EWGM's
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,521
- 2,112
In a Serious Note Wandugu!!
Nadhani mmeona kichwa cha habari hapo juu.
Hivi ushawahi kukaa peke yako sehemu tulivu na kuanza kutafakari yaliyotokea na yanayoendelea kutokea kwenye nchi yetu ya Tanzania kuanzia miaka 15 nyuma, mwaka hadi mwaka na ukafikia muda wa kujiuliza hivi kwanini nimezaliwa Tanzania au nchi kama hii.
Napenda kutanguliza kuwa fikra hizo si kwasababu ya ugumu wa maisha au kuotokana na kukosa kujikimu hapana bali ni mwenendo mzima wa nchi na mazingira jinsi yalivyo pamoja na mfumo wa watu wanavyoishi. Nasema hivyo sababu nimepata fursa tangu nikiwa mdogo sana za kujionea na kutembelea na kuishi nchi nyingi duniani.
Kuacha na kuweka pembeni hofu, uhuru wa kuongea, kufanya jambo bila kificho au kuwa na wasiwasi, usalama wa afya na mali naweza kusema ni Uzalendo na mwenendo mzima wa nchi na watu wake ndiyo unaoleta fikra hizo. Kama mtakumbuka miaka ya nyuma Kali Ongala alikataa kubadili passport yake ili achezee timu ya Taifa.
Bahati nzuri watoto wangu wanaishi hapa lakini wanaishi kwa visa kuna wakati wananiuliza baba sisi ni watanzania huwa nashindwa niwajibu nini? Kuna wakati nakuwa nasema hivi nawekeza Tanzania kwanini wakati sitapenda watoto wangu waishi kwenye mazingira kama haya.
Nchi hii imekosa maadili, inchi imekosa mwelekeo, nchi hii haina ile misingi ya kuheshimu sheria na watu wenyewe kujiheshimu, wananchi wake wengi wako wa wako tu. Ukija kwenye elimu ndiyo balaa (hapa naongelea shule za kina kayumba). Kusema kweli kwa sasa nashindwa kjivunia kuwa mtanzania kama ilivyo miaka ya nyuma, naona kama nchi inatia aibu miaka inavyozidi kusonga mbele.
Hivyo swali langu kwako, hivi ushawahi kukaa kwa utulivu na kujiuliza kwanini umezaliwa Tanzania kwasababu nilizozitaja mimi hapo juu?