chafu na hata kuhonga viongozi wa upinzani unatia mashaka na kuleta giza juu ya hatma ya Siasa za ushindani na amani yetu.

CCM inaongoza karibu halmashauri zote nchini lakini haiko tayari kuona halmashauri hata moja ikiongozwa na chama cha upinzani. Hili limejionesha wazi katika migogoro inayoendelea ya kiuongoziJijini Arusha, Mwanza, Manispaa ya Moshi na chokochoko za mara kwa mara za kiuongozi katika Manispaa ya Musoma Mjini iliyo chini ya CDM.

CCM kwa kutumia mbinu chafu na umafia imekuwa ikizalisha migogoro karibu katika halmashauri, manispaa na majiji yote yanayongozwa na upinzani. Hili halihitaji utafiti liko wazi.

Tafsiri yake ni moja tu kwamba, CCM hakiko tayari kuongozwa. Kina amini kina hakimiliki ya kutawala milele na hakuna chama kingine kinachopaswa kwa vyvoyote kuongoza hata halmashauri moja. Upinzani kuongoza ni mkosi, ni laana kwa CCM, haikubaliki na haipo.

Hii ndiyo imezaa kaulimbiu kama za ‘Ushindi ni lazima, Wapinzani Tuwachanechane tuwatupe' na zingine nyingi ambazo ama kwa hakika zinatoa jibu lilelile kuwa mpinzani ni adui, hapaswi kuongoza wala kushinda uchaguzi wowote.

Athari za mentality hizi za CCM ingawa zimeanza kujitokeza katika maeneo fulanifulani kama ilivyojitokeza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na baadaye vurugu zilizofuata kwenye chaguzi za umeya Arusha na Mwanza hakika hazitaliacha taifa salama katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Mvutano sasa si kati ya CDM na CCM kwenye nafasi za Umeya, Uenyekiti wa halmshauri nk. Nk. Bali ni kati ya umma usio na fedha lakini unataka mabadiliko kwa kasi sana na CCM iliyochoka, yenye fedha na dola hivyo kutmia fursa hiyo kuziba mwanya pekee wa kuleta mabadiliko yaani Uchaguzi huru na wa haki. Hakika njia hii kuu iliyozibwa na CCM ndiyo maafa yetu.
 
wana hesabu siku ndugu yangu isikutie shaka hata kidogo hii nchi tutachukua 2015 cha msingi niku waelimisha wananchi wazijue haki zao hakika tutafika
 
Back
Top Bottom