Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 19,953
- 34,446
Heshima kwenu wanajamvi,
Nchi za Kiarabu zilifanikiwa sana kutumia dhahabu nyeusi (Mafuta) kuitenga Israel.Nchi nyingi zenye uchumi dhaifu hasa nchi za kiafrika zilijikuta zikitumbukia katika mtego wa kuziunga nchi za kiarabu mkono dhidi ya Israel.
Tanzania na nchi nyingi zilifuta uhusiano wa kibalozi na Israel na kuiunga mkono Palestine.Ikumbukwe uhusiano wa muda mrefu baina ya Israel na Tanzania ulikuwa na manufaa ya kiuchumi,kisiasa na kijamii.Taifa la Israel lilisaidia kuanzishwa kwa JKT,ujenzi wa hotel ya Kilimanjaro,Seventy seven ..... na miradi mingine mingi yenye manufaa makubwa sana.Baada ya Tanzania kufunga ubalozi na Israel na kuamua kufuata mkumbo wa kiarabu hakuna manufaa ya maana tuliyopata.Hata bei za mafuta katika soko la dunia hatukupunguziwa bei,sana sana tuliona kiongozi wa Libya akijitahidi kujivika ufalme wa Afrika (ukoloni mwingine)
Waziri mkuu wa Israel yuko nchi Uganda na baadae ataendelea na ziara yake nchi za Rwanda,Kenya na Ethiopia.Jambo hili lisingewezekana kufanyika miaka ya 1970s,80s,90s lakini leo mwaka 2016 limefanyika tena kwa mbwembwe kubwa na kuhudhuriwa na marais wa Zambia,Rwanda,Kenya,Waziri Mkuu wa Ethiopia na Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania.
Nini kimetokea hadi nchi nyingi za Afrika kubadili msimmo wazi wazi ?.Najaribu kufikirisha akili kiduchu nayaangazia mambo kadhaa yamkini yamechangia mbadiliko haya kwa namna moja au nyingine.
Mosi,nadhani nchi za kiarabu hazina tena ule mshikamano uliokuwepo mwanzo.Waarabu/waajemi wamegawanyika sana hasa katika misimamo ya kimadhehebu (dini) Ushia na Usuni umewagawanya sana hawana tena umoja wanatazama zaidi madhehebu kuliko Uislamu wao.
Pili,nadhani uchumi wa mafuta waliokuwa wakiutumia kama silaha yao kubwa sasa hali ni tofauti nchi nyingi Amerika kusini,Afrika na hata USA wamezidi kugundua mafuta na kupunguza au kuacha kuzitegemea nchi za kiarabu.Mafuta ilikuwa fimbo ya kuzinyanyasa nchi masikini hasa nchi za afrika ambazo zilifuata siasa ya kuitenga Israel si kwasababu zilikuwa na sababu za maana lahasha bali ziliogopa kitisho cha kunyimwa mafuta na waarabu.Uganda ni mfano mzuri inatarajiwa mwaka 2020 itaanza kuuza mafuta yake katika soko la dunia,Kenya,Congo DRC na nchi nyingine nyingi zimegundua mafuta na kupunguza au kuweka kando ushawishi wa nchi za kiarabu.
Naomba kuwasilisha.