Ushauri wangu wa bure tu kwa Wanaharakati na Wapenda Siasa na Demokrasia za 'hovyo hovyo' Barani Afrika

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,052
2,000
Ukiamka Asubuhi mshukuru Mwenyezi Mungu wahi ama Kazini Kwako au Ofisini Kwako kapige Kazi ili ujipatie Pesa za Kuiendeleza Familia yako.

Siasa za Barani ( sina uhakika na za Tanzania kwakuwa siishi huko ) nyingi zimejaa tu Chuki, Unafiki, Fitina na ukicheza vibaya tegemea Kutekwa au Kubambikiwa Kesi na hata Kuteswa vilivyo hadi ukome..!!

Siasa na Demokrasia za Afrika ( sina uhakika na Tanzania kwakuwa sipo na siishi huko ) ni za 'Kukomoana' huku Wewe ambaye umejitolea Kuwapigania Watu ikitokea ukakamatwa Waafrika wale wale waliokuwa wakikuvimbisha Vichwa na kukupa Jeuri watakuacha uhangaike na hadi uteseke peke yako.

Siasa za Barani Afrika ( sina uhakika na za Tanzania kwani sipo na siishi huko ) ni kwamba unaweza ukajiona unapendwa zaidi na Waafrika wa Mitandaoni ( siyo JamiiForums ) nawe ukawaamini na kujawa na Kiburi ila pale likija kukupata la kukupata hakuna atakayehangaika nawe ukiwa ama Mahakamani au Gerezani sana sana hawa hawa 'Waafrika' watakua wanakucheka tu na Kukuona Bonge la Pimbi.

Waafrika tujikite zaidi katika kuwa Wabunifu, Kufanya Kazi kwa bidii na tuzaane sana tu na tujiletee Maendeleo yetu ila kujifanya tu nawe unataka Kupambana na Serikali ( Dola ) hasa kwa nchi hizi za Barani Afrika zenye Marais ( Viongozi ) wengi goi goi na wa hovyo hovyo ni kujitafutia ama Kutekwa, Kupigwa, Kuteswa,Kusodomiwa na Kugomolewa au hata ikibidi utauwawa au kuwekewa Sumu na hata Kubambikiwa Kesi Kubwa zisizo na Dhamana ili kuwatisha wengine wasithubutu Kukuiga au hata Kushoboka nawe.
 

chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,936
2,000
siasa nyingi zimejaa ulimbukeni, hasa za hao wenzetu maDJ ambao wanapiga kelele kwamba leo wapo segerea, hawajui wanakotoka, hawajui wanakoenda, wao wakifadhiliwa tu na mzungu hao mtaani na wanaamini mzungu atawatetea, kumbe mzungu yupo kwaooo, virungu wanapigwa wao. sawa na Tundu sasaivi anahamasisha wenzake wafanya fujo wakati yeye anakunywa bia ubelgiji na alipomaliza tu uchaguzi alikimbilia ubalozi wa ujerumani akawaacha wapiga kura wake hawajui waende nchi gani. wamekuja kustuka kumbe nchi yao ni hiihii ambayo Tundu anaichafua, hawana kwa kwenda, na bado wapo hapahapa hadi sasa.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,052
2,000
Umeandika kwa ushujaa na uwoga mkubwa. Hongera.
Mkuu nipo hapa nchini Somalia na yanayoendelea hapa ni makubwa hasa kwa Wanasiasa na Wapenda Demokrasia hadi natamani nirejee zangu Tanzania kwenye Siasa safi na Demokrasia ya kweli.

Kwa Mfano hapa nchini Somalia kuna Mwanasiasa Mmoja wa Upinzani anaitwa Manfree Alqaelida Wembo alishawahi hata kuwa Mbunge wa Jimbo Tajiri la Hargaesa na kinachompata sasa nadhani akitoka huko aliko Gereza Kuu la Aregese hatotamani tena kuendelea na Siasa zake za Kidemokrasia na Kiuanaharakati.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,120
2,000
Wengine tupo tayari kwa lolote kufungwa kuteswa ni sehemu ya maisha yetu.

Wewe nenda utafute hizo pesa halafu tusikusike ukija hapa kulalamika tozo na kodi 18 za mafuta.

Sitanyamaza Mimi never labda nikiwa kwenye futi 6.
 

HOPECOMFORT

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
3,232
2,000
Kwahiyo tumuache Madilu atupangie anavyo taka!?!? Tumsikilize Gwajima au nani??! Hata Mungu apendi unafiki....Haki huinua taifa
 

bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,645
2,000
Kwani ndugu yangu unafikili utaishi milele hapa duniani? Wote tunapita tu, hata ukikaa kimya basi hukohuko madhara yatakufwata na kukuangamiza kabisa
 

Ti Go

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
688
500
Gentamycine, ulichoandika kipo mawazoni kwangu kuwa walipoondoka wakoloni waliacha watawala wa kiafrika ambao wametengeneza aina mpya ya ukoloni ambao unahitaji mapambano mapya ya kuondoa mkoloni - mwafrika. Kama vile ilivyokuwa mgumu kumwondoa mkoloni- mzungu itakuwa mgumu pia kumwondoa mkoloni- mwafrika.

Hebu angalia afrika yote ilivyo. Watawala waliopo madarakani hawataki kutoka, wengine Wanabadirisha ndani kwa ndani kwa kofia ya chama kile kile.

Kama ilivyokuwa kwa baadhi ya waafrika wenzetu wakiungana na wakoloni-wazungu, ona hata sasa waafrika wachumia matumbo wako nyuma ya wakoloni-waafrika.
Never surrender, aluta continua
 

Wilhelm Johnny

JF-Expert Member
Jan 13, 2016
936
1,000
kumtetea mwafrica ni kazi sana haswa tanzania wakati unampigania anakushangilia ila yakikukuta wanakutizama tu. Kama umepata nafasi ni heri kuwa vuguvugu tu unangata na kupuliza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom