Naombeni ushauri wenu: Nimezama kwenye penzi la mwanajeshi

Pharm D

JF-Expert Member
Feb 17, 2017
1,230
2,938
First encounter: Alikuja mrembo mmoja ofsini kwangu na kwakua ulikuwa muda wa kukaribia kufunga, akawa mteja wangu wa mwisho kumhudumia kwa siku hyo. Baada tu ya kumhudumia nkajiwahisha kusign out ili nimuwah kabla hajafika mbali nimpe lifti nianze kuyajenga taratibu njiani. Hili lilifanikiwa kwa 100% nkampeleka mpaka kwao tukapeana contacts nikasepa zangu then tukaanza kuwasiliana kuanzia hapo.

Siku ya siku akaniambia huku mkoani ndio nyumbani kwa wazazi lakini yeye anaishi Dar ndiyo anafanya kazi huko (sikuwahi kumpeleleza anafanya kazi gani) hivyo likizo imeisha lakini kutokana na huduma aliyoipata siku ile pale ofisini kwangu ameona siyo vibaya akaniaga kabla hajaondoka.

Nikakubaliana na ombi lake ila nikajitia ugonjwa hivyo nko home nina E.D (mapumziko ya kiafya) hivyo kama hatojali aje tu home hakuna shida. Nikamuelekeza akafika nikamweleza kinachonisibu japo ilikuwa ni uongo mtupu, akatoa khanga kwenye handbag akaingia jikoni akakoroga uji wa mgonjwa.

Wanawake walivyo wadhaifu akaanza kunihurumia pale mara aniandalie uji aninyweshe kidogo tukaanza kuangaliana machoni huku zero distance nikaona hapahapa nikamshika kiuno yuko kimya nikamuegamiza kifuani kuanza kumtomasa mpaka akatoa kiss mara paaaaap mtu kaliwa tunda kimasihara.

Baada ya hapo hakuaga akavaa nguo zake akasepa kimyakimya hakutaka hata kusindikizwa. Tukachuniana kama baada ya wiki akawa amesharudi kazini kwake nikaanza kuona status zake WhatsApp akiwa na combart na SMG begani. Nkasapraizika lakini siku-comment chochote nkapita kimyakimya.

Nlipata safari ya kikaz Dar nikamtaarifu kwa meseji tu ya kawaida, “Habari za siku rafiki, niko njiani nakuja Dar kwa kazi ya kiofisi. Nitakuwepo kwa siku tatu. Kama ratiba yangu na yako zikiruhusu kusalimiana, naomba tufanye hivyo”

Msg sent and delivered but not replied...

Ile siku ya tatu jioni ili kesho yake nirudi mkoa ndiyo anapiga kunieleza alipo nimfuate, nikasogea mpaka maeneo ya jirani na kambi akaja tukakutana bar. Akalaumu kile kitendo (kuliwa tunda kimasihara) kilimkera na alitokea kunichukia ila ni kosa limeshapita, maisha mengine yaendelee. Hakutaka kuendeleza ule mchezo coz kwake mapenzi ni serious issue na hawezi kuingia kwenye mahusiano kwa bahati mbaya namna ile ingawa hana uhusiano na mtu kwa sasa ila hawezi kukurupuka. Baada ya kama dakika 15 au 20 hivi tukaagana kila mtu akasepa kivyake.

Kuanzia hapo tukaanza kuwasiliana upya kwa kasi ya ajabu, tunaongea na simu for hours. Imefika hatua anaomba emergency leave aje tu mkoa as friends; nikitoka tu kazini tunagandana ila kwangu hataki kufika lakini tunaweza kukaa bar tunaongea hadi saa 6-7 za usiku kwa siku za wiki na club hadi saa11 alfajir kwa siku za weekend. Tukitoka hapo nam-drop kwao then narudI kulala kwangu akiamka tu yuko na mImI ila swala la mapenzI ndio tunapotezeana.

