Ushawishi wa China barani Afrika watokana na ushirikiano wa dhati kati ya pande hizo mbili

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,003
1,024
pap-r8-china-34-countries-external_influence.png
Hivi karibuni, shirika maarufu la uchunguzi wa maoni la Afrika la Afrobarometer limetoa ripoti ya uchunguzi wa maoni, ikionesha kuwa ushawishi wa China barani Afrika unashika nafasi ya kwanza duniani, mbele ya Marekani, mashirika ya kikanda, mashirika ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Haya ni matokeo ya ushirikiano wa dhati kati ya China na Afrika kwa miaka mingi.

Uchunguzi huo uliofanywa katika nchi 34 barani Afrika unaonesha kuwa, kati ya watu 48,084 waliohojiwa ana kwa ana, asilimia 63 wanaona kuwa ushawishi wa China kwenye mambo ya uchumi na siasa katika nchi zao ulikuwa “mkubwa sana” au “mkubwa kwa kiasi”, huku asilimia 66 wakiamini kuwa ushawishi wa kiuchumi wa China barani Afrika ni chanya.

Kwa muda mrefu, China imekuwa ikifanya ushirikiano mzuri na nchi za Afrika katika nyanja mbalimbali, na kupata mafanikio mengi makubwa. Kwa upande wa biashara, China imeendelea kuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 12 mfululizo. Tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili imeongezeka kuwa dola bilioni 200 za Kimarekani mwaka 2020 kutoka dola bilioni 10 ya mwaka 2000, na kuongezeka kwa mara 20. Kwa upande wa miundombinu, Afrika imekuwa soko la pili la China kwa miradi ya ujenzi wa miundombinu katika nchi za nje. China imetekeleza miradi mingi ya miundombinu kufuatia mahitaji ya nchi za Afrika.

Takwimu zinaonyesha kuwa tangu kuanzishwa kwa FOCAC, makampuni ya China yameongeza na kuboresha zaidi ya kilomita 10,000 za reli na karibu kilomita 100,000 za barabara barani Afrika, na kutoa nafasi za ajira zaidi ya milioni 4.5. Kwa upande wa uwekezaji, uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika umezidi dola bilioni 43.4, za kimarekani, na kushika nafasi ya nne kwa ukubwa wa uwekezaji barani Afrika. Matokeo haya ya ushirikiano yamezifanya China na nchi za Afrika kuwa washirika wa maendeleo wenye hatima moja.

Tangu kutokea kwa janga la COVID-19 barani Afrika, China imetoa misaada mbalimbali kwa nchi za bara hilo, ikiwa ni pamoja na kutoa dawa na vifaa vya kujikinga na virusi, kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao, kutuma vikundi vya wataalam wa afya, na kutoa chanjo. Aidha, ili kuisaidia Afrika kukabiliana na athari za janga hilo kwa uchumi na jamii, China pia imefikia makubaliano ya kupunguza na kuahirisha malipo ya madeni na baadhi ya nchi za Afrika.

China ni rafiki na mshirika wa kutegemeka wa maendeleo wa Afrika. Ushirikiano wa China na Afrika unazingatia ustawi wa watu wa Afrika, na kufuata mahitaji na maslahi ya upande wa Afrika, bila ya kuweka masharti yoyote ya kisiasa. China inatumai kwa dhati kwamba nchi za Afrika zinaweza kujiendeleza na kujitegemea, na inapenda kuzisaidia nchi za Afrika katika kuongeza uwezo wao wa kujiendeleza. Hili linatambuliwa na kuthaminiwa na serikali na watu wa nchi za Afrika.

Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa FOCAC hivi karibuni utafanyika nchini Senegal. China na Afrika zitachukua fursa hii kupanua na kuimarisha zaidi ushirikiano wao katika nyanja mbalimbali, na kuendeleza ujenzi wa jumuiya ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja.
 
Mchina sijawahi kumwamini. Wazungu na wachina wote wanatuibia hakuna rafiki wa dhati ila bora wazungu.

Nasema hivi kwasababu ukicompare mishahara wanayolipwa waliojariwa na mzungu unakuta wanalipwa vizuri na benefits kibao. Sasa njoo kwa mchina, mishahara ovyo na mazingira ya kazi magumu hata iwe ni project kubwa.

Sasa watuibie na bado hata mishahara iwe kiduchu.
 
Waafrika wanabaguliwa China kuliko sehemu nyingine yoyote chini ya Jua! Njaa zenu mmerushiwa "makombo" mnawafagilia wabaguzi wakubwa!

Mko tayari kuwasaliti kaka na dada zenu kwa matumbo yenu! Mlaamiwe!
 
How do you mean?
Karibu kila nchi ya Afrika imepata uhuru.Basically ni uhuru wa kisiasa tu kwani kwa kiasi kikubwa bado tunatawaliwa kiuchumi na nchi tajiri. Uwepo wa institutions kama (WB, IMF, UN) ni platforms za kuhakikisha hatutoboi kiuchumi. Sasa China imekuja na strategy tofauti ya kutoa mikopo inayo tie in strategic infrastructure [Airports, bandari etc] kama collateral knowing somewhere down the road mta default na yeye kuchukua rasilimali hizo kuwa mali yake.

It will go on and on mpaka itafikia kuchukua mbuga za wanyama, madini etc.

Zambia (sina hakika na South Afrika) sasa hivi wana polisi wa kichina na kichina imekuwa ni lugha inayofundishwa mashuleni. Huitaji microscope kuona direction ambayo China inaelekea..
 
Karibu kila nchi ya Afrika imepata uhuru.Basically ni uhuru wa kisiasa tu kwani kwa kiasi kikubwa bado tunatawaliwa kiuchumi na nchi tajiri. Uwepo wa institutions kama ( WB, IMF, UN) ni platforms za kuhakikisha hatutoboi kiuchumi. Sasa China imekuja na strategy tofauti ya kutoa mikopo inayo tie in strategic infrastructure [Airports, bandari etc] kama collateral knowing somewhere down the road mta default na yeye kuchukua rasilimali hizo kuwa mali yake. It will go on and on mpaka itafikia kuchukua mbuga za wanyama, madini etc.
Zambia( sina hakika na South Afrika)sasa hivi wana polisi wa kichina na kichina imekuwa ni lugha inayofundishwa mashuleni. Huitaji microscope kuona direction ambayo China inaelekea..
Reading in between the lines one gets an impression you're unquestionably mega smart upstairs - now a million dollar question, is: Inakuwaje tena MTU msomi kama wewe unakubali ku-join band wagon ya main stream media za magharibi kwa lengo la kuwakandia Wachina by preaching evil of communism/socialism and blessings of Capitalism!!

For your information ukichunguza kwa umakini all allegations raised against Chinese in Africa, utabaini kwamba 99.99% ni Mickey Mouse stories fabricated by western Intel agencies to demonise ujio wa Chinese barani Africa, in other words ni a well organised crusade ya kuhujumu Wachina both Economically and Geopolitically.

Haya mambo ya ku-dramatise projects/uwekezaji wa Wachina barani Africa kwamba bila shaka una walakini mkubwa na wakinyonyaji/wizi tuhuma hizo ni za kutunga tu: Chukulia tuhuma kwamba eti Wachina walipora bandari ya Sri Lanka baada ya ujenzi kukamilika, wakati Serikali ya Sri Lanka haijawahi kulalamika popote kwamba hawatendewi haki na Wachina katika uendeshaji was Bandari husika - habari hizi zinaenezwa na Reuters, BBC,CNN,VoA na like mind wenzake. Haya tuje kwenye Bandari ya Djibuti adithi ni zile zile Wachina wezi, Wachina wezi, wanayasema hayo lakini wako kimya kuhusu USA kumiliki Military Air base Djibouti na kuitumia base kurusha Drones to kill and maim real and imaginary enemies.

Tukija Zambia, Congo DRC, Kenya, Uganda adithi ni zile zile: Wachina wamepora machimbo ya shaba, Wachina wamepora viwanja vya ndege, Wachina wamepora Bandari za watu - vyote hivyo wanadai kwamba wachina wamefikia hatuwa ya kuchukuwa mahamuzi hayo kama njia ya kufidia mikopo yao kwa nchi walizo kopesha - - kama nilivyo fafanua hapo mwanzo hatujawahi kusikia Serikali za nchi tajwa hapo juu zikilalamika kwenye mahakama za kimataifa kwamba Uchina inapora Mali zao kufidia mikopo - hatujawahi!

Upotoshaji huu mkubwa unakuwa manufactured na Serikali za Uingereza na Merikani kwa kutumia vyombo vyao vya habari wakiwa na ajenda ya siri yenye lengo la kuhujumu ujio wa Wachina barani Afrika, wazungu hawapendi kabisa ujio huo - ni mwafrika gani ambaye hajui pivotal role ambayo taifa la China lime-play in terms of ujenzi wa Viwanda, infrastructures (Reli, Barabara, madaraja, telecommunication, hydro electric Dams), usafiri, Shule za Ufundi and what have you, repeat, Chinese are helping Africans help themselves ni hilo, unlike vocal western Nations hell bent to draw a wegde between Africa and China.
 
Reading in between the lines one gets an impression you're unquestionably mega smart upstairs - now a million dollar question, is: Inakuwaje tena MTU msomi kama wewe unakubali ku-join band wagon ya main stream media za magharibi kwa lengo la kuwakandia Wachina by preaching evil of communism/socialism and blessings of Capitalism!!

For your information ukichunguza kwa umakini all allegations raised against Chinese in Africa, utabaini kwamba 99.99% ni Mickey Mouse stories fabricated by western Intel agencies to demonise ujio wa Chinese barani Africa, in other words ni a well organised crusade ya kuhujumu Wachina both Economically and Geopolitically.

Haya mambo ya ku-dramatise projects/uwekezaji wa Wachina barani Africa kwamba bila shaka una walakini mkubwa na wakinyonyaji/wizi tuhuma hizo ni za kutunga tu:hayo hayana ukweli wowote - chukulia mad
Hakuna mahali nime support Western capitalists infact nimeeleza kuwa institutions kama IMF, World Bank and the likes zipo strategically kuhakikisha third world countries will never see the light of economic freedom. Frankly both Western capitalists, China wote nawaona ni opportunists towards third world countries resources kila mmoja wao ana siphon kwa namna yake. It is all about carrot and stick - doesn't matter who gives more carrots or hits harder than the other.
 
Mchina sijawahi kumwamini. Wazungu na wachina wote wanatuibia hakuna rafiki wa dhati ila bora wazungu.
Nasema hivi kwasababu ukicompare mishahara wanayolipwa waliojariwa na mzungu unakuta wanalipwa vizuri na benefits kibao. Sasa njoo kwa mchina, mishahara ovyo na mazingira ya kazi magumu hata iwe ni project kubwa.
Sasa watuibie na bado hata mishahara iwe kiduchu.
Na kubalihana na wewe mchina sio mtu mzuri ni tapeli

Sent from my MAR-LX3A using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mahali nime support Western capitalists infact nimeeleza kuwa institutions kama IMF, World Bank and the likes zipo strategically kuhakikisha third world countries will never see the light of economic freedom. Frankly both Western capitalists, China wote nawaona ni opportunists towards third world countries resources kila mmoja wao ana siphon kwa namna yake. It is all about carrot and stick - doesn't matter who gives more carrots or hits harder than the other.
Please revisit my detailed comments - ya mwanzo ilikuwa uploaded/posted kabla sijakamilisha kuiandika - sorry.

One more thing, kutaja capitalism/communism sikulenga wewe kivile, nilikuwa natania.
 
Please revisit my detailed comments - ya mwanzo ilikuwa uploaded/posted kabla sijakamilisha kuiandika - sorry.

One more thing, kutaja capitalism/communism sikulenga wewe kivile, nilikuwa natania.
Ulikuwa unatania au umezidiwa hoja? Go and read to update your knowledge. Chinese has nothing called GOOD WISHES towards the Africans,rather than feeding it's Overgrowing Population inside China itself.
 
China wamepata ushawishi mkubwa. barani Africa kwa lengo pekee ya kupata eneo la kufanyia majaribio ya vitu vyake, kibiashara kiteknolojia, na kutupa takataka zote mbovu za ujenzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo tukubali propaganda za Kichina au sio?
Comments nyingine bwana!! Ni hivi mkuu, Wachina wana ahidi na kutenda/timiza/tekeleza tofauti kabisa na wasanii wa Hollywood California.

Hulka ya Wachina ni kuelewana na kutaka kushirikiana na Mataifa karibu yote Duniani without strings attached - mfano: lini Wachina waliwahi kushauri mataifa ya Africa, Asia na Latin Amerika kuhusu mataifa gani washirikiane nayo au kuingilia masuala ya ndani hasa yanayo husu uchaguzi na uzabazabina wao wa kujidai wana tetea haki za binadamu na demokrasia, wakati wao ndio vinara wa ukihukwaji wa haki za binadamu Duniani - their trigger happy Policemen shoots first and asks questions later na ukiwa ni MTU mweusi au Latino ndio basi tena kifo mkononi!!

Taifa kama hilo lina moral authority gani kuwapa somo Wachina kuhusu masuala ya haki za binadamu na demokrasia.

USA waeleze Dunia lini rafiki zao Falme ya Saudi Arabia waliwahi kupiga kura na kuchagua viongozi kwa njia ya kidemokrasia, lini? Merikani hiko radhi kuwasema vibaya Serikali ya Korea ya Kaskazini na Kim, Uchina na Urusi lakini sio Saudi Arabia!! Double standard, that is.
 
Back
Top Bottom