Ushawahi kujiuliza haya maswali?

Showio

JF-Expert Member
May 16, 2019
255
481
Kuna wakati unajiuliza “Mbona katika watu wote mimi ndio napitia CHANGAMOTO KUBWA kila siku?” Kuna mara nyingine unatamani kupata mapumziko kutoka katika mambo yanayokuandama. Likiisha moja linakuja lingine, na kabla haujatulia limeibuka na lingine.

Kuna wakati unashangaa mbona hata watu walionizidi na wako juu yangu kama wanakazana kunishusha chini na kunipiga vita. Unajiuliza mbona kama ANGUKO langu huwa linashangiliwa na wengi ambao hawafaidiki chochote hata kama nikianguka ama kufeli?

Mara nyingine unashindwa kuelewa:Inakuwaje VITA zako ni kubwa kila siku na haupumziki?Mbona ni kama vile watu wanasubiri MWANYA na UPENYO wa kunishambulia?

Jibu lake ni hili:UMEBEBA HATIMA KUBWA.UMEBEBA HATIMA ZA WATU WENGI.

Dunia haikuoni kama mtu mmoja,inakuona na maelfu ya watu walioko nyuma yako. Unapigana kwa ajili YAKO na kwa AJILI ya wote WALIO NYUMA YAKO.

Kuna watu wengi HATIMA yao iko kwenye USHINDI wako. Kuna watu umebeba MAFANIKIO ya FAMILIA,UKOO na wengine TAIFA zima.Kuna watu Mungu amewachagua kutangulia mbele ya wengine,inawezekana wewe ni mmoja wao.

UKIKATA TAMAA,UMEPOTEZA HATIMA ZA WENGI.Nakuombea MUNGU akupe NGUVU za KUSHINDA na KUVUKA katika unayopitia.

TUNASUBIRI USHINDI WAKO!
 
hizi changamoto nazopitia ndo mana jiwe amekuwa rais hlf me nmekuwa mpiga kura.
 
Amina, umesema vyema. Pia ukubwa wa ndoto zako ndiyo unatoa picha ya maadau au tabu na mateso ili kuiitimiza ( the big the vision , the big the problem your required to solve )
 
Amiin mkuu..maneno yenye faraja sana haya,yanatia nguvu,yanarudisha tumaini lililopotea..Siku zote dhahabu hupatikana kupitia tanuru la moto mkali..bila moto dhahabu ni mchanga tu,kinachoitofautisha dhahabu na mchanga ni tanuru la moto..
Mateso yako,taabu zako,changamoto zako,mateso yako,dharau kejeli na kukataliwa kwako tambua hivyo vyote vipo ili kukushape na kukufanya uwe bora zaidi ya ulivyo sasa.kamwe usikate tamaa maana giza likizidi ujue ndio kunakaribia kupambazuka..

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
 
Back
Top Bottom