Ushauri wenu: Kuna umuhimu kuridhisha wakwe wa siku hizi?

kilomita

Senior Member
Sep 11, 2011
100
210
Salam sana, naandika hapa nikiwa sina ujuzi wowote wa kiuandishi, kwenye makosa mtanisamehe. Ninachotaka kuelezea hapa na kuomba ushauri wenu ni experience yangu binafsi ambayo nadhani sijapata mtu sahihi bado wa kuongea nae vizuri akanielewa.

Mimi ni kijana fulani wa makamo, katika miaka ya thelathini ya mwanzo, na nina ndoa ya miaka mitano(5) sasa, namshukuru Mungu sana kwa baraka tele za watoto pia.

Naomba nielezee background vizuri ili kujaribu kujenga picha halisi iliyopo na kinachonisibu hasaa ingawa maisha yanasonga vizuri tu!

Mwaka 2010 nikiwa masomoni nchi fulani barani Asia, nilikutana na mrembo wa kichaga ambae kwakweli nilipomuona tu niliona mke hapohapo (Hii kitu sijawahi kujua imekaaje lakini ndo ilikuwa hivo na watu niliokuwa nao niliwaambia pengine walichukulia maneno tu!).

Baada ya kuonana nae uzuri yalikuwa ni mazingira ambayo ilikuwa rahisi kupata namba yake na kuanzisha nae mawasiliano, wote tukiwa mji mmoja lakini umbali wa takribani km25 tu. Alinichatisha kwa muda(tofauti na wanawake wengi wa age na mazingira tuliyokuwepo ambao pengine ingekuwa rahisi kuwapata) alipojiridhisha sikuwa na mahusiano mengine na baada ya kumuimpress hivi na vile basi alinikubalia. Kiukweli tulipendana sana, mimi nilikuwa mjanja janja tayari zaidi yake, so vitu vingi nilifanya nae vilikuwa vigeni kwake.

Kama ni bata tulikula sana, maholiday ya wiki2-4 tulienda sana, nilimtunza sana(pocket money yangu ilikuwa nzurinzuri zaidi) na yeye alinitunza sana (niliumwa kipindi flani masomoni na yeye alikaa na mimi vizuri sana). Baada ya miaka mitatu yeye akawa amemaliza masomo, akarudi Tanzania na mimi nikabakia kwa mwaka mwingine mmoja pia nikamaliza na kurudi nyumbani.

Kipindi chote ambacho yeye yupo Tz tulikuwa tunawasiliana almost kila siku na ndipo mipango ya ndoa ilipoanza kusukwa taratibu baina yetu, kwamba nikimaliza chuo nikae mwaka mmoja halafu ndoa. Kweli mtu mzima hivo ndio ilivokuwa, baada ya kurudi 2014, basi 2015 June, exactly 1year baada ya kurudi tukafunga ndoa baada ya kufata taratibu zote za kimila na kikanisa.

Hiyo story yote ni kuonyesha vile tulikutana na sisi wawili kupendana na kuchaguana, na kuona kila mmoja anamuhitaji mwenzie. Ilikuwa sisi kama sisi, sikumpendea familia yake na yeye naamini alinipenda mimi kama mimi maana hakunijua kwetu na sikujua kwao akati tunaanza kupendana na kuzama hivo.

Wakati tunaoana, nilikuwa nimefanya kazi mahali kama miezi 9 nikaacha kipindi karibu na ndoa lakini sikuwaza sana kuhusu kipato maana nilikuwa najiamini siwezi kukosa cha kufanya mjini hapa, pia backup ya mzee ilikuwa fiti na nyumba nikapewa kubwakubwa tu maeneo ya sinza sema ikawa kubwa kuliko mahitaji ya wakati ule tulipokuwa tunaanza, so tukapangisha na sisi tukapanga nyumba iliyotupendeza sote wawili nje kidogo ya mji. Maisha yalianza vizuri kabisa, tukaanza kupata baraka za watoto na mimi nikaanzisha biashara yangu tofauti na elimu yangu ambayo kwakweli kimekuwa hakiniangushi kwa miaka mi4-5 sasa.

Hiki kisa kinaanza tupo karibia mwaka wa 3 ndani ya ndoa na watoto wawili, pale ambapo mke wangu alienda kwao kusalimia na kushauriwa na mama na baba yake kwamba tuachane na nyumba za kupanga kuna nyumba wameanza kujenga kama vp niunganishe nguvu iishe tujiweke hapo kwa miaka kadhaa wakati tunajenga yetu taratibu. Mimi nilikataa kabisa wazo hilo lakini wazazi wa mke wangu walimforce sana mke wangu kiasi cha kumpigia simu za kwamba wanasikilizia majibu na kumbeba kumpeleka site aje anionyeshe.

Baada ya kukataa kabisa, mke wangu akaanza kuwa kama mbogo kodi ilivokuwa inakaribia kuisha, anakataa nisilipe ingine eti hiyo kodi (milioni6 kwa mwaka) bora nikaiweke kwenye hiyo nyumba inayojengwa iishe faster tuhamie. Nikakataa sana, akaja na style mpya, kwamba kodi ikiisha ni heri tukakae kwenye nyumba yetu ya sinza au hata kwa wazazi wangu hadi tutakapojenga yetu ila kodi ni kubwa sana nisilipe kokote. Lakini kumbuka kodi haikuwa kuwa tatizo kwangu.

Baada ya mvutano saana nikaona isiwe tabu, nikaanza kushiriki ujenzi wa hiyo nyumba. Nikawa nafanya hiki, wao(mama na baba mkwe) wanafanya kile. Nikaongeza kodi kwangu kama miezi miwili hivi ili tumalizie hiyo nyumba ambayo pia ilikuwa walking distance na nyumbani kwa wazazi wake.

Katikati ya ujenzi kuna muda unakuta labda inabidi nikanunue alluminium windows, nimepata quotation nshajua gharama labda nimelipia sehemu ya pesa, nikiwa natafuta ingine baba mkwe anaanza kunisumbua nimwambie baba yangu anisaidie atoe hela, kuna wakati alikuwa anataja hadi amount "mwambie akupe kama milion10-15 utamrudishia na kodi ya sinza", na baadae anakupigia kuulizia kama umemwambia na amesemaje!! Imagine, mimi sikutaka kuwaingiza wazazi wangu kwenye hiyo ishu kabisa, nilipambana mwenyewe na nilichoweza kufanya nilifanya lakini kama kulikuwa na nguvu sana upande wa pili kutaka familia yangu ishiriki wakati nyumba ni yao.

Nyumba iliisha kiaina na tukahamia, hadi inaisha mimi binafsi nilikuwa nimetumia kama mil12, ambayo kwakweli mimi nilichokuwa nawaza kichwani mwangu ni kwamba nimecover kodi ya 2-3years at once, nikae hiyo miaka huku najenga kwangu bila pressure nihame. Lakini sikuwa nimefurahia sana zile pressure zilizokuwa naekewa na wakwe sema nikamezea tu!

Baada ya kukaa miezi kadhaa nikaanza kuona dalili zisizokuwa nzuri za wakwe kuja home anytym bila taarifa yoyote maana actually ni kwao. Baada ya takriban miezi 6 tokea tuhamie, nilisafiri na mke na watoto kama kwa siku5 hivi, gari ikanilazimu kuegesha kwa usalama akati hatupo maana tulikuwa tunaishi karibu. Siku tuliyorudi, tulifika nyumbani vizuri tu mida ya saa 1 hivi tukiwa tumechoka tukakuta nyumba saafi imesafishwa hadi master bedroom hali tofauti na tuliyokuwa tumeacha, nikajua tu ni mama mkwe na dada zake wa kazi, nikashangaa sema nikauchuna. baada ya kuoga nikasema nitoke nikachukue gari pale ukweni niende zangu misele kidogo kufatilia hela flani kwa jamaa na bia kadhaa 2-3 tu zingehusika pia (ni mnywaji tu kidogo, sio mlevi na bangi natumia ile safi tu, mke wangu ananielewa tokea siku ya kwanza tunaonana, tena nimepunguza sana baada ya kuoa).

Sasa picha linaanza saa 2 hivi nimeenda kufata gari niende kwenye mitikasi yangu, nakutana na mama mkwe na shemeji ambae ni mdogo kwangu kama 2years tu wamekaa kibaraza cha nyuma kama wanaongea. Nikafika nikasalimia, nikajibiwa na mama mkwe kwamba "nilidhani ungeondoka bila kusalimia, unaenda wapi usiku huu? embu rudi nyumbani haraka ukakae na familia yako, umefika tu safari hata hujala kiguu na njia", nikaona duuh nikamjibu "kwanza mama nimekuta nyumba imedekiwa hadi master bedroom kwa mpango upi mbona maagizo hayo hatujaacha?", nikajibiwa "Una masterbedroom wewe??" duuuh nikamjibu "Daah kisa nakaa kwenu ndo unadhani unaweza kuniongelesha hivo eti nirudi nyumbani haraka?" dogo nae akanunua ugomvi akaanza kunifukuza kwao nisimjibu mama yake vile, mimi nikatoka nikaendelea na ratiba yangu kama nilivopanga tena ndo nikalewa vibaya mno nikaona siwezi kunyanyaswa kijinga nikavimba nilivorudi asubuhi yake nikataka watoto na mke wote watoke kwenye ile nyumba nikapeleka kwa wazazi wangu kwa wiki 1 nikatafuta nyumba ingine ya kupanga tukahamia. Nikaapa sitakanyaga kwenye ile nyumba au nyumbani kwao nilipofukuzwa usiku ule tena!!

Issue ikawa ndo hivo, kesho yake maneno yakawa mengi sanaaa, kutoka upande wao na kutoka kwangu binafsi niliongea saana kuhusu wao kutaka tu kunitumia kujenga na mengi tu, nikatamka maneno mabaya sana kwa mke wangu kuhusu wazazi wake na yeye akawakingia kifua sana, baada ya kama miezi 6 wale wazee wakajiskia kulipa kiasi walichokuwa wamejiskia kurudisha maana haikuwa hata karibu ya nilichotumia na nyumba sitaki hata kuiona hata sijui kama wamepangisha au inatumikaje.

Yale maneno nilikuwa naongea juu ya wazazi wa mke wangu yalimuumiza pia sana mke wangu na kufanya nyumba ishake, mimi mwenyewe hata hamu nae nikawa sina namuona msaliti tuu maana yeye alinipandia sana kichwani wakati wa kujenga halafu hiyohiyo nyumba imekuja kuwa tatizo kwenye familia yetu. Hii kitu ilitusumbua sana kwakweli lakini sababu naamini tunapendana tuliiweka nyuma na sisi tukaendelea na maisha yetu lakini ndo mimi ukweni sitaki hata kupasikia huu ni mwaka wa pili sasa.

Kuna kipindi mke wangu alijifungua mtoto mwingine hapa kati nikaonana na mama mkwe hospitali hata kumwangalia siwezi (sio namuogopa, ila ni chuki kali aisee naona nilinyanyaswa nae). Maana kama ananichukia kisa kunywa bia na kuvuta hizo mara moja moja ambazo mke wangu anaelewa na tunaishi vizuri tu kweli kuna sababu ya kumridhishwa mkwe? Au kama ananichukia kisa sina kazi nzuri, mbona mwanae hafanyi kazi mwaka wa 4 huu, ni mimi nacover kwa KILA KITU kwa hii hii mishe yangu ninayofanya ambayo pengine yeye anaidharau?

Mimi binafsi niliamua kuwafuta tu akilini mwangu niishi na mke wangu na watoto wangu, mwaka wa pili huu nimepotezea na tuko vizuri hatugombani kijingajinga labda mimi nizingue kama kawaida yetu wanaume. Mwaka mpya kuingia 2020 baba mkwe alinicheck kwamba kachinja nyama niende na familia yote tukachome tule tusahau yaliyopita yasiongelewe kabisa, mimi nilichofanya nilipeleka familia yote bila mimi.

Hapo niko sawa kwa nilichochagua kufanya hadi sasa?
Poleni sana kwa maneno meengi lakini nahisi nimeelezea nilivotaka kueleza! Ila ndoa za sikuhizi zinachance kubwa sana ya kuharibiwa na wazazi kuliko zile za zamani, hii kitu mtu ameolewa ila kila asubuhi, mchana na jioni anaongea tu na mama yake kilakitu sio poaaa! Mjifunze wadada!
 
Ulikosea kujiingiza kwenye mtego wa kuchangia kujenga ukweni,hapo ulitumika kwa maslaha yao tu,ila sio mbaya fanya kama umetoa sadaka tu,

Nakuunga mkono kuhusu wewe kutokwenda huko ukweni,huo ndio uanaume lazima ujiamini,hakuna mtu anayependa dharau juu yake,

Kuhusu watoto,usiwanyime haki yao ya kumtembelea Bibi na Babu yao na wajomba,ila wewe usikanyage huko,hapo heshima itarudi tu na wataona kua una msimamo na unajiamini,

Hao wakwe wasifikiri kua kujengewa/kujenga hiyo Nyumba basi ndio maisha wameshayapatia tayari,Dunia inazunguka,ipo siku watakuja kujuta kwa waliyokufanyia,Time will tell.

Pole sana Mkuu.
 
Kujipendekeza kote ukwenu huko lkn bado huna thamani,hapo utakuta hata mama yako mzazi hujawahi kumnunulia hata doti moja ya kanga,ila ukweni ushatoa million 12 na matusi ju.

Mimi ningewachana live na binti yao ningemwambia achague kati yangu mimi au wazazi .

Yaani mie kitu cha kwanza kabisa nitakachomwambia wife to be ni fungu linaloenda home kwa bi mkubwa ni hili na hapo hamna mjadala.

Ikitokea mtafaruku kati yako na bi mkubwa na inabidi nichague ujue ni wewe ndio utakae fungasha vilago.....papuchi zipo kibao.

Ni ujinga kwenda kunufaisha watu baki wakati wazazi waliokulea na kukuandaa mpaka huyo mlimbwende amwkubali kuolewa na wewe unawaacha hoi....watu wa namna hiyo siwaelewagi kabisa.
 
Tatizo umeona mwanamke ukaona huyu ni mke halo halo, bila hata kujiridhisha familia yake ikoje.

Kuoa si habari ya watu wawili tu, ni muunganiko wa familia mbili.

Jenga chako ukae kwako, jenga heshima watu wasije kukupigia deki bila taarifa mpaka master bedroom.

Isije kuwa mara paap, Mama mkwe anapiga deki chumbani kwako, anakutana na vipisi vya yale masuala yetu.
 
Back
Top Bottom