Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,036
- 20,337
- Thread starter
- #21
Pole sana mkuu Kumbe hua wanatumia na dawa kufanya mazingira.Nilikua nasikia watu wanatapeliwa simu wanawekewa sabuni,
nikawa nasema haiwezekani ukapewa simu alafu umrudishie akuwekee kwenye bahasha.
maana kwa staili hiyo wale wezi ndio wanabadilisha simu na kukuwekea sabuni bila wewe kujua.
sasa siku moja katika pitapita zangu kariakoo karibu na duka la sandaland pale nikakutana na
wale matapeli wa simu, ilikua tecno spark ile nakumbuka, mmoja akawa anasema
ana elfu ishirini tuu. yule aliye kua akiuza akawa anasema 25, nilipo kua nakatiza karibu yao
yule muuzaj akanambia huyu jamaa ana elfu ishirini mimi nataka elfu 25 tu, akilini nasema
yess hawa ndo wale matapeli subiri sasa niwaonyeshe
nikamwambia hebu lete hiyo simu, nikaangalia nikaikagua kama ndio yenyewe nikaridhika nayo nikaiweka mfukoni
nikamwambia sasa sikia hapa mimi sina pesa twende kwenye kibanda cha mpesa nikakutoleepesa yako
yule jamaa akakubali, sasa wakati tunaenda niliitoa ile simu nikawa naiangalia tena. yule jamaa akaniambia twende haraka
iyo simu nimeikwapua dukani hapo, polisi yenyew sio mbali sitaki kukamatwa hapa , nikamwambia kama unaharaka
chukua sim yako usinchoshe, akasema basi twende tu
tukafika kwenye kibanda nikatoa pesa , nikaangalia sim mara ya mwisho nikampa pesa jamaa nikaweka simu mfukoni
nikaenda kupanda basi, nikasema subiri niweke laini humu nianze kuitumia, aisee nilipoweka mkono mfukoni nakutoa.
sikuamini kitu nilichokua nimeshikilia mkononi mwangu, nilitumbua mimacho kama kobe. nikairudisha mfukoni maana
sikua na ujasiri wa kutupa ile sabuni mule ndani ya basi
nikabaki tu najichekea mwenyewe huku nikiamini atakua kanifanyia mazingaombwe, sio kwa umakini ule nilio kuanao.
basi kilicho fauta tu ni kuanza kuifikiria ile 25 yangu ningeinunulia vitu gani kama nisinge tapeliwa
Mimi nikajua hua ni ujanja tu wakati wa kubadili ili kumukabidhi muhusika.