Ushauri: Wapinzani mngeendelea na shughuli nyingine ya CCM muwaachie wana-CCM

utukufu mwanjisi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
2,830
2,417
Habarini hapa jukwaani

Katika mnyukano ambao unaendelea katika mitandao ya kijamii kati ya watu ambao wamewahi kushika nyadhifa kubwa katika Chama Changu cha Mapinduzi, ambapo ni ndugu Humphrey Polepole na Ndugu Nape Nnauye. Ni kili kwamba hakuna jambo ambalo linatokea kwa bahati mbaya katika Chama chetu narudia tena hakuna.

KABLA ya kuendelea, lazima niwaambie ya kwamba ninaeandika hii thread hapa ni Mwana CCM ASILIA na sijawahi kuogopa kusema hivyo hata kipindi cha Mwenyekiti wangu aliefariki hapo karibuni, ukitaka kulijua hilo pitia thread zangu zote zilizopita hapo awali.

TUENDELEE, wengi wenu hapa jukwaani na huko mitandaoni mmemuona ndugu Nape kama amekosa busara katika mchakato mzima wa kitu kinachoendelea kwa sasa kwa chama chetu, lakini niwe wazi kuwa Nape anajua nini anakifanya na mnayoyaona leo kipo katika mahesabu na mikakati ya hapo mbeleni.

HIVYO, nilitaka kuwashauri tu kuwa ndugu wapinzani mngeendelea na shughuli zingine maana ngoma inayochezwa na watu wa CCM kwenu nyinyi ni kubwa sana na hamtaweza kujua midundo yake abadani hata tuliomo ndani ya chama baadhi ya midundo inatushinda, sasa mtaiweza nyinyi mlio nje ya chama.

CCM NI DUBWANA KUBWA LINAJUA NINI LINAKIFANYA NA KWA WAKATI GANI.
 
Asante kwa ushauri ila hatuwezi kuyanyamazia yaliyowaumiza wa Tanzania kwani nasi ni watanzania pia tena wazalendo, tunataka wajue tunajua na tulijua yote waloyotufanyia na waliyowafanyia Watanzania.
 
Huna akili.Kwa adui yako moto ukiwaka unapaswa ukaongeze petroli au uendelee na shughuli nyingine?
Mchezo unaochezwa hamuwezi kuulewa ndio maana kila siku CCM wanawapigia ngoma na nyinyi ni kucheza tu bila kujiuliza mara mbili mbili
 
Asante Kwa ushauri ila hatuwezi kuyanyamazia yaliyowaumiza wa Tanzania kwani nasi ni watanzania pia tena wazalendo, tunataka wajue tunajua na tulijua yote waloyotufanyia na waliyowafanyia watanzania.
Na wewe ni mpinzani?
 
Habarini hapa jukwaani

Katika mnyukano ambao unaendelea katika mitandao ya kijamii kati ya watu ambao wamewahi kushika nyadhifa kubwa katika Chama Changu cha Mapinduzi, ambapo ni ndugu Humphrey Polepole na Ndugu Nape Nnauye...
Kwanini na wewe usiganye shughuli nyingine kuliko kuiwaza Chadema muda wote?
 
Back
Top Bottom