Kwa utaratiiiiiibu kama kumsukuma mlevi mteremkoni vile, Mwandosya anazidi kumpiga fimbo ya kisiasa kigogo wa wanamtandao Lowasa. Katika kipindi kisichozidi miezi sita ya ugomvi na ushindani mkubwa, Mwandosya ameibuka kidedea kwa kumshinda Lowasa kwenye kampeni za uchaguzi wa NEC na kwenye issue ya Mwakyembe.
Inavyooneka Lowasa ameshindwa kabisa kupambana na huyu kigogo wa nyanda za juu kusini kwa vile alivyoshindwa kumtoa kwenye NEC na hivyo kuacha hai ndoto za Mwandosya kugombea urais 2010 au 2015.
Katika hatua inayoonekana kama uchezaji wa hali ya juu kama wa Michael Jordan, Mwandosya ametumia nguvu ya mpiga kampeni wake maarufu wa kugombea urais mwaka 2005 (Dr Mwakyembe) kumgalagaza kabisa Lowasa katika kinyanganyiro hiki cha pili ambacho kimepelekea kabisa Lowasa kuutema uwaziri mkuu na kuzima ndoto za Lowasa kuwa raisi wa Tanzania.
Kwaheri Lowasa......... na Mwandosya jiandae kwa round ya pili ambayo sasa ni kati yako na Bingwa wa kampeni chafu dhidi ya wanaccm - Membe.
Inauma lakini wale wapiga kampeni wa Lowasa hapa sijui kama wako hai au wamepata magonjwa ya moyo, mchambuzi upooooo?!