Ushawahi kutapeliwa na rafiki yako wa karibu

Mshkaji wangu sana mwanangu sana anakofanya kazi palisimama kutokana na azabu ya serikali so mkewe yupo hospital aksema niazime 50k tukishafungua nakulipa ni mwezi ujao tu akaleta camera ya bondi nikamwambia hapana chukua pesa then muda ukifika mkifungua niludishie kiroho safi na iyo canera baki nayo we mwanangu sana.
niliona camera kama tunauziana ivi na ile ela nikaacha kulipa bili ya maji nikampa yeye nilijua nikichukua camera ndio kaniuzia na camera yenyewe ni vidogo ivi. Muda ukawadia kimya muda unakwenda kimya aisee nikienda kwake ana Samsung mpya Mara kachange ana iPhone mpya Du moyoni najiuliza mshkaji akumbuki den langu alafu anasema kabisa hii niliagiza dar 350k hii simu. khaaaa kudadadeki napata hasira moyoni kumbuka ni manager wa longe kubwa tu 50 kwake sio tatizo.
Kuna siku nikasema ngoja nimkumbushe mwana ile ela vipi anajibu biashara sio nzur kabisa mbaya sana khaaaa wakati anavyotumbua namuona nikamfata akanipa EF 10 yani kibishi duuuuuuuuu moyoni nikacheka mkikaa utaskia uyu demu namuandalia 20k naenda chapa da Kuna siku ananiambia kama unahitaji demu niambie kila kitu nagharamia Mimi ahaaa nikamwambia kabla ungenipa kwanza ile 40k iliyobaki kimasihara ivi naongea anaijbu sasa ile tulia tu ntakupa ile bili ya maji ikanijambia ikabidi nikope nilipe moyoni iliniuma na inaniuma toka mwez Tisa 2019 mpaka Leo 2020 hii wa Tisa it means mwaka kimya sijawai kumbusha tena. Ila juzi kupitia twita nimeona post ya Mo dewji mikopo inaua urafiki na huo ndio ukweli japo bado tupo ila ishu ya pesa nimekaa mbali never.
Kuna mjeda kazama na 75k yangu piga simu apokei mesag ajibu uyu nilimpa nikijua kwa kazi yake akuna longo longo atanilipa 0-0 Amna kitu akuna maandshi utadai wapi nikapiga chini life goes on
.MIKOPO INAUA URAFIKI.
√√√√√√√√√√√√√√√√√√
 
Mm nilishatapeliwa na jamaa niliekua nae laki tatu ,aisee ingawa nacheka nae kwasasa Ila tokea anifanyie huo uhuni sijawah mkubal hata cku moja ingawa na yeye analijua Hilo kuwa simkubal kabisa so kilichobak hapa Ni urafik wa kinafki tu.

Na Nina mpango wa kumfungia vyoo jumla maana pesa ya kunilipa anayo Sana tu sema dharau na mazoea.

Kuna kenge mwingine nilimkarijisha kwangu no iliish nae vzr Sana Zaid ya wiki moja anakula anachotaka anakunywa anachotaka ,siku nimeenda job akachukua simu yang mpya kabisa ilikuwa haina hata mwez ,akachagua pamba zangu Kali zote akasepa na akaniblock mazima .Ila huyu najua tu ipo cku ntaonana nae tu na tutamalizana kibingwa yaan afe kipa au afe beki.

In short kwasasa sitak urafik na mtu yeyote na sitak mtu akanyage kwangu au mtu kuniazima pesa ,sitak Zaid tukikutana tupeane hi bac shobo zingine sitak kabisa na nawashukuru maana wamenifundisha ukauzu ambao sikuzaliwa nao
 
..niazime tuu..ntakurejeshea mshahara ukitoka mwisho wa mwezii.

..niazime tuu..ntakurejeshea ....kikoba kikivunjwaa

..niazime tuu..ntakurejeshea . kuna hela nategemea kupata wiki ijayoo
Hizi kauli hizi mnh, ukija kumkumbushia ugomvi wake unakua kama vita ya 4 ya dunia
 
Sijawahi kutapeliwa ila nimejifunza kwa wezangu waliotapeliwa, sasa kuna bro wangu mmoja tulikua tunafanya kazi kampuni moja ni mtu wa starehe sana,,na tunaaminiana sana, sasa kuna siku kaja kunikopa hela 1M, nilichomjibu hakuamini masikio yake nikamwambia unaweka bond nini, akaanza kuleta habari za kujuana kwamba atarudisha mapema kama wiki 1 hivi, nikamwambia kwako kuna TV kubwa tu LG55inch weka bond nikupe hela, na kwa vile umeomba wiki 1 mimi nakuongezea wiki 1 ikipita hapo tusitafutane kuhusu TV, wiki ikakata ya kwanza namchora tu akila bata kwenye ki IST chake tena mda mwingne tukiwa wote tunakula bata na wala simkumbushi kuhusu deni lake,, ikabaki siku 2 wiki ya pili iishe ananiletea nusu deni eti 400K nikamkatalia, nikamwambia fata makubaliano, siku zikapita TV nikabaki nayo, nikaona inanikosesha amani tu nikiwa nayo nikaiuza mil 2, mpaka leo jamaa hatuongei kanichunia. anapambana na hali yake huko na mimi napambana na hali yangu.
Ulimuweza
 
Mimi siju niseme nilitapeliwa au nilidanganywa hata sijui ikoje hii ila roho inaniuma mpaka leo.

Mwanzon mwaka huu nikiw nafanya kibarua kampuni X bos wangu alikua na friend wake ambaye naye anamiliki kampuni Y.Zote zinajihusisha na kandarasi za IT.Ikatokea tumezoeana sana na frnd ake bos mwenye kampuni Y.Ni kampuni sio kubwa snaa ni za kawaida tu.Kilichotufanya kuzoeana na mshkaji ni baada ya yy kugundua pale ofsn ndio nimekua na take charge ya mirad kuanzia kuomba tender mpaka execution.Bos yy ana deal na yale yalio nje ya uwezo wangu like zile tender za kupika mezan ambazo u need to utilize connection zako kwa washika dau walioko kwenye taasis zinazohitaji huduma ila hiz za ushindan mm ndio nakomaa nazo.

Basi bwana kwakua jamaa alikua ana tatizo upande huo hasa wa kuandaa competitive documents, hivyo kaz kwake ikawa ni za nadra nadra tu mpaka siku aliponitafuta.Akanieleza A to Z alichokua nataka nimsaidie.Ofcz i was no body kwenye kampuni yetu, kazi nying ila wako mshahara tu hata ufanye ku acquire mrad wa 300m.
Kipind ananitafuta nilikua napambana na miradi miwili ya taasisi moja ya serikali iko mikoa tofauti.Baada ya kunililia sana shida na kutoa ahadi za hapa na pale tukafikia makubaliano nimfanyie kaz ya ku apply bid same same nilizokua naziomba kupitia kampuni yetu.

Maneno yasiwe mengi , nikampigia kazi (ofcz kile nilichokifa ya kwa kampuni yetu X nikaki boresha zaid nikakitumia kwa kampuni Y ya mshkaji) kwa makubaliano kwamba akipata tender yangu ni 1M kwa kila mradi kama fee.Pia nita execute mwenyewe mwanzo mwisho (hapa kuna agreement ambazo nilimu ensure kua nitamsaidia ku maximize profit kwa ku lower expenses as nilikua na magumash zangu za ku access grey market so same products OG unazipata kw bei chee kwakua delears wana namna zao za ku kwepa taxes) .hapa tukawa n makubaliano ya kulipana kivingine so jumla ikaja kama 5m.

Mungu si athumani jamaa akaikwaa miradi miwili .ofcz haikua mikubwa Cz ilikua na grand total ya 79M.
E bwana eee toka hapo simu zikawa hazipokelewi.Nikaja kumpata kashamaliza miradi na kashalipwa.
Nadai changu (zile 2M sasa za kumpatisha miradi) akaanza stori mara bank accntza kampun alikua ame over draft mara nin sijui daah..nikaona isiwe shida inawezekana Mungu kaniadabisha maana mm nili snitch chama langu nikampa deal mdau mwingine ...naye kaniliza.Ila kwakifupi jamaa ni kama kanitapel maana mpaka leo ni stor ingawa ana kiri ninamdai na akipata atanipa ila mpaka na post hii mtanzania mwenzenu 0-0 .Roho huwa inaniuma sana.

NB.
Alivyomjinga sasa mwez uliopita akanitafuta nimjazie tena document..Dah..mjini akil nguvu kijijin
Hana hata haya mxiuuu,
Kwahiyo na wewe ukamjazia au........
Nimejikuta hasira napata mimi
 
Kuna mtu anataka kunikopesha kinguvu.Kuna biashara anafanya sasa anaforce mzigo uishe haraka.Nimemwambia bajeti yangu kwa Sasa hairuhusu kununua kitu ambacho sikupanga.Ananiambia we kopa tu utarejesha japo Kuna hela itaongezeka,nimejibu kuwa siwezi kuingia kwenye ugomvi wa kudaiana wakati najua siwezi kurejesha.Kaning'ang'ania sijui kanionaje,ila sijataka kuingia kwenye majaribu
 
Duh jamani Kuna watu wana roho Mbaya mno jamani huyo sio binadamu ni mnyama
Mimi rafiki yangu alikuwa anakuja kwangu ananikopa million tatu Nampa bila riba, anarudisha, siku nilipata shida nikamkopa nilikoma. Alinipa hela VIZURI Ila baada ya week akanifata kageuka anasema hela sio yake hivyo kila million niilipie laki moja. Na Ile hela nikawa siipati kila week namlipa laki tatu Hadi nikafilisika. Nikaja kugundua kumbe kile kipindi ananikopa Ni alikua anajenga namna ili Mimi nikipata shida nimkope yeye ili animalize.
 
Mimi nilitapeliwa na ndugu kabisa upande wa mama yani jamaa tulikua vizuri sana siku moja rafiki yangu akaniomba nimtafutie mtu amtengenezee furniture yeye alikua mkoa ili akirudi ziwe tayari.
Basi sababu huyo ndugu yangu anajua sana kutengeneza nikaona nimpe kazi pia nilijua hawezi kuzingua au kutengeneza hovyo basi jamaa akatuma pesa nikampa yote yani kama laki 7 hivi na akaniambia poa natengeneza na sikumfuatilia kabisa sababu nilimuamini ndugu yangu.

Jamaa akarudi town nikawakutanisha mimi nilikua bize wakaenda kuangalia hizo furniture eti hazipo story nyingi kumbe hazikutengenezwa kabisa pesa kala, tangu hapo kaniblock home haji tena yani dah kaniachia msala.
Sema mshkaji akaniambia bro achana nae sidhani kama umeshirikiana nae kunidhurumu nakuamini sana nimesamehe kabisa. Mwaka wa 2 sasa huyo ndugu hatuongei pia na sitaki kuongea nae maisha mpuuzi yule, maana jamaa angeweza hata kunilaza ndani maana miamala yote inasoma kwangu aliyotuma nikasema kweli ndugu hawa dah sitakaa niamini tena mtu aisee.
 
It pains kwa kweli kuna jamaa nilimkopesha laki mbili kwanza akarudisha mshahara ulivyoingia tu mara ya pili akataka nimkopeshe laki tatu kama kawa msharaha ukiingia ananipa changu kawaida kwetu hatuchelwi naona ivi meseji kapata pesa namkumbusha dah anatype whsap dk 2 nzima kuja kusoma meseji ujinga tu😥😥😥😥kanipanga tena sijui pesa haitoshi nina familia nigaiye changu mwanangu kama ahadi kakataa katu ananichekea ofisi tu nilimwamini ghafla


Kwa kweli inaniuma sana nikiona huu uzi kwa nn watu hawasaidiki dunia ya sasa mtu pesa anayo ila kulipa mtihani
 
Mimi kuna mmoja hapa nilimkopesha pesa naona ananizungusha tu ila nishaweka nadhiri kabisa kwamba akinitapeli nitamfanya kitu kibaya au nimuue kabisa...mimi ni mmachame likija suala la pesa sipendag upumbavu
 
1. Kuna dogo nilimpokeaga akija kuanza chuo na kumtafutia mpaka kwa kuishi ila alinitapeli 280k miaka ya 2010-11 mpaka leo, alicheleweshewa hela yake ya ada mpaka siku ya deadline anahangaika tu. Kaja kunililia shida nikaenda kumlipia ada 350k tena jumamosi saa nne anatakiwa kuwaisha risiti chuo jumatatu afanye mtihani kwa ahadi father yake atamtumia pesa week inayofuata. Kafanya mtihani kamaliza akatumiwa ada yake, sasa hapo anacrew ana watoto wa chuo ada nishamlipia na mtihani ndiyo wamemaliza nikaona kwenye simu nimerushiwa 70k tu na akasenda likizo, washkaji zake wakanipa taarifa fujo alizofanya mjini. Kipindi hicho yeye bado anamwaka 1 chuo mimi nipo semester ya mwisho. Fatilia hela miezi 4 bila mafanikio chuo kimoja washkaji zake wote wanajua, washkaji zangu wanafahamu. Nikatulia, nikakutana naye last year mjini hapa, bro nipatie number yako. Week mbili kaniadd kwenye group lake la harusi, nilimchangia views zangu tu whatsapp group.

2. Kuna jamaa alikua kibarua eneo langu la kazi, payments zao ni 20k per day. Kaja na stori za mkewe kujifungua na mtoto kuumwa nikamuazima 30k tu. Ikapita miezi 3 hajalipa, sasa mfanyakazi huwezi kumdai kibarua kwa pressure hela kama hiyo, nikawa muelekeza tu umuhimu wa kulipa madeni. Siku nyingine anataka kukualika beer halafu ukimwambia hiyo hela lipia deni anapotea. Nikaja kugundua kakopa pia kwa wafanyakazi wenzangu na wenzake pia, tena kuna waliompa mpaka 300k, kiukweli jamaa hana sura ya hatia kabisa ukimwona very gentleman. Na ukimdai anakuelewa na anaonesha moyo wa kulipa ila halipi. Mwisho wa siku alinipa 10k na lile eneo la kazi alikimbia maana kuna watu walimdai mpaka kwake na kwa ndugu zake akahama mkoa.

3. Dah! Jamaa yangu kabisa huyu form 5 & 6 tumekaa wote ghetto, miaka miwili kishidashida tukishindia ukoko na hustle zote za kitaa, kodi tunalipa 7k kurasini uswahilini kabla zile nyumba hazijabomolewa. Tulikua marafiki sana, familia zikatufahamu washkaji. Tumechaguliwa chuo, chuo changu wanawahi kufungua, nafika tu 1st year na boom linaingia. Rafiki anatakiwa kuripoti na hata nauli alikua hana na ikasemekana boom lake litachelewa, kiroho safi natoa boom 100k yangu mchizi akarepoti chuo, boom likitema anirefund. Yaani 100k ikaua urafiki kabisa. Nilifahamu hela imeingia chuo chao nikamkumbusha jamaa mara 2 au 3 na hakulipa. 100k ikaua urafiki wetu mzee, sikumsema wala yeye hakunitafuta mpaka anamaliza chuo. Tunakutana mitandaoni humo na aliwahi nicheki mwanzo wa mwaka huu salamu tu ila kikubwa anajua urafiki wetu ulikufa baada ya kumtumia 100k na yeye kunitapeli. Captain kama unasoma hii ni mimi Engineer hapa na bado nakumbuka hata baada ya 10+ years.

4. Ndugu huwa nawakopesha kiasi ambacho huwa najua sitajutia kukipoteza, na kweli wengi huwa hawarudishi, na ndugu wasiorudisha hela huwa nawapenda maana kile kiasi kilikua kipimo na yeye asiporudisha simdai, ispokua hawezi kuja kukuazima kiasi kingine tena. Ila undugu unaendelea na kujuliana hali kupo ila pesa yangu ataisikia tu.
 
Kuna jamaa alikuwa rafiki yangu mnoo alinitapeli milioni na laki tatu akapote tangu mwaka 2019 sijui hata yuko wapi ila namuombea kwa mungu
 
Back
Top Bottom