Ushawahi kupigana, kuchokozwa? Chanzo ni nini?

fyddell

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
7,411
2,000
Haha nimecheka sana baada ya kusoma Visa vya wadau, ngoja nishee nami hiki kimoja. Niko na best friend wangu/ classmate wangu (may his soul rest in peace) mapumziko, kumbe alikuwa na ugomvi na vijana wa form two, sisi form one. Gafra jamaa wakaibuka tulipokuwa tunakula mihogo wakaanza kumzingua, kuona vile nikashindwa kumuacha mshkaji wangu akionewa wakati mi nipo. Nikachomoa kuni kwenye jiko la mihogo na kuanza kuwatembezea wale jamaa. Wakati napambana nao, kumbe mshkaji wangu alikuwa amekimbia pembeni na kuokota mawe na kuanza kuyarusha kwa wale washkaji nami nipo katikati yao. Ile nageuka tu, jiwe likatua juu ya jicho, damu zilizoruka pale sijawahi ona. Jamaa wote na mshkaji wangu wakakimbia, mimi kilio juu huku nimeshikilia pale nilipopigwa na jiwe, uniforms zote zimelowa damu.
Baada ya hapo sikuingilia tena ugomvi usionihusu
 
LaRosa

JF-Expert Member
Jul 3, 2020
685
1,000
Aliechezea simba ni Haruna shamte kwa sasa yupo Namungo na uyu kabla ya simba alikua Toto Africa ya mwanza. Shamte Ali wa yanga naona umechanganya majina tu kidog
Ni huyu huyu alikuja kuwa Mwanangu saana baadae! Nilicheza nae timu ya shule Nyakabungo Primary miaka hiyo baadae tulikuja kuwa washkaji saana sababu ya soka then Nikacheza nae soka Hadi Toto Africa kwa Teacher Bilo.

Seema tunaitana majina ya utani muda wote.. yeye nlikuwa namuita Ngobese ujanani utotoni nilikuwa namuita Kigo master. Maisha haya!
 
fyddell

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
7,411
2,000
Ni huyu huyu alikuja kuwa Mwanangu saana baadae! Nilicheza nae timu ya shule Nyakabungo Primary miaka hiyo baadae tulikuja kuwa washkaji saana sababu ya soka then Nikacheza nae soka Hadi Toto Africa kwa Teacher Bilo.

Seema tunaitana majina ya utani muda wote.. yeye nlikuwa namuita Ngobese ujanani utotoni nilikuwa namuita Kigo master. Maisha haya!
So now mko kwenye fani tofauti right?
 
Mohamedy cadinaly

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
2,109
2,000
Haya mambo yanatokea sana

Niwape kisa kimoja kilitokea kwangu

Ilikua ni siku moja ambapo jirani yetu mmoja aliua kuku wetu kisha akaja kumtupa nje getini kwa dharau kwamba ameua!

Nyumbani hawakuwepo hata mtu mmoja

Nikamuuliza kwanini kafanya hivyo akanijibu kwa hasira kwamba hata mm anaweza kuniua kama huyo kuku

Kipindi hicho nilikua na miaka 17 tu nilihisi hasira utadhani kuna kitu nilikua nimekula

Niliingia ndani nikitetemeka kwa hasira nikitafuta panga maana hasira zilinituma nimuue tu...sijui kwanini

Niliangaza macho sikuona panga....Nikakuta mpini wa jembe nikatoka nao nje nikamwambia sasa aniue sasa

Jamaa alivyoona nimechemka akaacha kufikiria kupigana na mimi badala yake akaanza kunitusi na mama yangu

Nilimvaa nikaanza kumpiga sana na ule mpini wa jembe nilimpiga shigoni akaanguka pale pale......Nikajua nishafanya mauaji..watu walianza kujaa pale nilihisi nimeshaua nikaingia nikafunga geti nikajichimbia ndani

Kumbe alikua hajafa alikuja kuzinduka pale akaanza kujaribu kuleta fujo watu wakamkamata, sasa kutokana na kuwa na rekodi mbaya na ule mtaa na kwa kua ni mtu wa kuja alipewa wiki tu awe amehama

Mwisho alikuja kuhama ila tukawa tukikutana hatuongei huku mitaa ya pili hadi alipofariki mwaka jana

Nina visa vingi sana nitashare humu...hebu tuambie kwako ilikuaje hadi ukapigana?
Kwahyo una miaka kumi na 18 sasa hv?
 
cocastic

JF-Expert Member
Nov 30, 2019
23,549
2,000
Haha nimecheka sana baada ya kusoma Visa vya wadau, ngoja nishee nami hiki kimoja. Niko na best friend wangu/ classmate wangu (may his soul rest in peace) mapumziko, kumbe alikuwa na ugomvi na vijana wa form two, sisi form one. Gafra jamaa wakaibuka tulipokuwa tunakula mihogo wakaanza kumzingua, kuona vile nikashindwa kumuacha mshkaji wangu akionewa wakati mi nipo. Nikachomoa kuni kwenye jiko la mihogo na kuanza kuwatembezea wale jamaa. Wakati napambana nao, kumbe mshkaji wangu alikuwa amekimbia pembeni na kuokota mawe na kuanza kuyarusha kwa wale washkaji nami nipo katikati yao. Ile nageuka tu, jiwe likatua juu ya jicho, damu zilizoruka pale sijawahi ona. Jamaa wote na mshkaji wangu wakakimbia, mimi kilio juu huku nimeshikilia pale nilipopigwa na jiwe, uniforms zote zimelowa damu.
Baada ya hapo sikuingilia tena ugomvi usionihusu
Poleeeh sana.
 
Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,913
2,000
Me nilipigana sana kupiga na kupigwa niliona kawaida

Ila kuna in charge wetu kiwandani nilipokua nafanya kazi alizidisha Ungese nilimpiga na ndoo kichwani tena zile ndoo nzito mpk nikatimuliwa kazi.
Enzi zangu nilishapigwa Sana na nilishawapiga sana
 
Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
9,365
2,000
Ugomvi sio mzuri
Kuna jamaa nilijifanya mtemi nimzingue jamaa akawa mpole tu watu wakaamulia

Sasa Leo nimepita sehemu nimemkuta jamaa huyo huyo anafundisha karate
 
Awuot

JF-Expert Member
Nov 10, 2018
1,170
2,000
Enzi za Tyson nikitoka kuangalia najiona mi ndo Tyson mwenyeweSiku natoka shule Niko drs la 3 lidada la drs 7 nilimkanyaga Banat mbaya

Weee alin NASA Kofi nikasema hunijui si nikajifanya mbabe

Alinigaragazaaa mchangani sitosahau.
Hahahahaaa!!!!!
 
Fernando Jr

JF-Expert Member
Jul 12, 2017
2,473
2,000
Haha nimecheka sana baada ya kusoma Visa vya wadau, ngoja nishee nami hiki kimoja. Niko na best friend wangu/ classmate wangu (may his soul rest in peace) mapumziko, kumbe alikuwa na ugomvi na vijana wa form two, sisi form one. Gafra jamaa wakaibuka tulipokuwa tunakula mihogo wakaanza kumzingua, kuona vile nikashindwa kumuacha mshkaji wangu akionewa wakati mi nipo. Nikachomoa kuni kwenye jiko la mihogo na kuanza kuwatembezea wale jamaa. Wakati napambana nao, kumbe mshkaji wangu alikuwa amekimbia pembeni na kuokota mawe na kuanza kuyarusha kwa wale washkaji nami nipo katikati yao. Ile nageuka tu, jiwe likatua juu ya jicho, damu zilizoruka pale sijawahi ona. Jamaa wote na mshkaji wangu wakakimbia, mimi kilio juu huku nimeshikilia pale nilipopigwa na jiwe, uniforms zote zimelowa damu.
Baada ya hapo sikuingilia tena ugomvi usionihusu
huyo jamaa yako ni zaidi ya Yuda Iskariote!

Yuda alimuuza Yesu akachukua chake akasepa. Jamaa kakugawa bure, kaona haitoshi kakutandika, kaona bado haitoshi kakukimbia
 
fyddell

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
7,411
2,000
huyo jamaa yako ni zaidi ya Yuda Iskariote!

Yuda alimuuza Yesu akachukua chake akasepa. Jamaa kakugawa bure, kaona haitoshi kakutandika, kaona bado haitoshi kakukimbia
Yaani dah 😂😂
Mi marehemu sasa hivi. Mungu ampe pumzisho zuri huko aliko
 
Gaddy Fazzy

Member
Jan 16, 2021
90
125
Nakumbuka wakati nipo kidato cha 6 , kishoju sec school huko Kagera, nilikuwa na ka mwili kadogodogo hivi sasa kwenye bweni letu nikaenda chumba jirani kuazima ndoo ya kuogea. Kwakuw nilikuta ndo ipo hainakazi na sioni kama kuna mtu ikabidi nichukue then nitairudisha maana ndo ulikiwa utaratibu. Basi bwana ile nimetembea hatua kadhaa nikasikia sauti nzito inaniambia "fanya haraka uirudishe" (lakini ilikuwa kwa dharau sana sio kibinadamu),kumbe alkuwa kalala dela la juu mm sikumuona. Haya bwana nikambwambia usihof nairudisha, mara jamaa akaendelea kunikoromea et usipoirudisha utaona (maana mm nilikuwa na mwili mdogo yeye alikuwa kajazia). Ahh namim nikajam nikafungua koki ya matusi, lakini hatukuzichapa. Ila nilibaki na hasira sana na nilijua jamaa simuwezi ila mpaka nitumie "Ambush" ambayo ndo teknik ninayoikubali sana maana huwa sishindwi nikitumia njia hii. Sasa nikavizia mida ya usiku nikaokota mpini wa fagio nikamkuta kalala nilimchapa sana bila kumpa nafasi hadi mpini ukavunjika kisha nikakimbia baada ya yeye kupiga makelele. Nilienda kulala bweni lingine lilikuwa linaitwa bweni la AZIMIO kwa kujificha. Kesho yake kumbe jamaa aliumia sana akapelekwa hospital,niliogopa sana nikawa sina amani nikajua sina shule tena. Ila nilipewa exile ya mwezi mzima na mwisho yaliisha , kumbe jamaa aliniheshimu sana tokea hapo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom