Ushindani wa vigogo wawili - Mwandosya 2 Lowasa 0

Mwafrika

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,490
226
Kwa utaratiiiiiibu kama kumsukuma mlevi mteremkoni vile, Mwandosya anazidi kumpiga fimbo ya kisiasa kigogo wa wanamtandao Lowasa. Katika kipindi kisichozidi miezi sita ya ugomvi na ushindani mkubwa, Mwandosya ameibuka kidedea kwa kumshinda Lowasa kwenye kampeni za uchaguzi wa NEC na kwenye issue ya Mwakyembe.

Inavyooneka Lowasa ameshindwa kabisa kupambana na huyu kigogo wa nyanda za juu kusini kwa vile alivyoshindwa kumtoa kwenye NEC na hivyo kuacha hai ndoto za Mwandosya kugombea urais 2010 au 2015.

Katika hatua inayoonekana kama uchezaji wa hali ya juu kama wa Michael Jordan, Mwandosya ametumia nguvu ya mpiga kampeni wake maarufu wa kugombea urais mwaka 2005 (Dr Mwakyembe) kumgalagaza kabisa Lowasa katika kinyanganyiro hiki cha pili ambacho kimepelekea kabisa Lowasa kuutema uwaziri mkuu na kuzima ndoto za Lowasa kuwa raisi wa Tanzania.

Kwaheri Lowasa......... na Mwandosya jiandae kwa round ya pili ambayo sasa ni kati yako na Bingwa wa kampeni chafu dhidi ya wanaccm - Membe.

Inauma lakini wale wapiga kampeni wa Lowasa hapa sijui kama wako hai au wamepata magonjwa ya moyo, mchambuzi upooooo?!
 
Lowasa bado atapigwa fimbo right and left mpaka alie kimasai..

kichghweeeeee .... horrrrrooooiiiiii
 
Kindly clarify, this was posted last year 2008, Februry, is kind of riddle to me!
 
Wandugu, kuuliza si ujinga. Jina la Mwandosya linasikika sana kama mmoja wa marais wetu wa baadaye.. Mimi sijawahi kuona wasifa wake kwa nini awe Rais, je ni mchapa kazi sana? alimaliza tatizo la umeme?alisaidia DAWASA kumaliza tatizo la maji na kuongeza mapato ya DAWASA? Alimaliza matatizo ya wakulima na wafugaji? Amefanya nini katika vita dhidi ya mafisadi? wizara zake alizoongoza zina ufanisi wa namna gani?Hayo niliyoyataja ni mifano midogo sana, lakini naomba kuelimishwa ili nami nisipoteze kura yangu kwa kuchagua mtu mwingine, lets say Magufuli au Lowasa, au yeyote yule atakayegombea.
 
Tusidanganyike jameni, hakuna anayefaa hapo kwani mtoto wa nyoka ni nyoka tu sio kenge, wote ccm tu hao, to hell.
 
Mwafrika nadhani unapima upepo!!!!Asha Rose nae watapambana nae kwani inasemekana ndio chaguo la muungwana.
 
Wandugu, kuuliza si ujinga. Jina la Mwandosya linasikika sana kama mmoja wa marais wetu wa baadaye.. Mimi sijawahi kuona wasifa wake kwa nini awe Rais, je ni mchapa kazi sana? alimaliza tatizo la umeme?alisaidia DAWASA kumaliza tatizo la maji na kuongeza mapato ya DAWASA? Alimaliza matatizo ya wakulima na wafugaji? Amefanya nini katika vita dhidi ya mafisadi? wizara zake alizoongoza zina ufanisi wa namna gani?Hayo niliyoyataja ni mifano midogo sana, lakini naomba kuelimishwa ili nami nisipoteze kura yangu kwa kuchagua mtu mwingine, lets say Magufuli au Lowasa, au yeyote yule atakayegombea.

