Ushimen: Ebu ngoja leo niwape mawazo machache ya kujikwamua

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
37,170
85,200
Pole na hongereni kwa kuwa wenye afya njema. Na kwapamoja tuwaombee wale wote ambao wakati kama huu hawana nafasi ya kusoma haya tuliopata pumzi ya bure na tukayasikia, kuona, kusoma na kuchangia. Kwakuwa Mungu wetu ni mwema, basi yote kwake ni mema pia.

1. Ungekua Dom ningekupa wazo/location ya biashara ya chipsi dume, na ninahakika hapa ungeweza kupata faida isiyo punguwa 10 elfu per day, kwa mtaji usio zidi elfu 300.

2. Pia ningeweza kukupa wazo/location ya biashara ya majeneza ambapo ungeweza pata faida isiyo punguwa 100 elfu kwa kila wiki kwa mtaji usio zidi elfu 1,200.

3. Na ningekupa wazo/location yenye ungefanya biashara ya matunda kwa mtaji usio zidi 400 kwa kupata faida isiyo punguwa 12 elfu daily.

4. Alafu ninge kupa wazo/locations kadhaa ya kufanya biashara ya shoe shine/kusafisha viatu kwa mtaji usio zidi 100 elfu na ukapata faida isiyo punguwa 5 elfu kila kukicha.

Ebu ngoja nimalizie kwanza hii whatever-Vant, then kesho nitakuja na mawazo mengine kwenye muendelezo.
 
Chipsi dume ndio issue hapo, unauzia mtaa gani, maili mbili, makole, airport, mitaa ya st. John au wapi?
 
Comrade, tatizo la vijana ni kuendekeza woga hasa kwenye kuthubutu. Na mbaya sana ni kusikiliza eti watu watasema nini, wakati wanasahuau kwamba wao wanataka nini hasa...
yaani mm na lidegree langu nikauze chips dume!!!? Au nikapige viatu rangi?? 😀, utani tu mkuu hizi ndio zingekuwa comments za wasomi kama ingekuwa ni enzi zile za jk kurudi nyuma, ambapo ajira kwa wasomi zilikuwa ni za kumwaga.
 
yaani mm na lidegree langu nikauze chips dume!!!? Au nikapige viatu rangi?? , utani tu mkuu hizi ndio zingekuwa comments za wasomi kama ingekuwa ni enzi zile za jk kurudi nyuma, ambapo ajira kwa wasomi zilikuwa ni za kumwaga.
Mkuu, kila kukicha humu jf naona vijana wakilalamika kuhusu ajira na wengi wanalalamika zaidi hata kufikia kuomba wasaidiwe mawazo ya biashara.
 
Tunasubiri mkuu
Kwalugha nyepesi naweza sema kwamba vijana wengi wana danganyika na degree walizo nazo. Lakini wanasahau kwamba pindi wanapo kosa ajira tu, hizo degree zao zinapoteza thamani yake.

Vijana wengi wanapenda kuishi kwa ndoto kubwa, lakini wanasahau kwamba pesa kubwa huanzia kwenye pesa ndogo.
Nikiwa mkweli huwa nashangaa sana ninapo waona vijana wanalalamika na kuomba omba pasipo kujitathmini kwamba hata nguvu na afya njema walizo zawadiwa na Mungu wetu, hivyo ni mtaji tosha.
 
Nipo Dom naomba location ya biashara ya kiepe.
Nenda barabara ya kuelekea makulu, baada ya kupita jengo la BoT na unapo karibia Treasure tower, kuna njia panda inayo elekea kushoto kama unarudi Veta. Pale njia panda kuna boda wengi, taxi bubu kwa wingi, mkuu pale unaweza ukaweka biashara ya kiepe/dume na matunda ukauza vizuri sana. Kumbuka pale pana mzunguko na muingiliano mkubwa wa watu pia wanao tokea jengo la NHIF pamoja na jengo la CAG
 
Nenda barabara ya kuelekea makulu, baada ya kupita jengo la BoT na unapo karibia Treasure tower, kuna njia panda inayo elekea kushoto kama unarudi Veta. Pale njia panda kuna boda wengi, taxi bubu kwa wingi, mkuu pale unaweza ukaweka biashara ya kiepe/dume na matunda ukauza vizuri sana. Kumbuka pale pana mzunguko na muingiliano mkubwa wa watu pia wanao tokea jengo la NHIF pamoja na jengo la CAG
Shukrani mkuu,ishaalah nitaanza kesho kufika eneo hilo.
 
Back
Top Bottom