Ushauri wangu wa bure kwa Commander in Chief Rais Dkt. Magufuli

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,466
108,621
Najua kwamba muda wowote utafanya 'uteuzi ' wako wa kujaza nafasi za Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na Mkuu wa JKT baada ya ' Makamanda ' waliotukuka akina Mwakibolwa na Isamuhyo Kustaafu rasmi jana kwa mujibu wa Sheria za Kiutumishi / Kijeshi.

Amiri Jeshi Mkuu wangu na Rais wangu Kipenzi kabisa hujawahi kuniangusha kwa kila ninayokuomba au kukushauri humu JamiiForums na najua kuwa hata threads na posts zangu karibia nyingi tu huwa unazipitia na naambiwa huwa unavunjika nazo mbavu sana na nasubiri tu nami siku moja unialike nije nikae nawe hapo Jumba Jeupe ili tuzungumze mengi huku tukiwatizama hao Ndege wazuri Tausi ambao huwa nawapenda mno hasa pale wakiwa wanalia na huo ukimya uliopo hapo.

Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu wangu Rais Dkt. Magufuli nakuomba sana usifanye makosa wala kupoteza muda wa kufikiri sijui ni nani anapaswa Kuwarithi hao ' Majemedari ' waliostaafu JWTZ badala yake nakuomba ' uteuzi ' wako kuziba nafasi zao utokee katika moja tu ya hii Mikoa tajwa hapa chini

  1. Tabora
  2. Mara
  3. Iringa
  4. Mbeya
  5. Mwanza
  6. Kigoma
  7. Ruvuma
Kisaikolojia tu ni kwamba Watu ambao ni ' Mashujaa ' wa Kuzaliwa kwa hapa nchini Tanzania na ambao nina uhakika tena wa 100% kwamba wataweza kuziba kwa ufanisi kabisa nafasi za ' Majemedari ' akina Mwakibolwa na Isamuhyo wanatoka katika hiyo Mikoa yangu ya ' Kutukuka ' saba ( 7 ) niliyoitaja hapo juu hivyo naamini hutofanya makosa na kama kawaida yako mawazo ya / ushauri wa GENTAMYCINE utauchukua na kuufanyia Kazi kwani sijawahi Kukoesea katika Kukushauri na ndiyo maana napata hata moyo wa kuzidi Kukushauri.

Nawasilisha.

Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki GENTAMYCINE
 
Mabeyo kwa uzoefu na miaka yake mingi jeshini tayari ameshamshauri Amiri jeshi mkuu yupi azibe nafasi zilizoachwa

Kwahiyo ushauri wako peleka kwenye vijiwe vya wauza magazeti
 
Acha kutuletea ukanda wewe.

Yeyote mwenye weledi na uzalendo ateuliwe bila kujali dini yake, kabila lake, wala rangi yake.
 
Najua kwamba muda wowote utafanya 'uteuzi ' wako wa kujaza nafasi za Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na Mkuu wa JKT baada ya ' Makamanda ' waliotukuka akina Mwakibolwa na Isamuhyo Kustaafu rasmi jana kwa mujibu wa Sheria za Kiutumishi / Kijeshi.

Amiri Jeshi Mkuu wangu na Rais wangu Kipenzi kabisa hujawahi kuniangusha kwa kila ninayokuomba au kukushauri humu JamiiForums na najua kuwa hata threads na posts zangu karibia nyingi tu huwa unazipitia na naambiwa huwa unavunjika nazo mbavu sana na nasubiri tu nami siku moja unialike nije nikae nawe hapo Jumba Jeupe ili tuzungumze mengi huku tukiwatizama hao Ndege wazuri Tausi ambao huwa nawapenda mno hasa pale wakiwa wanalia na huo ukimya uliopo hapo.

Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu wangu Rais Dkt. Magufuli nakuomba sana usifanye makosa wala kupoteza muda wa kufikiri sijui ni nani anapaswa Kuwarithi hao ' Majemedari ' waliostaafu JWTZ badala yake nakuomba ' uteuzi ' wako kuziba nafasi zao utokee katika moja tu ya hii Mikoa tajwa hapa chini

  1. Tabora
  2. Mara
  3. Iringa
  4. Mbeya
  5. Mwanza
  6. Kigoma
  7. Ruvuma
Kisaikolojia tu ni kwamba Watu ambao ni ' Mashujaa ' wa Kuzaliwa kwa hapa nchini Tanzania na ambao nina uhakika tena wa 100% kwamba wataweza kuziba kwa ufanisi kabisa nafasi za ' Majemedari ' akina Mwakibolwa na Isamuhyo wanatoka katika hiyo Mikoa yangu ya ' Kutukuka ' saba ( 7 ) niliyoitaja hapo juu hivyo naamini hutofanya makosa na kama kawaida yako mawazo ya / ushauri wa GENTAMYCINE utauchukua na kuufanyia Kazi kwani sijawahi Kukoesea katika Kukushauri na ndiyo maana napata hata moyo wa kuzidi Kukushauri.

Nawasilisha.

Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki GENTAMYCINE
Unaangalia historia ya kina mkwawa na mirambo au ni ubaguzi na dharau kwa mikoa mingine?
 
Back
Top Bottom