Kutokana na ukaribu wa mawasiliano tulio nao, it's likely kwamba hana serious relationship na kama ipo labda atakuwa ni mume wa mtu ambaye hamkabi kihvyo ndiyo maana tunapiga video call mpaka tunapotelea usingizini.

Hoja yangu:

Hapa nimeshikilia button ya push-to-start; niki-press tu engine inawaka na safari ya mapenzi na 'mjeda' inaanza rasmi. Hofu yangu ni kwamba sina uzoefu wa kutosha na hawa watu, hata kwenye ukoo wetu hatuna mtu hata mmoja aliyewahi kuwa hata mgambo.

Kwa ambao mshawahi kuwa na uhusiano au mliopo kwenye mahusiano na hawa watu, huwa wana character gani kulingana na mienendo ya kazi zao achilia mbali zile tabia personal ambazo kila mtu ana za kwake. Nazungumzia general ambazo combat ladies wanashea in general.

Naombeni ushauri wenu mapema nisije nikajifunika shuka moja na nyoka nikakosa msaada.

tapatalk_1578369689262.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pharm D,

Mkuu, kwenye swala mapenzi usiangalie physical character ya MTU, yaani hata uwe baunsa gani Ila linapofika kwenye mapenzi utashangaa unaanza kuita baby! baby! tena wakati mwingine unawaza kweli kweli ukiona unamtafuta mtu halafu ha-respond!!

Point ni kwamba kila kitu kina muda wake ingawa ratiba za hao watu huwa hazieleweki lakini huyo mwanamke anakujali na anakupenda sema tu inaonekana anakuchukulia kama vile haupo tayar kuishi naye kwa kuwa yeye ni mjeda so ukitaka kukaa naye sawa muweke wazi kuwa kazi aliyonayo hainifanyi nishindwe kuanzisha familia na ww lakini Kumdanganya kuwa unampenda kumbe ww target ni kula papuchi na kusema mjomba utakuja kupigishwa squart mpaka ujinyeeee!!!!

Tena ni vyema ukaenda hata kwao ili kumfanya moyo wake uwe mwepesi, hakika ukionyesha kumjali bila kuangalia kazi yake utadumu naye na anaweza akawa mke wako.

Wish you GOODLUCK BRO!!



don't waste your time on lecturing me, this is 2020
 
Mkuu kwenye swala mapenzi usiangalie physical character ya MTU, yaani hata uwe baunsa gani Ila linapofika kwenye mapenzi utashangaa unaanza kuita baby! baby! tena wakati mwingine unawaza kweli kweli ukiona unamtafuta mtu halafu harespond!!

Point ni kwamba kila kitu kina muda wake ingawa ratiba za hao watu huwa hazieleweki lakini huyo mwanamke anakujali na anakupenda sema tu inaonekana anakuchukulia kama vile haupo tayar kuishi naye kwa kuwa yeye ni mjeda so ukitaka kukaa naye sawa muweke wazi kuwa kazi aliyonayo hainifanyi nishindwe kuanzisha familia na ww lakini Kumdanganya kuwa unampenda kumbe ww target ni kula papuchi na kusema mjomba utakuja kupigishwa squart mpaka ujinyeeee!!!!

Tena ni vyema ukaenda hata kwao ili kumfanya moyo wake uwe mwepesi, hakika ukionyesha kumjali bila kuangalia kazi yake utadumu naye na anaweza akawa mke wako.....

wish you GOODLUCK BRO!!



don't waste your time on lecturing me, this is 2020
Asante mkuu kwa ushauri haya mambo hayahitaji ujuaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shairi hili niliandika mwaka 2017,Tarehe mbili ya mwezi December

NAMPENDA MWANAJESHI

Mzuri anapendeza, sura ye yanivutia
nawaza kama ntaweza, ukweli kumuambia
naota anikimbiza, bunduki anashikia
Ukweli bora eleza, akili yaniambia
nampenda mwanajeshi, naogopa mtongoza

Mtani anapopita, magwanda kajivalia
moyo wangu unasita, hata kumsogelea
mtoto kwanza sa sita, ndo kwanza imewadia
Kweli nitafurukuta, kama akinkubalia
nampenda mwanajeshi, naogopa mtongoza.

Anayo njema heshima, maadili anajua
nawaza nseme mapema,tatizo pakuanzia
mpaka ninapata homa, kila nikifikiria
kichwa nacho kinauma, ninazidi kuumia
nampenda mwanajeshi, naogopa mtongoza.

Anapigiwa saluti, heshima wamtolea
siwazi kumsaliti, siku nikija muoa
hata wavaao suti, bado wanamkimbia
nyororo yake sauti, pindi anapoongea
nampenda mwanajeshi, naogopa mtongoza.

Endesha dege la jeshi, angani ajipaia
uso kama muhabeshi, Arusha twakutania
mwongeaji na mcheshi, napenda kumtania
ila shida mwanajeshi, bastola ajibebea
nampenda mwanajeshi, naogopa mtongoza.

Amanitume rafiki, aende muelezea
naogopa unafiki ataweza kuzengea
ili niepushe chuki, labda tajikakamua
sitaki moyo wa dhiki, mapenzi kuyakimbia
nampenda mwanajeshi, naogopa mtongoza.


SHAIRI-Nampenda mwanajeshi
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Mkuu huyo ndio mkeo sasa!! mimi Kilwa94 nikiwa kama mzoefu, nakwambia huyo mjeshi weka ndani kwa maelezo yako ulivyoeleza ni dhahiri kuwa huyo ni wife material.

Kama haupo serious kuchukua jiko niuzie mazero saba yake(namba)

5/5
Mzee baba huyu baada ya kuliwa kimasihara dizain kama anahitaji kuwekewa commitment ndio maisha yawe hvyo ila ntamchagulia fungu jema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unataka kumuoa muoe ili ummiliki 100%, ila kama unataka kumchezea itakula kwako. Kuwa makini.

Usisikilize maneno ya watu kuwa wajeda wote ni malaya sio kweli. Ninawafahamu wajeda wengi wanaojiheshimu kuliko hata sisi raia.

Ushauri: Oa mkuu kama ame-meet vigezo vyako, achana na majungu ya watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni mtu poa sana sema hatabiriki ana mambo ya kushtukiza sana japo hatujawahi kukwazana kwa hilo na pia ni muelewa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika pitapita zangu nishadate na wajeda watatu mmoja MP nilimla kimasihara pale Kimbiji, ukweli hawatabiliki kabisa. Na mmoja nilitamani kuoa kabisa lakini hao watu aiae ni shida sijajua wa kwako cheo chake lakini ukweli waliopita jeshi watakwambia ukweli, raia ukioa mjenda aise ina changamoto zake hao wanawezana wenyewe kwa wenyewe
Kahamishwa kituo kawaida tu! Kwenda kozi kawaida na huko kiujinga ujinga utapigiwa bila hata yeye kupenda!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika pitapita zangu nishadate na wajeda watatu mmoja MP nilimla kimasihara pale Kimbiji, ukweli hawatabiliki kabisa. Na mmoja nilitamani kuoa kabisa lakini hao watu aiae ni shida sijajua wa kwako cheo chake lakini ukweli waliopita jeshi watakwambia ukweli, raia ukioa mjenda aise ina changamoto zake hao wanawezana wenyewe kwa wenyewe
Kahamishwa kituo kawaida tu! Kwenda kozi kawaida na huko kiujinga ujinga utapigiwa bila hata yeye kupenda!

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahih kabisa anytime anything can happen yaan unatakiwa kukaa kimachale
Kuna siku tunaongea kwenye simu nlikua kazin huo muda tunapiga tu story za kawaida ghafla naitwa naambiwa nina mgen wng nje natoka namkuta niyeye
Wakat huo kwenye maongez anadai yuko guard kumbe alikua njian ananifuata nilipo...
Wako poa sana ila hawatak ubabaishaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom