Ushauri wenu unahitajika ili nisije kuharibu mahusiano yangu

Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
2,813
3,766
Habari za wakati huu wakubwa

Mie ni kijana wa kiume mwenye miaka 28, Mtoto wa Pili katika familia yetu ila Kaka (First born), Baba na Mama walishatangulia mbele za Haki, nipo na wadogo zangu wanne wanaoniangalia kama Baba na Mama kwao. Nakaa mkoa mmoja upo Kusini Nyanda za juu.

Nimekuja kwenu ndugu zangu watanzania kuomba ushauri. Nimechagua platform hii kwa sababu kuna mambo kadha wa kadha nilikutana nayo nikaomba ushauri kuna watu walinishauri vizuri wengine walikejeli kama ujuavyo binadamu hatuwezi kuwa sawa.

Changamoto hii ninayo inahusu mahusiano yangu.! Mimi mwaka jana niliachana na mwanamke ambaye nikimuoa kwa dini kabisa( Islam) ila kuna mambo hayakwenda sawa nikawa nimeamua kukubaliana na hali nikamrudisha binti wa watu kwao ili kuepuka Madhara mengine ambayo yangetokea kama ningekaa naye maana mwenzangu alikuwa vitabia sikuvipenda na hakuwa tayari kuacha tabia zake. Tabia hizo kipindi cha uchumba hazikuonekana kabisa ila baada tu ya kumuwekea pete kidoleni bibie akaota mapembe.

Baada ya muda huu toka mwezi February mwaka jana, nimekuwa nikipata changamoto ya mazoea ya kuwa na mwenza maana mwili nao unahitaji kutimiziwa hitaji lla nakuta sina mke tena. Imenisumbua sana. Lakini, Alhamdulillah, Mwezi wa 11 mwaka jana nikampata bibie mmoja nikampenda na nikaomba niwe naye kwenye mahusiano akakubali.

Hadi leo tunavyoongea, huyu bibie (23) sijaona shida yoyote kusema ukweli. Na hata hivyo suala la kumuoa nilimwambia akakubali ila akasema hadi amalize Chuo yupo mwaka wa pili chuoni Mzumbe anasomea Mambo ya Sheria.

Kulingana na hali ile Ndugu wamekuwa wakinisihi kuoa tena niachane na mambo ya kuwa bachelor maana Umri wangu umefika na pia nina wadogo zangu napaswa kuawaangalia hivyo napaswa kuwa na msimamo na familia ili niweze kuwaangalia wadogo zangu vizuri.

Sasa huyu bidada anaonekana anapenda sana sherehe, namaanisha yaani anataka nayeye siku moja awe kwenye shera, afanyiwe send off na sherehe zingine. Mwenzangu ni Mchaga mimi ni Mzigua ila sijakulia uziguani kwahiyo sijui kizigua hata najua kisukuma maana ndiko nimekulia.

Mie nataka kumuoa ila sitaki sherehe, sijui send off mara sijui Harusi mie hayo sitaki kiukweli maana sitaki kabisa kusikia habari ya Sherehe za harusi masikioni mwangu. Kitu ambacho nipo tayari ni kwenda kwao kujitambulisha nitoe mahali na kama kuna sherehe ndogo ya watu wasiozidi kumi sawa ila sio harusi ya watu sijui rundoooo .

Sasa natafuta namna ya kumuuliza mwezangu kama anakubaliana na hilo kwa namna ambayo asihisi natafuta gear ya kumuacha ili anielewe hitaji langu la kumuoa ila Bila harusi. Nampenda ila sitaki sherehe kabisa


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
1. Mwanasheria
2. Mchaga
3. Unamuogopa kumwambia ukweli means haujiamini.

IMG_20200407_142309.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifupi mchaga na sherehe huwezi kuwatenganisha maana inajulikana ndafu lazima aliwe, Halafu kingine mchaga halafu mwanasheria jiandae kisaikolojia kuna uwezekano ukapata pasua kichwa mwingine

Akiwa daktari, vipi hapo ?? Ni Mwanafunzi wa Udaktari Chuo kipo mbeya Rufaa..! Nimetumia ile taaluma ila yeye ni Mwanafunzi wa udaktari


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom