Ushimen: Ebu ngoja leo niwape mawazo machache ya kujikwamua

Ni taasisi gani za kifedha zinaweza kukopesha ila kwa collateral ambayo inahimilika kwa kijana ambaye yupo mtaani bila kua na mali kama ardhi, nyumba, shamba, gari n.k.
Sijui lolote kuhusu mikopo mkuu. Hii iwe kwa taasisi yeyote ya kifedha ama hata benki yeyote
 
Mkuu nipe locationa ya biashara ya Matunda.
Kwajinsi dunia inavyo kwenda kwa kasi. Na vile akina sisi tunavyo zidi kuelimika, watu wengi tunakula sana matunda hasa nyakati za jioni. Pia kwakuwa tumekuwa wavivu na pengine tunabanwa na kazi za kujenga taifa, basi tunajikuta hatupati nafasi ya kwenda sokoni kunua matunda.
Ninaamini ukiweka kijiwe hapa Area-C, kwenye kituo cha NAM hapo lazima utauza.
Ukiweka matunda pale njia panda inayo gawanyisha Area-C na D, pale kwa kona ya Pezzeria kama unaelekea Desert, lazima uuze pale.
Pia kila nikipita hapo Malaika Annex, sioni kama kuna muuza matunda kwa sisi tunao ingia kugonga whatever-Vant....
Mkuu, nimechoka kuandika
 
Mkuu Ushimen, asante kwa kutoa mwongozo wa fursa zinazopatikana Dom.

Nina mpango wa kufungua duka la cosmetics huko, naomba mwongozo ni mtaa gani unafaa zaidi , ambao ntapata wateja wengi.

Asante
 
Ni sehemu nzuri ile kwani kuna maafisa wengi wa serikali kwenye hayo majengo na wengine wanatoka kule wizarani udom jioni wanapita pale.

Kadhalika wale wafanyakazi wa udom na wanafunzi wanaweza kuwa wateja wako kwa siku za baadae.

Na ili kuongeza efficiency unakua unafanya delivery kule maofisini unaanza hata na mmoja wakiona bidhaa nzuri lazima wataagiza na wengine.


Kwenye biashara ya chakula faida sio kubwa sana hivyo unatakiwa kuwa na wateja wengi zaidi ili uone faida.

Ikikupendeza tengeneza na juice kabisa ziite HAWACHI JUICE. na uuze na matunda yale take away kwa sababu hapo maofisa ni wengi.


Mwaka jana nilikua na kijiwe cha matunda pale sema mambo fulani yalinibaana nikaacha ile kurudi akawa ashachukua jamaa mwingine. Pale kuna hela.

Kitu kingine kupata location pale inasumbua kidogo. Jitahidi lakini.

Na ukianza biashara ulete mrejesho tukupe ushauri zaidi.

NB: UKIFANYA KAZI KWA BIDII HUKOSI 20K TAKE HOME KAMA UPO WEWE ILA UKIACHIA MTU HUWEZI KUKOSA 10K KWA SIKU
Nenda barabara ya kuelekea makulu, baada ya kupita jengo la BoT na unapo karibia Treasure tower, kuna njia panda inayo elekea kushoto kama unarudi Veta. Pale njia panda kuna boda wengi, taxi bubu kwa wingi, mkuu pale unaweza ukaweka biashara ya kiepe/dume na matunda ukauza vizuri sana. Kumbuka pale pana mzunguko na muingiliano mkubwa wa watu pia wanao tokea jengo la NHIF pamoja na jengo la CAG
 
Mkuu Ushimen, asante kwa kutoa mwongozo wa fursa zinazopatikana Dom.

Nina mpango wa kufungua duka la cosmetics huko, naomba mwongozo ni mtaa gani unafaa zaidi , ambao ntapata wateja wengi.

Asante
Mkuu, kwanza pole kwa kuchelewa kukujibu hapa.
Na kuhusiana na swalilako naomba nianze kwa maelezo yafuatayo:-
Dodoma kuna vyuo vungi sana, na pia wahamiaji wanaingia kwa kasi sana, hivyo hali hii hupelekea muingiliano na mzunguko wa pesa kuwepo kwa kasi.
Kwa ushauri wangu kuhusu aina hiyo ya biashara unayo fikiria kuifungua, unaweza kuifanya popote katikati ya mji hasa maeneo ya kuanzia one way, barabara 1 hadi ya 8, maeneo ya sango na hata maeneo ya 7/7, na kwabisahara yako ukiichanganya na nywele za wadada utapata biashara nzuri chief.

Karibu sana Dodoma
 
Mkuu, kwanza pole kwa kuchelewa kukujibu hapa.
Na kuhusiana na swalilako naomba nianze kwa maelezo yafuatayo:-
Dodoma kuna vyuo vungi sana, na pia wahamiaji wanaingia kwa kasi sana, hivyo hali hii hupelekea muingiliano na mzunguko wa pesa kuwepo kwa kasi.
Kwa ushauri wangu kuhusu aina hiyo ya biashara unayo fikiria kuifungua, unaweza kuifanya popote katikati ya mji hasa maeneo ya kuanzia one way, barabara 1 hadi ya 8, maeneo ya sango na hata maeneo ya 7/7, na kwabisahara yako ukiichanganya na nywele za wadada utapata biashara nzuri chief.

Karibu sana Dodoma
Ahsante, nimekupata mkuu
 
Nafikiria kufungua studio ya picha(photoshoot) na kazi za graphics vipi mkuu eneo gan litanifaa? Je ni biashar itayolipa au? Naomb muongoz wako mkuu
 
Nafikiria kufungua studio ya picha(photoshoot) na kazi za graphics vipi mkuu eneo gan litanifaa? Je ni biashar itayolipa au? Naomb muongoz wako mkuu
Mkuu, binafsi sina uzowefu kwenye biasara hii.
Lakini tu nikushauri kwamba, Dodoma ni jiji/mji unao kuwa kwa kasi sana. Na nikiangalia naona serikali imeelekeza fedha nyingi Dodoma, hali ambayo imeprlekea mzunguko wa pesa kuwa mkubwa kiasi.
Ninacho kushauri tu nikwamba ukitaka kufanya aina hiyo ya biashara, kwanza anza na uthubutu kwakuwa tayari umesha anza na wazo, basi karibu Dodoma na ujipe walau siku 3 za kuzunguka na kufanya utafiti kidogo.
 
Mkuu Ushimen nahitaji kufungua biashara ya mini supermarket hapa dodoma, ni maeneo gani kwa uzoefu wako yanafaa kwa hii biashara.. Natanguliza shukrani
 
Pole na hongereni kwa kuwa wenye afya njema. Na kwapamoja tuwaombee wale wote ambao wakati kama huu hawana nafasi ya kusoma haya tuliopata pumzi ya bure na tukayasikia, kuona, kusoma na kuchangia.
Kwakuwa Mungu wetu ni mwema, basi yote kwake ni mema pia.

1. Ungekua Dom ningekupa wazo/location ya biashara ya chipsi dume, na ninahakika hapa ungeweza kupata faida isiyo punguwa 10 elfu per day, kwa mtaji usio zidi elfu 300.
2. Pia ningeweza kukupa wazo/location ya biashara ya majeneza ambapo ungeweza pata faida isiyo punguwa 100 elfu kwa kila wiki kwa mtaji usio zidi elfu 1,200.
3. Na ningekupa wazo/location yenye ungefanya biashara ya matunda kwa mtaji usio zidi 400 kwa kupata faida isiyo punguwa 12 elfu daily.
4. Alafu ninge kupa wazo/locations kadhaa ya kufanya biashara ya shoe shine/kusafisha viatu kwa mtaji usio zidi 100 elfu na ukapata faida isiyo punguwa 5 elfu kila kukicha.

Ebu ngoja nimalizie kwanza hii whatever-Vant, then kesho nitakuja na mawazo mengine kwenye muendelezo.
Kwa biashara ya majeneza wap panafaa mkuu@ushimen
 
Mkuu Ushimen nahitaji kufungua biashara ya mini supermarket hapa dodoma, ni maeneo gani kwa uzoefu wako yanafaa kwa hii biashara.. Natanguliza shukrani
Mkuu, kwanza nikuombe radhi kwa kuchelwa kujibu hoja yako na kama ujuavyo jana ilikuwa oyaoya pale Pestana, hivyo kidogo nilichelewa kulala sababu ya whatever-Vant...

Nikirudi kwenye hoja ya msingi ni kwamba, Dodoma unaweza fungua Mini Supermarket kwenye maeneo yafuatayo.
Kama utapata eneo pale Wajenzi, njiapanda ya kwenda kwa Kasim Majaliwa panapo gawanyika na njia ye kuelekea Chang'ombe, kama unaelekea Mipango ukitokea mjini.
Pia ukiweza kupata eneo la biashara yako kule mitaa ya St.John itafaa zaidi.
Na ukipata jengo maeneo ya Kito Bar, kama unatokea Police Central, kuelekea Mlezi.
Na ukipata eneo pale mitaa ya Stella, Nkuhungu mkabala na kanisa LA Roman itakuwa shangwe tupu.
Kwa kifupi maeneo ni mengi, na ikiwa kweli unania ya kufanya biashara, basi nakushauri utembelee mitaa hiyo na ufanye utafiti.

Karibu sana Dodoma...
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom