Ushauri wenu ni muhimu sana kwangu

Ba Bii

JF-Expert Member
Jan 22, 2018
204
160
Nimepata kazi ya "UALIMU" katika hizi ajira ambazo zimetoka juzi. Lakini wakati naomba hii ajira ya Ualimu sikuwa na kazi.

Ila katika kipindi hiki cha kusubiria ajira ya Ualimu nimepata kazi nyingine ya UHASIBU katika moja ya taasisi kubwa sana hapa Tz ya mtu binafsi ambayo pia ni fani yangu na mshahara wake ni 1.5mil.

Nimepewa mkataba wa miezi 6 kwa kuanzia then baadae nitapewa mwingine na mshahara utaongezeka baada ya Probation kuisha.

Je, niache hii kazi niende kufundisha au niendelee na kazi yangu hii ninayofaifanya?

Nisaidie ushauri wenu?
 
Mkuu kama malengo yako ni kuajiriwa forever nenda kufundishe.
But ukinamalengo ya kuja kuwekeza kwenye issue zingine badae piga hiyo kazi ya uhasibu
Nina malengo makubwa sana na ninachotaka ni capital nifanye mambo yangu binafsi baadae kidogo
 
Nina malengo makubwa sana na ninachotaka ni capital nifanye mambo yangu binafsi baadae kidogo
Kama tayari unalijua hili ndiyo upambane sasa ili kufikia lengo, hiyo capital unayoitaka kwa hiyo plan b unayotaka uiendee walaqhi' utasota sana mpaka ufikishe kiasi unachotaka, na kwanza mpaka unastaafu unaweza usiwe umekifikisha hata, baki uliko!
 
Kama tayari unalijua hili ndiyo upambane sasa ili kufikia lengo, hiyo capital unayoitaka kwa hiyo plan b unayotaka uiendee walaqhi' utasota sana mpaka ufikishe kiasi unachotaka, na kwanza mpaka unastaafu unaweza usiwe umekifikisha hata, baki uliko..!
Thanks in deed.
 
Mshirikishe Mungu atakupa jibu, kwa haraka huko uliko Sasa Ni green pasture Sana ila at when it will ends.
 
Bado naendelea kuwashukuru sana kwa shauri zenu. Ni nzuri sana sana na zinanifariji kwa kiasi kikubwa sana
 
Mshirikishe Mungu atakupa jibu, kwa haraka huko uliko Sasa Ni green pasture Sana ila at when it will ends.
Kazi hii ipo zaidi ya miaka 70 iliyopita na bado inaendelea kwa maana sio ya kuisha leo wala kesho...!
 
Piga chini hiyo kazi ya binafsi ,nenda serikalin karipoti Fanya kazi mwaka mmoja ingia benki chukua mkopo wekeza kwenye unachoona kitakufaaa .kazi za private zina stress sanaaa inaweza isha kesho na pia unatumika sanaa.

serikalin raha yake kama una akili mda upo wa kufanya mambo yako tena kazi yenyewe ualimu ni rahisi sanaa unashika somo lako unafundisha miaka yote hilo hilo inafika mda unakuwa kama unaimba pambiao tu maana hutumii nguvu kufundisha ,kutunga mitihan na kujua vijana wako ufanye vipi wafaulu

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
NENDA KAWE MWALIMU KIJANA NARUDIA TENA PRIVATE HAWATABILIKI HAO ,...Nenda kapate ajila ya kudumu utakuja kujuta mpaka unakufa dadek...
 
Niunganishe mimi hapa kwenye uhasibu mkuu nikasake mchongo mapema
Wewe nenda ualimu nitakugawia kidogo kidogo
 
NENDA KAWE MWALIMU KIJANA NARUDIA TENA PRIVATE HAWATABILIKI HAO ,...Nenda kapate ajila ya kudumu utakuja kujuta mpaka unakufa dadek...
Duh! Napata shida sana kuacha mshahara wa 1.5 mil kwa mwezi na kwenda kupokea 500 kwa mwezi.
 
Ukiona kitu hakina changamoto ujue hakilipi... Ualimu ni kazi ya kimaskini na ya kinyonge nenda kawe mhasibu experience tu ya mwaka mmoja ya uhasibu ni mtaji kuliko kiinua mgongo cha mwalimu. Kama ukienda kwenye ualimu kubali utaiona hela ya maana siku ya kupokea kiinua mgongo.
 
Bado naendelea kuwashukuru sana kwa shauri zenu. Ni nzuri sana sana na zinanifariji kwa kiasi kikubwa sana
Kuna thread yangu naomba ushauri namna ya kurudisha check No serikalini nilisomea Engineering nikasema Mimi lazima Niwe tajiri kutoka familia masikini nikakataa ajira ya ualimu mwaka 2016, nikafanya kazi kwenye taasisi binafsi zinazolipa vizuri, nikajenga na nyumba freshi kumbe nilitakiwa niwekeze hata kwenye biashara Mimi sikufanya hivyo mkataba ukaisha life likanipiga kisawasawa.
Zilipotoka ajira hizi ikabidi nirudi kuomba tena na jina limetoka hapa siangalii nyuma naenda kuripoti nikapambane kurudisha check No.
Pamoja na engineering yangu nimeona bora nikawe MWALIMU tu na maisha yaendelee.
Kazi za binafsi zina changamoto sana zipo results oriented ukizingua tu huna kazi,majungu baina ya wafanyakazi nayo ni shida private wakiona unapiga hela tu utachongewa kwa boss utimuliwe.
Hapo Ni sawa na kutema big g kwa karanga za kuonjeshwa.
Fanya maamuzi usije kujutia.
Nimekushauri kutokana na yaliyonikuta.


 

Similar Discussions

Back
Top Bottom