Understand, hamna mtu pelekwa chuo kikuu kusomea shahada ya kuwa rais, kuwa kiongozi ni kipaji ikiwemo na mambo mengine ambayo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaorodhesha kama mambo ya msingi ya mtu kuwa rais wa Tanzania. Prof. Mwandosya is an attractive candidate for the presidency na huu hapa ni wasifu wake:

1010.jpg

First Name: Prof. Mark
Middle Name: James
Last Name: Mwandosya
Member Type: Constituency Member
Constituent: Rungwe Mashariki
Political Party: CHAMA CHA MAPINDUZI
Office Location: P.O. Box 9120, Dar es Salaam
Office Phone: +255 784 602596
Ext.: Office Fax: +255 22 2112751
Office E-mail: mmwandosya@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Start Date: 28 December 2005
End Date:27 December 2010
Date of Birth 28 December 1949

Education:

University of Birmingham - UK PhD (Electrical& Electronic Eng.)
1974 - 1977 PHD Aston University - UKBSc. (Engineering)Hons.
1971 - 1974 GRADUATE Dar es Salaam Technical College
A-Level Education 1969 - 1970 HIGH SCHOOL Malangali Secondary School
O-Level Education 1965 - 1968 SECONDARY Majengo Primary School
1957 - 1958 PRIMARY White Fathers Chunya Primary School
1959 - 1960 PRIMARY Chunya Middle School Primary Education
1961 - 1964 PRIMARY

Experience:

- Vice-President's Office (Environment) Minister 2006
- 2/8/2008 Ministry of Communication and Transport
- Minister 2000 - 2005
- Ministry of Water and Irrigation Minister 2/13/2008
- University of Dar es Salaam Professor 1994 - 2000
- Ministry of Industries and Trade Principle Secretary 1992 - 1993
- Ministry of Water, Energy and Minerals Principle Secretary 1990 - 1992
- Ministry of Water, Energy and Minerals Commissioner 1985 -1990
- University of Dar es Salaam Associate Professor 1983 - 1987
- University of Dar es Salaam Senior Lecturer 1980 - 1983
- University of Dar es Salaam Lecturer 1977 - 1980

Ministry/Political Party/Location Position:

Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of the National Executive Committee 2002 -Todate
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of Parliament of Tanzania 2000 - Todate
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member - Political Committee(Regional& District)2000 - 2005
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member 1977 - Todate
TANU Member 1971 - 1977
TANU Youth Leader 1967 - 1968

Source: Parliament of Tanzania website
 
Last edited:

Asante mkuu, Experience nimeiona.Lakini nilikuwa ninajua kuwa aliwahi kushika nafasi zote hizo. Lakini sijajua bado alifanya nini huko kizuri mpaka tuseme anafaa kuwa Rais. Kwa maneno mengine kwa nini nimpigie kura yeye? Kama ni experience hata Lowassa anayo, tena ya kumshinda Mwandosya, kwa sababu yeye alishakuwa waziri mkuu, kama ni experience hata Chenge anayo, hata Kusila anayo. Nataka kujua job perfomance yake. Rais wa sasa tuliambiwa ni chaguo la mungu, watu hawajawahi kuhoji utendaji wake wa kazi wakati akiwa waziri. Matokeo yake sasa hivi watu wanamuita msanii.
Kwa mfano wakati Mwandosya ni waziri wa maji na umwagiliaji, je ni hekta ngapi za kilimo cha umwagiliaji ziliongezeka? Wakati yupo wizara ya nishati na madini je aliingia mikataba yoyote ya kifisadi?
 
Tusidanganyike jameni, hakuna anayefaa hapo kwani mtoto wa nyoka ni nyoka tu sio kenge, wote ccm tu hao, to hell.

Yeba wewe umeukata mzizi wa fitna. Wote hawa ni CCM, na CCM = Mafioso.
 
Last edited:
ukilinganisha hawa wawili ni bora lowasa bwana,angalau tunaweza kusema alifanya hili na lile,huyu mark sijawahi kusikia rekodi yake ya utendaji wa kuridhisha zaidi ya hiyo cv yake kuonesha kuwa amekuwa kwenye chama tokea enzi za youth league,na labda tu niliwahi kusikia wakati anajiandaa kugombea ubunge aliwahi kumwaga misaada ya kompyuta na na satelaiti dishi kwenye shule moja huko jimboni kwakwe[nadhani mwakaleli]vinginevyo labda achaguliwe kwa vigezo kama vya huyu muungwana.
 
swali rahisi, lowasa kafanya nini???????
 
