Ushawahi kutapeliwa na rafiki yako wa karibu

Ungana na mwanahamisi singano

Anasimulia
Ushawahi kutapeliwa? Mimi nimetapeliwa Tsh milioni kumi (10m) na rafiki yangu wa karibu, (best friend) rafiki ambaye mpaka familia zinajuana. Ila 10m ikafanya urafiki, ushoga na udugu ukafa moja kwa moja. Ilikuwa hivi, Shoga alinunua gari ya kubeba mafuta na kuanza biashara.

Biashara yake ni kununua mafuta depo na kusambaza. Akaniomba niwekeze kwenye biashara yake mana ana upungufu wa pesa ya kuzungusha, tukakubaliana kila mwezi atanipa faida ya mtaji wangu 10% ambayo ni 1m. Na nikitaka pesa zangu nimpe notice ya mwezi 1. Nikaona ni jambo jema.

Badala ya kudunduliza kuweka akiba benki ngojea nimpe shoga, nami nipate tufaida. Nikampa 10m kash. Tulikubaliana tutaandikishana kwa lawyer ila makaratasi hayakuja. Mwezi wa kwanza nikatumiwa 1m fresh, mwezi wa pili mpaka nikakumbusha, nikatumiwa nusu nusu.

Nikaja kujua kuwa amechukua pesa kwa rafiki yetu mwingine kwa dizaini hiyo, ila sikumuuliza. Siku moja kwenye mazungumzo, akajisahau akasema sasa hana stress mana gari kawakodisha watengeneza barabara, yeye wanamlipa tu kwa kutumia gari yake. Nikamwambia, ni vema anirudishie pesa.

Hapo ndio shida ilipoanza, miezi kama minne hivi tunadaiana, nikashikwa na hasira nikamwambia ntampeleka polisi. Hamadiiii naletewa barua ya mwanasheria kuwa niache kumsumbua na kumtisha mteja wake. Jema ni kuwa barua ya mwanasheria wake ilikiri kuwa niwekeza hela kwa makubaliano.

Kiukweli nilipata ghadabu kubwa mno, nikapata mwanasheria akajibu barua. Swala likafika kwenye familia. Kaka yake akaahidi kuwa nitalipwa. Kutoka october 2018 mpaka leo sijalipwa hata mia. Na si kuwa hawana hela wana mashule ya nursery mpaka college, basi tu, dhulma.

Nikataka kufungua kesi, mama na baba Mishy wakanisomea risala ndefuuuuuuuuu. Nakumbuka mama aliniambia, kama familia yake wamemuacha rafiki yako akufanyie ubaya sisi wazazi wako hatukuruhusu umlipe mwenzio ubaya, ulinde uungwana wetu Samehe. Mungu akatajwa kama mara alfu...hapo.

Jana usiku, kuna mtu alikuwa analalamika katapeliwa kikombe (mug) na alikuwa determine kupata haki yake, ikanifanya nikumbuke madhila yangu, nikiri, kahoro bado kanauma - 10m parefu jamaniiii. Nikaona japo niandike kuwakumbusha msirudie kufanya ujinga niliofanya. Nimejifunza mnoo.

Asante
Me nilietapeliwa 800k na bosi wangu bora nipunguze hasira na kinyongo. Km watu mmetapeliwa 10m na mmesamehe.

Bosi wangu nmempa 1m mwaka 2018 nmeishiwa kulipwa 200k tuu. Nayo nimelipa baada ya mwaka na kwa kudai saana.
 
Hizi zimetulostisha wengi sana, but for now! Wacha nionekane mmbaya tu. Kulikoni nikupe kitu kwa ahadi ni aheri nikunyime tu maana haitanipunguzia chochote, unataka 1M leta gari paki acha funguo na card!

Mambo ya sijui next week ni uhakika, hayo siyataki hata kuyasikia. Ukifika ule muda ni kitendo cha kuita dalali tu, nauza kinachozidi namega riba yangu nakupa chenchi yako. Tunamalizana namna hio.
Me baada ya kupigwa saana, nmejicommand kuazimisha hela ni chini ya 50k. Sitoi zaidi ya hapo
 
Ila Tala wanajua kudai.
Nilikuwa natumiwa message mpaka ikawa kero.
Halafu hela yenyewe sipati.
Nililipa bila kupenda
 
Dah pole sana dada ake

sema nini embu Fanya nipate 450k kwanza

Bora tukopeshane wanyumbani tu

Nyumbani natoka saa 11alfajiri narudi SAA sita usiku; Mzee mwenye nyumba kanikalia vibaya.
Hahahah kizembe tu namna hio🤣🤣🤣 af jana nipo kwenye basi jamaa anamwambia mwenzie mbona huyo hana shida. Pokea simu tu unamtia sound anakaa vizuri maisha yanaendelea..Mi nadaiwa sana ila siachagi kuwapokelea simu!
 
Tz hii wamiliki wa hivi vikampuni uchwara 95% ni matapeli sana,atadhulumu stahiki za wafanyakazi wake akitoka hapo atadhulumu suppliers wake mara atakopea asset 1 kwny bank 3 tofauti tofauti kwa kweli ni changamoto sana.
Mkuu umeongea exactly uhalisia ulivyo.Hiv vikampun uchwara aisee ni pasua vibaya mnoo
 
Ungana na mwanahamisi singano

Anasimulia
Ushawahi kutapeliwa? Mimi nimetapeliwa Tsh milioni kumi (10m) na rafiki yangu wa karibu, (best friend) rafiki ambaye mpaka familia zinajuana. Ila 10m ikafanya urafiki, ushoga na udugu ukafa moja kwa moja. Ilikuwa hivi, Shoga alinunua gari ya kubeba mafuta na kuanza biashara.

Biashara yake ni kununua mafuta depo na kusambaza. Akaniomba niwekeze kwenye biashara yake mana ana upungufu wa pesa ya kuzungusha, tukakubaliana kila mwezi atanipa faida ya mtaji wangu 10% ambayo ni 1m. Na nikitaka pesa zangu nimpe notice ya mwezi 1. Nikaona ni jambo jema.

Badala ya kudunduliza kuweka akiba benki ngojea nimpe shoga, nami nipate tufaida. Nikampa 10m kash. Tulikubaliana tutaandikishana kwa lawyer ila makaratasi hayakuja. Mwezi wa kwanza nikatumiwa 1m fresh, mwezi wa pili mpaka nikakumbusha, nikatumiwa nusu nusu.

Nikaja kujua kuwa amechukua pesa kwa rafiki yetu mwingine kwa dizaini hiyo, ila sikumuuliza. Siku moja kwenye mazungumzo, akajisahau akasema sasa hana stress mana gari kawakodisha watengeneza barabara, yeye wanamlipa tu kwa kutumia gari yake. Nikamwambia, ni vema anirudishie pesa.

Hapo ndio shida ilipoanza, miezi kama minne hivi tunadaiana, nikashikwa na hasira nikamwambia ntampeleka polisi. Hamadiiii naletewa barua ya mwanasheria kuwa niache kumsumbua na kumtisha mteja wake. Jema ni kuwa barua ya mwanasheria wake ilikiri kuwa niwekeza hela kwa makubaliano.

Kiukweli nilipata ghadabu kubwa mno, nikapata mwanasheria akajibu barua. Swala likafika kwenye familia. Kaka yake akaahidi kuwa nitalipwa. Kutoka october 2018 mpaka leo sijalipwa hata mia. Na si kuwa hawana hela wana mashule ya nursery mpaka college, basi tu, dhulma.

Nikataka kufungua kesi, mama na baba Mishy wakanisomea risala ndefuuuuuuuuu. Nakumbuka mama aliniambia, kama familia yake wamemuacha rafiki yako akufanyie ubaya sisi wazazi wako hatukuruhusu umlipe mwenzio ubaya, ulinde uungwana wetu Samehe. Mungu akatajwa kama mara alfu...hapo.

Jana usiku, kuna mtu alikuwa analalamika katapeliwa kikombe (mug) na alikuwa determine kupata haki yake, ikanifanya nikumbuke madhila yangu, nikiri, kahoro bado kanauma - 10m parefu jamaniiii. Nikaona japo niandike kuwakumbusha msirudie kufanya ujinga niliofanya. Nimejifunza mnoo.

Asante
Nikikumbuka 1.5 M imeenda mdada kanitapeli akzima simu acheni tu Mungu yupo
 
Hii kitu huwa inaumiza sana, nadhani ni kwa sababu unakuwa umefanyiwa na mtu wa karibu unayemuamini sana!!!!

Mini jamaa ya ngu mmoja aliwahi nifata nimuazime ela, nyuma kidogo pia nilkishadulumiwa e;a so nilishasema mm kumpa mtu ela tena basi, ila mshikaji jinsi alivyokuja unamuangalia usoni mpaka unamuonea huruma alivyokuwa na shida nikasema poa **** mmama ofisini anakopesha wafanyakazi wenzie tu kwa riba ya 10% kwa mwezi na jamaa alisema ndani ya week mbili atakuwa amerudisha nikasema poa nikaenda kumchukulia ela.

Nilikaa mpaka ikafika karibu millioni 2 jamaa kila siku sound zinabadilika na mnbaya zaidi ni kipindi nilikuwa naelekea kwenye harusi yangu, so mwenyewe nahitaji ela kwa ajili ya kufanikishia harusi huku nadaiwa.
Nimemsamehe jamaa lakini sintomsahau kwa jinsi alivyonisurubisha maana ilibidi niilipe mimi!!
 
Ili neno 'What goes around comes around' linanipa nguvu sana kila napoikumbuka 250k yangu niliyomkopesha rafiki yangu na amegoma kunilipa.Nimeumia sana ukizingatia kipindi nampa hii hela nilikuwa naanza maisha ya kujitegemea,21yrs daah! Nilikuwa bado dogo sana.
 
Duh pole sana mkuu.
 
Bwashee, imesha-come around hadi sasa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom