Biashara ya Kuuza Nyama (Butcher's Shop): Mambo Mbalimbali ya Kujifunza

Second Lieutenant

Senior Member
Jan 13, 2014
143
26
2377177_Meat.jpg

Habari za Mchana wana JF,

Ndugu yenu hapa naomba info kuhusu biashara ya Nyama (Burchery), Bei wanazonunua Machinjioni inakuwa kiasi gani? wangapi wamefanikiwa through this business.


WADAU WENGINE NAOHITAJI MUONGOZO WA BIASHARA HII
Nataka kufunga baadhi ya biashara nilizo nazo kwa sababu zimekuwa zikijiendesha kihasara kwa mda Sasa, nikafikiria kuanza biashara ya nyama.

Nafikiria kujenga mabucha ya kisasa, natafta eneo najenga zizi kwa ajili ya kuhifadhia ng'ombe ambao nitaajiri watu wa kwenda kununua mnadani na watahifadhiwa humo kabla ya kuchinjwa, nataka nianze na ng'ombe zaidi ya 60 kwa kuanzia.

Then ng'ombe watakaochinjwa watapelekwa kwenye mabucha yangu na pia nitakuwa nachakata nyama kwa ajili ya kusambaza kwenye masupermarket.. japo bado sijajua kiundani soko na changamoto ya biashara hii, naombeni wajuzi wa biashara hizi mnifahamishe na mkoa gani ambao biashara hii inafanyika vizuri zaidi.

Napenda kujua pia Kama biashara hii itanilipa,

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari zenu wadau, kwa wajuzi na wataalam wa biashara ya bucha naombeni kujuzwa bei ya vifaa vifuatavyo.

1. Mashine ya kisasa ya kukatia nyama
2. Vyuma vya kuning'inizia nyama
3. Mizani ya kisasa
4. Freezer kubwa

Kama kutakuwa na vifaa vingine vinavyohitajika naomba mnijuze na gharama zake nataka nianze rasmi mwakani hii biashara.

Naombeni ushirikiano wenu
Wakuu, ni vitu gani vya kuzingatia katika kufungua biashara ya Bucha ya Nyama ya Ng'ombe, Kuku na Samaki?

Msaada mwenye ufahamu na changamoto zake!

Wasalaam,

SH
Habari wadau. Ninaomba ushauri juu ya kuanzisha biashara ya nyama ya ng'ombe kwa kuuza katika mabucha ya kisasa. Hii ninamaanisha kuwa nitakuwa nakata nyama kitaalamu kwa visu au misumeno maalumu ya kukatia nyama, kupaki katika vifurushi vidogo na kuuza katika bucha nitakayoitengeza pamoja na kusambaza kwa wateja.

Nyama itazingatia masuala yote muhimu kiafya pamoja na kuitengeneza katika kiwango cha kuvutia.

Sasa ninaomba mnisaidie kunifahamisha gharama za visu hivi maalumu kwa kukatia nyama hiyo, mafriji ya kuhifadhia nyama isiharibike, mizani ya kisasa pamoja na mtaji wa kuanzia.

Biashara hii nataka niifanyie mbeya japo hakuna machinjio ya kisasa kama iliyopo pale dodoma lakini naamini kwa kutumia machinjio iliyopo naweza kuwapata nyama nzuri.


MICHANGO NA MIONGOZO
Umuhimu wa packaging
Mkuu hiyo biashara ni nzuri sana tatizo linokuja kudhoofisha biashara ni suala la Packing ya nyama

Changamoto kubwa hiko hapo bado wa Tz hatuwezi ku design parking nzuri ya product kama ya nyama ndio maana katika Supermarket zetu wanauza sana nyama ya nje kwasababu inakidhi viwango vya kimataifa

Ushauri wangu

1. Jenga banda sehemu yenye ardhi ya kutosha ambayo pia kuwe na Majani ya kutosha (ranch kidogo hivi unakipiga na fensi)

2. Jenga Machinjio madogo ya kisasa

3. Tafuta alternative source of energy usitegemee umeme wa tanesco kwa sababu bucha za kisasa zinatumia mashine kukatia nyama na sio vigogo na hizo mashine zinatumia umeme kwaiyo ukitegemea umeme wa Tanesco unaweza ukakaa siku bila kufanya kazi

4. Kuhusu Packing nenda TFDA kuna wataalam watakupa ushauri wa jinsi gani unaweza kufanya parking ya International standard

5. Usikope hela bank kwaajili ya kuanzisha biashara hii inaweza ikakugharimu biashara ikawa ngumu mwanzoni alafu jamaa wakaanza kukuchachamalia mwishowe ukamwaga manyanga

6. Fanya Study tour nakushauri nenda pale SUA (Moro) yuko Professor mmoja Ana mradi mkubwa wa hii kitu na anapiga hela ndefu sana atakupa muongozo wa kila kitu usitegemee ushauri wa hapa JF tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ushindani si mkubwa sana
1.Nikupe hongera kwanza kwa kutaka kujiajiri ila nikupe dokezo na Tahadhari hapo kwa usimamizi lazima mwenyewe uwepo nikimaanisha uwe na usimamizi wa karibu zaidi.

