Papaa Kinyani
JF-Expert Member
- Feb 25, 2013
- 1,459
- 697
Nenda kasomeee "ukamataji wa dhahabu" inalipa sanaHabari.mimi ni kijana wa kawaida nimemaliza form 4 miaka zaidi ya 7 huko nyuma,nimetanua weeee mtaani,ila sasa nimeona nijiendeleze kielimu lakini watu walionizunguka naona hawafiti kunishauri ndyo maana nimeona nije hapa.
Cheti changu kipo kama ifuatavyo.
MATH-F
HISTORY-D
ENGLISH-D
KISW-C
BIOS-C
CHEMIS-D
CIVICS-D
GEOG-C
Sasa hapa nilitaka nikasome afya lakini jamaa wananismbia nina mkia wa hesabu siwezi kuendele,wakuu nishaurini nikaongeze elimu,kwa kada ipi wakuu elimu muhimu japo sio lazima,mimi nimeona ni muhimu nikasome.
Nilikuwa nasoma dini ili watu kama kina kiranga na wana falsafa wengine wasiniyumbishe mana ukienda mtupu huko vyuoni mara unarudi kama kiranga,sasa nipo fiti nataka kusoma elimu dunis wakuu.
Ushauri wenu wadau mbali mbali humu akiwemo mams yangu mpeeeeeenzi FaizaFoxy na wengineo.
Na vipi suala la kurudia form four tenaa likoje,taratibu faida na hasara zake?
Asanteni nategemea majibu kutoka kwenu wasomi mbali mbali wa humu.
Sent using Jamii Forums mobile app