Ushawahi zimikiwa na jiko la gesi ukiwa unapika?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,190
4,103
Jamani gesi ni nishati inayorahisisha mapishi kwa haraka.

Ila ina kero yake jamani wakati ndio unapika inaweza isha ghafla na pengine kwa wakati huo huna hela ya kununua tena au unanunua mbali.

Unaanza hangaika na kuwasha mkaa nk.

Hebu tueleze ilikuwaje.

1621419131400.png

Ilinizimikia juzi tu hapo, nilirudi kwenye mishe mida ya saa 9 njaa balaa.. Nikapika mboga ikaiva.

Nikaweka sufuria ya ugali jikoni, maji yakachemka nikaweka unga ile naanza kuchanganya unga (kusonga) ikazima. Dah, nilikula ile mboga, ule urojo wa ugali nikawapa kuku nikaenda kukopa Ugali mgahawani.

Nilishindwa kuihimili njaa!
 
Kuna siku nimekata nyanya vitungu karot na pili pil hoho vzur nmeweka kwny sahani kwa ajiri ya kuunga nmeweka mafuta kwny sufuri inachemka ghafla ges imekata afu mtung mkubwa nkaishiwa poz ikabid nmwage kila kitu jiko la mkaa nlikuwa sina
 
Ishawahi kunitokea hii, usiku napika zangu chips ndiyo nimeweka hata hazijaiva jiko si likazima, aargh ni usiku na sikua na pesa nilichofanya nikatoa viazi kwenye mafuta nikalala na njaa tu😬🙌

Na nahisi hata sahivi inakaribia kuisha gas gani tangu November 2020 hadi leo ipo tu mmh , japo huwa sipiki mara nyingi ila...
 
Ishawahi kunitokea hii, usiku napika zangu chips ndiyo nimeweka hata hazijaiva jiko si likazima, aargh ni usiku na sikua na pesa nilichofanya nikatoa viazi kwenye mafuta nikalala na njaa tu

Na nahisi hata sahivi inakaribia kuisha gas gani tangu November 2020 hadi leo ipo tu mmh , japo huwa sipiki mara nyingi ila...
Jiandae kulala njaa tena hahaaaa
 
Kuna siku nmekata nyanya vitungu karot na pili pil hoho vzur nmeweka kwny sahani kwa ajiri ya kuunga nmeweka mafuta kwny sufuri inachemka ghafla ges imekata afu mtung mkubwa nkaishiwa poz ikabid nmwage kila kitu jiko la mkaa nlikuwa sina
Pole sana mkuu
 
Ilinizimikia juzi tu hapo, nilirudi kwenye mishe mida ya saa 9 njaa balaa.. Nikapika mboga ikaiva.

Nikaweka sufuria ya ugali jikoni, maji yakachemka nikaweka unga ile naanza kuchanganya unga (kusonga) ikazima. Dah, nilikula ile mboga, ule urojo wa ugali nikawapa kuku nikaenda kukopa Ugali mgahawani.

Nilishindwa kuihimili njaa!
Pole sana
 
Back
Top Bottom