2. Kuhusu nyama nunua tu vingunguti ama ukonga km unaishi Dar es salaam kg machinjion 4,500 mpaka 5,000 unaweza pata connection na gari yaan wasambazaji nyama kwa gari wakakuletea mpaka ulipo.

Kwa upande wa samaki nenda ubungo River side sato kg 8,000 na sangara 4,500 kwa kg km ukizoea utapata connection ya wauzaji wanaoleta mojakwamoja huwa wanauza

Sato 5,500 sangara 4,000 note hizi bei ni za jumla rejareja Sato 10,000 kwa kg na Sangara 8,000 nyama rejareja 6,000 sehemu zengine 7,000

3. Ushindani sio mkubwa ila vyema ukawa na Machine ya kukatia nyama, ofisi layout iwe nzuri, Muuzaji awe mchangamfu hapo utakuwa umewapa pigo washindani wako.

4. Faida nafikiri ushajua kwa nyama faida 1,000 kwa kg kwa samaki Sato ni 2,000 km unanunua riverside sangara 3,500 kwa kg Hasara zipo nazinakuja kutokana na miundo mbinu ukikatika umeme jua nimaafa

5. Changamoto zipo nyingi sana kwanza ukikosea kuchagua eneo yaani ukifail kuchagua location ya ofisi yahiyo butcher basi jua ni hasara kwenda mbele, Pili wauzaji sipendi kuongelea vibaya watani wangu wagogo ila usije kumueka Mgogo buchani kwako kama huna usimamizi wa karibu atakufilisi nasema tena atakufilisi kuepuka hilo tafuta machine unaweza weka yoyote akauza. Usinambie kama nafanya lahasha namuona Kaka angu anavoendesha

Kama wewe ni mgogo utanisemehe jamani
Namna ya kujua vifaa muhimu unavyohitaji
Ili ujue ni kiasi gani kitahitajika fanya haya:-

1. Orodhesha vifaa vyote utavyohitaji kuwa navyo mf. Cutting machine, freezer (la kuhifadhia nyama iliypbaki ili isiharibike), mzani , fan (hii inasaidia kufukuza nzi, mteja akija akakuta mazingira machafu manzi yamejazana kesho, hatorudi tena) n.k (hakikisha umelist vitu vyote muhimu)

2. Ulizia bei ya kila kifaa (tembelea kwa wauza bucha kwanza uwaulize ili wakupe estimate ya kila kifaa ili usilanguliwe pesa nyingi huko dukani wanapouza)

3. Baada ya hapo piga hesabu ya vifaa vyoote ulivyoorodhesha(+usafirishaji kutoka sehemu uliponunua mpaka kwenye frem), bila kusahau kodi ya frem (angalau ya miezi sita sio mbaya), mshahara kwa muuzaji (kama utakua umemuajiri mtu), umeme, n.k

Kwa kufanya hivi, utaweza kujua ni kiasi gani cha pesa kitahitajika. Hapa sijapigia hesabu za kufatilia leseni na vibali (sijui kama vipo/vinahitajika au lah), matengenezo ya fremu kuwa na hadhi ya bucha (mara nyingi huwa wanaweka aluminum door na tiles kufanya mazingira kuwa nadhifu na kuvutia wateja) n.k
 
Kwa hapa nilipo mimi wafanyabiashara wengi wa mabucha wanaenda ktk minada ya ng'ombe wananunua ng'ombe hupeleka machinjion kisha huuza mabuchani.
 
Mfano ng'ombe mnadani ni Tsh 400,000/=

Ng'ombe labda ana wastani 200kg

bei ya nyama buchani tsh6000 kwa 1kg

6000mara 200=Tsh 1,200,000/

Endapo utauza ngombe mmoja kwa siku faida ni laki 8.
 
Kwa hapa Dar sijuhi hii biashara ikoje, I mean in small scale,Tofauti na Kununua ngombe mzima and kuuza nyama, Just for business of 60Kg and below.
 
Tunazungumza nyama ikiwa buchani.

Okey. Ng'ombe wa kilo mia mbili hawezi kuuzwa kwa laki NNE, ng'ombe mwenye kilo mia mbili za nyama sio ng'ombe wa kawaida hasa kwa hizi breed zetu za kawaida.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Okey...ng'ombe wa kilo mia mbili hawezi kuuzwa kwa laki NNE,ng'ombe mwenye kilo mia mbili za nyama sio ng'ombe was kawaida hasa kwa hizi breed zetu za kawaida
Usisema haiwezekani bwana,kwani bei za minada yote Tanzania ni moja?

Mnada wa Meserani Arusha unanua kwa bei hiyo. Usibishe
 
  • Thanks
Reactions: amu
Back
Top Bottom