alidiriki kuwafukuza wale wezi wa city water,
alidiriki kuwakoromea misri kuhusu matumizi ya maji ya ziwa viktoria,
alikuwa na maamuzi ya kijasiri na utayari wa kuyasimamia,
sio mnafiki,ukiharibu anakupa live na ikibidi kusimamisha ajira yako kama unakwaza utekelezaji wa ilani ya chama, hayo ni kwa uchache tu,
 
Kama sikosei CV ya Mwandosya inapaswa kuwa na University of Nairobi alikosomea digirii ya kwanza
 
Semilong;

Ni chuki au? pamoja na mabaya yake bado unauliza Lowassa kafanya nini?. Hivi wewe ni "mla vumbi" au?. Hilo swali linatakiwa liulizwe na "wabeba mabox" tu. LOL
 
Kwa utaratiiiiiibu kama kumsukuma mlevi mteremkoni vile, Mwandosya anazidi kumpiga fimbo ya kisiasa kigogo wa wanamtandao Lowasa. Katika kipindi kisichozidi miezi sita ya ugomvi na ushindani mkubwa, Mwandosya ameibuka kidedea kwa kumshinda Lowasa kwenye kampeni za uchaguzi wa NEC na kwenye issue ya Mwakyembe.

Inavyooneka Lowasa ameshindwa kabisa kupambana na huyu kigogo wa nyanda za juu kusini kwa vile alivyoshindwa kumtoa kwenye NEC na hivyo kuacha hai ndoto za Mwandosya kugombea urais 2010 au 2015.

Katika hatua inayoonekana kama uchezaji wa hali ya juu kama wa Michael Jordan, Mwandosya ametumia nguvu ya mpiga kampeni wake maarufu wa kugombea urais mwaka 2005 (Dr Mwakyembe) kumgalagaza kabisa Lowasa katika kinyanganyiro hiki cha pili ambacho kimepelekea kabisa Lowasa kuutema uwaziri mkuu na kuzima ndoto za Lowasa kuwa raisi wa Tanzania.

Kwaheri Lowasa......... na Mwandosya jiandae kwa round ya pili ambayo sasa ni kati yako na Bingwa wa kampeni chafu dhidi ya wanaccm - Membe.

Inauma lakini wale wapiga kampeni wa Lowasa hapa sijui kama wako hai au wamepata magonjwa ya moyo, mchambuzi upooooo?!

Ndugu Mwafrika:

Mbona unaichukulia siasa very lightly. Kwanza sikuelewa kile ulichoandika hapa. Pili hakuna point yoyote uliyotoa ya kuonyesha kuwa Mwandosya ameshinda kwa kutumia CV yake au performance zake za kazi. Tatu unaingiza Nyanda za juu. Kwanini usiseme tu Mbeya. Nne utatumia ushabiki wa mpira (Simba na Yanga) kuelezea masuala ya kisiasa. Nafasi za watu hawa ni kubwa kitaifa.
 
Lowassa mchapa kazi mzuri ila ni jambazi, hana nafasi tena ya kuwa rais. Mwandosya ana utendaji mzuri sana kwenye jimbo lake ila kwenye nafasi ya uwaziri utendaji wake hakuna. Amejiangusha mwenyewe kwa kushindwa kuonyesha uchapa kazi wake kwenye nafasi za uwaziri alizowahi kushika.

Membe ni bomu lingine tupilia mbali kabisa. Tutafute mgombea mwingine, ikiwezekana awe mwanamke.

Mziwanda, huyo Mwafrika ni mtu wa Kyela, umepatia kweli kweli. Anaongoza kwa kuwa na majina mengi hapa JF; mwombe Sikonge akutajie. Jamani msije mkanifungia bure!
 
Iliwahi kuandikwa kwenye vyombo vya habari kwa Mwandosya aliwahi kumsomesha mtoto wake au wa ndugu yake nje ya nchi kwa gharama za moja ya mashirika yaliyokuwa chini ya wizara yake ( Mawasiliano na uchukuzi) ikiwa kama ahsante yake kwa msaada haramu aliyowasaidia. Hii kama ilikuwa ni kweli basi hafai kabisaaaaa kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Kumbukeni pia huyu ni miongoni mwa wale waliyofanikisha kununuliwa kwa ndege ya rais isiyotumika kwa kuisifia sana ubora wake.
 
Back
Top Bottom