Ushindi dhidi ya Yanga umefuta matatizo yote Msimbazi

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,840
2,000
Hizi ni kauli za wanachama wa simba kabla ya mechi ya mtani jembe na Yanga.
''mara baada ya mechi na yanga tukishinda au tukifungwa tutaenda nyumbani kwa Rage atuonyeshe fedha za Okwi ziko wap na hatuondoki mpaka ajiuzulu'' mwingine akasema'' tunataka tujue pia pesa za mauzo ya samata, ochan na kazimoto zimetumika vipi maana ziliingia kwenye account ya mwanamke fulani'' n wengine wakathubutu kwenda hadi Bungeni kwa Mh. Spika. Lakini pia bado kukawa na mvutano kati ya mwenyekiti na kamati ya utendaji.
Lakini baada ya mechi ya mtani jembe na Simba kushinda goli 3 kwa 1 , matatizo yote ya wanasimba yamefutika na yale yote waliodhamilia yamepatiwa ufumbuzi hali sasa ni shwari kabisa gogolo hakuna tena, kweli simba na yanga ni zaidi uzijuavyo, mafanikio makubwa kabisa katika timu hizi ni mmoja kumfunga mwenzake hata kama mechi isiyo ya kimashindano.
Mpira wa Tanzania kukua itabaki kuwa ndoto isiyotimia kama Simba kumfunga Yanga au Yanga kumfunga Simba ni zaidi ya kuwa na matumizi bora ya fedha, uadilifu, kuwa na viwanja bora vya timu na timu kujitegemea.
Maana 3 kwa 1 imelipa fedha za okwi, Rage amegeuka kuwa kiongozi bora, mpira pesa na Rage wanakula sahani na wote wameshiba na kuridhika.
Simba na Yanga zinaingia katika maajabu ya Dunia na sasa tuna maajabu 8 ya dunia.
 

Uledi

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
583
500
Mkuu unachosema ni kweli hivi vilabu vimekuwa kama vya walevi. Havielewiki vipo kwa ajili ya malengo yapi maana wao mmoja akimfunga mwenzie ndio kamaliza kila kitu.


Aliyetuanzishia hivi vilabu ametuachia mtihani mkubwa wapenda soka wa Tanzania.
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
8,269
2,000
swalala rage kutimuliwa lipo palepale na rage hakuchangia chochote kuhusiana na matokeo ya mtani jembe kama unakumbuka rage alipinga kutimuliwa kina kibadeni na akasema hamtambui kocha mpya lakini kamati ya utendaji iliamua kushikilia msimamo wake ndio maana ulimuona Kaburu yuko karibu na timu na hata check alienda kupokea mzee wa kinesi na hata pale matawi yalipokutana rage aliwatuma polisi walipofika wakamweleza wao wako kwenye vikao kujadili mechi yao dhidi ya yanga lakini baadae wakatoka na tamko la kumtaka aitishe mkutano kwa kifupi siku zake zimefika mwisho hana pesa,ni mwizi wa pesa ingawa yote yalikuwa yanajulikana kabla ya kuchaguliwa na sasa timu haiko mikononi mwake kwani kuanzia viongozi wenzake,wanachama mpaka wachezaji hawamtaki
 

Masuke

JF-Expert Member
Feb 28, 2008
4,613
1,250
Mkuu Rage kuondoka ni suala ambalo halijafutwa na ushindi dhidi ya watani, kwa sasa unaona ni kama limefifia kwa sababu kuu mbili; moja ni kwamba TFF wameingilia kati baada ya kamati ya utendaji kutangaza kwamba Rage ameondoka na hali ilivyo ni kama vile tu ameshaondoka au ni mwenyekiti asiyekuwa na madaraka kwa sababu kila anachosema kwenye timu hakifuatwi, alitangaza kuwarudisha Kibadeni na Julio, nadhani wewe mwenyewe ni shahidi kwamba Julio na Kibadeni hawako na timu.
Baada ya Rage kuwagomea kamati ya utendaji ya TFF kwamba hawezi kuitisha mkutano wa wanachama wote kama alivyoagizwa na badala yake akaomba warejee maamuzi yao, TFF waliamua kupeleka suala hilo katika kamati husika, tusubiri tuone kamati itaamuaje.

Mbili ni kwamba wanachama walivyotangaza kwamba wataenda nyumbani kwa Rage baada ya mechi na Yanga, Rage alitoa taarifa polisi na polisi wakachimba mkwara, wewe unafikiri nani anapenda kuvunjwa miguu mwisho huu wa mwaka?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom