Ushauri wangu wa bure tu kama unajijua/ukijijua kuwa wewe ni ama Mwanaharakati au Mpingaji wa Mamlaka

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,401
2,631
1. Acha Kuwaamini kwa 100% wale Watu wanaojifanya ni wa karibu Kwako.

2. Tumia ID iliyo anonymous na siyo ile ambayo inakutambulisha Kiuhalisi na wengi wanaijua.

3. Acha kupenda hovyo Wanawake au Wanaume kwani kwa 100% hao ndiyo watatumika Kukumaliza.

4. Hakikisha Mizunguko yako yote ya Siku uwe unaijua Wewe tu na ikiwezekana iwe ni ya Zig Zag Style.

5. Ukiona kuna Watu wanakusifia na kukupongeza kwa uanaharakati wako waangalie mara mbili mbili.

6. Wa Kumkaribisha Kwako awe ni Mama au Baba yako tu kwani Ndugu / Marafiki wengine hutumika.

7. Ukijua unaviziwa ama toa Taarifa kwa Watu mapema na ikiwezekana piga Picha Matukio yote.

Tuwe makini sana na nasisitiza tena tuwe makini mno na namalizia kusisitiza kuwa tuwe makini zaidi Maadui zetu hawalali 24/7.
 
Ila anawapambazua nyie werevu?
Hivi pale pembeni ya Mdude kwenye ile picha akiwa na pingu mahakamani umemuona kigogo 2014?
Umemuona Mange?
Umemuona Zitto?
Umemuona Mbowe?
Umemuona Mdee??
Umemuona Lema?
Umemuona Fatuma karume?
Umewaona wale wafuasi wake waliokuwa wana like matusi yake?

Nauliza umewaona hao wakimsaport ndugu Mdude nao wakiwa wamefungwa pingu pamoja nae?

Umeona hata maandamano ya watu 5 tu kumsapot ndugu Mdude?

Tafakari sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu serikali ikitaka kukumaliza ina njia nyingi tu huko nyuma enzi za Raisi Mwl.Nyerere ukionekana much know na utawasumbuwa mahakamani wanakuja saa nane usiku kwamba kaaege mke wako unapelekwa detention yaani kizuizini kwa kipindi maalumu kama miaka saba lakini baadhi wanaombewa msamaha wa mkakati na familia zao au rafiki zao wanafunguliwa.
 
Hivi pale pembeni ya Mdude kwenye ile picha akiwa na pingu mahakamani umemuona kigogo 2014?
Umemuona mange?
Umemuona zitto?
Umemuona mbowe?
Umemuona mdee??
Umemuona lema?
Umemuona fatuma karume?
Umewaona wale wafuasi wake waliokuwa wana like matusi yake?

Nauliza umewaona hao wakimsaport ndugu mdude nao wakiwa wamefungwa pingu pamoja nae?

Umeona hata maandamano ya watu 5 tu kumsapot ndugu mdude?

Tafakari sana!

Sent using Jamii Forums mobile app

Itachukua muda mrefu Ndugu Kueleweka ila Watu tunatakiwa kuwa makini kuliko tena hasa kwa mwaka huu muhimu 2020.
 
Back
Top Bottom